Hili la kuwaajiri graduate wa miaKa hii na kuwaacha wa miaKa ya nyuma sana limekaaje?

Hili la kuwaajiri graduate wa miaKa hii na kuwaacha wa miaKa ya nyuma sana limekaaje?

Duh,tokea 2014 degree yako si itakua imeshaevaporate.

Kigezo cha kumwagwa ni kwamba kweli umesoma ila elimu yako ni ya muda mrefu sana,ni outdated

Suluhisho:Kapige hata masters au postgraduate diploma ui-upgrade uwe up to date
 
Nimekuwa nikifuatiria wahanga mbalimbali wa ajira za serikali, moja ya jambo linalonishangaza ni kuona wahitimu wa vyuo wa miaKa hii yaani 2020 mpaka 2024 wengi wao wakipata ajira za serikali kwa wingi zaidi ukilinganisha na wale waliomaliza vyuo kwa miaka 2014 mpaka 2021 je kigezo kinachotumika ni kipi hasa! Nadhani wakuu mnaweza kuwa na majibu kuhusu hili.
Wanamini wa zamani mmeanza kujitegenemea na ujasiriamali!Haiko poa.
 
Wazamani nendeni Kwanza VETA sw.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Duh,tokea 2014 degree yako si itakua imeshaevaporate.

Kigezo cha kumwagwa ni kwamba kweli umesoma ila elimu yako ni ya muda mrefu sana,ni outdated

Suluhisho:Kapige hata masters au postgraduate diploma ui-upgrade uwe up to date
Anaitoa wapi hio pesa ya kulipia Ada ya masters
 
Katika makosa awamu ya tatu ilifanya ni kubadili vyuo vya diploma vitoe degree; Badala ya kujenga vyuo vikuu vipya kama kulikuwa na Ulazima.
Hii ilifanya tuende kinyume na mfumo wa Elimu ambao siku zote ni Piramid; diploma wanakuwa wengi sana, wakifuata degree na wachache master na phd. Sasa sisi tukajikita kuongeza degree na kuacha Diploma (wazalishaji); Ulimwengu wa tatu unahitaji wazalishaji....na hii itatutesa sana!
 
Kuna mpwa wangu alimaliza chuo mwaka 2022 kwa ngazi ya diploma kada ya ualimu alisoma mchepuo wa EGM kapangiwa tayari ajira lakini Kuna jamaa zangu wamemaliza vyuo miaka ya 2014 mpaka 2017 kwa mchepuo huohuo bado wanasota Mtaani hii inanishangaza kidogo.
INTA - VIYUUUU …jamaa zako waambie muda wa vya kunyonga umepita sasa ni kupambana , wanahitajika walimu BORA na sio BORA walimu
 
Back
Top Bottom