Kwa utaratibu wa haya makanisa yetu makubwa Kuna vigezo unatakiwa uvifikie ndo upate huduma Yao ya kiroho, hata kama umekufa kama hujafikia vigezo vyao hata huduma ya mazishi hupati
Najiuliza tu, hivi hii Misa ya kuwakumbuka waliofariki October 29 inawahusu waliokua waumini kamili au hata wasiokua waumini, kama tunawaombea wasio waumini ni unafiki tu, hivi mtu asie muumini akiuawa na police kwa kuonewa utaratibu wa kanisan unaruhisu kuzika.kama hauruhusi unawezaje kumfanyia Misa ya kumbukumbuk
Me nadhani Kuna kitu zaidi ya vile Vifo
Hivi kuna mzazi anaweza kumhamadisha mwanae aende aende akaandamane kweli
Kanisa linaweza kuombea mtu yeyote aliyedhulumiwa haki ya kuishi.
Kanisa lina haki ya kuamua nani linaweza kumuombea na nani haliwezi kumuombea. Hii ni sehemu ya uhuru wa kuabudu.
Na wewe unaweza kuanzisha kanisa lako ukagoma kuombea watu usiotaka kuwaombea, hiyo ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu ya uhuru wa kuabudu na kujiamulia mambo.
Yani ni hivi, wewe ambaye huna mamlaka katika kanisa, huna haki ya kulipangia kanisa limuombee nani na lisimuombee nani.
Kimsingi hii ni sehemu ya kukaa na wanyonge, walioonewa. Kanisa halishindwi kutafuta aya za kuhalalisha hilo. Kila siku kanisa linaombea watu mamilioni ambao hata si waumini, walio katika vita, njaa, magonjwa, etc.
Pia, kanisa ni sehemu ya siasa, hii ni namna yake ya kuonesha kuwa halikubaliani na mauaji yaliyotokea, kwamba wale waliouawa ni watu, wanastahili dignity ya utu.
Kingine, misa hizi ni zaidi ya kuombea waliofariki/waliouawa, misa hizi ni sehemu ya collective public grief therapy, kisaikolojia zinapunguza machungu ya waliobaki, kwa hiyo namna nyingine ya kuziangalia si kama misa za kuombea waliouawa, ni misa za kuwapoza machungu waliobaki hai.
Wazazi wanahamasisha watoto wao waandamane dunia nzima, na wao wanaandamana.
Ila tatizo wewe uko Tanzania huijui dunia, ukiandamana unauawa, unaona kuandamana ni jambo la hatari.
Wakati kuandamana ni haki ya kikatiba na kibinadamu.
Tanzania watu wamenyimwa uhuru mpaka haki ya kikatiba na kibinadamu inaonekana jambo la hatari.