PostGE2025 Hili la kuwaombea marehemu wa Oktoba 29 linanitafakarisha sana

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nimetangulia kusoma kabla ya kuangalia mchangiaji!! Kumbe ni lile ibilisi shetani BIG SHOW! haishangazi kwa mwendawazimu mwenye roho ya shetani kama BIG SHIW kuweka comment kama hii!
KANISA KATOLIKI Lina Chuki na Samia

Na simply because she’s Muslim

Hawana hoja yoyote zaidi ya hiyo
 
wewe baki na akili zako za kuvukia barabara vitu vingine vimekuzidi AKILI
 
Wewe nawe ni mpumbavu tu. Kwa hiyo kuna ubaya gani kuombea watu wote, hata kama unataka kufanya ubaguzi, utaseparate vipi hayo maombi kuwa haya yaende kwa wanaostahili na yasiwafikie wasiostahili
 
Kanisa linaweza kuombea mtu yeyote aliyedhulumiwa haki ya kuishi.

Kanisa lina haki ya kuamua nani linaweza kumuombea na nani haliwezi kumuombea. Hii ni sehemu ya uhuru wa kuabudu.

Na wewe unaweza kuanzisha kanisa lako ukagoma kuombea watu usiotaka kuwaombea, hiyo ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu ya uhuru wa kuabudu na kujiamulia mambo.

Yani ni hivi, wewe ambaye huna mamlaka katika kanisa, huna haki ya kulipangia kanisa limuombee nani na lisimuombee nani.

Kimsingi hii ni sehemu ya kukaa na wanyonge, walioonewa. Kanisa halishindwi kutafuta aya za kuhalalisha hilo. Kila siku kanisa linaombea watu mamilioni ambao hata si waumini, walio katika vita, njaa, magonjwa, etc.

Pia, kanisa ni sehemu ya siasa, hii ni namna yake ya kuonesha kuwa halikubaliani na mauaji yaliyotokea, kwamba wale waliouawa ni watu, wanastahili dignity ya utu.

Kingine, misa hizi ni zaidi ya kuombea waliofariki/waliouawa, misa hizi ni sehemu ya collective public grief therapy, kisaikolojia zinapunguza machungu ya waliobaki, kwa hiyo namna nyingine ya kuziangalia si kama misa za kuombea waliouawa, ni misa za kuwapoza machungu waliobaki hai.

Wazazi wanahamasisha watoto wao waandamane dunia nzima, na wao wanaandamana.

Ila tatizo wewe uko Tanzania huijui dunia, ukiandamana unauawa, unaona kuandamana ni jambo la hatari.

Wakati kuandamana ni haki ya kikatiba na kibinadamu.

Tanzania watu wamenyimwa uhuru mpaka haki ya kikatiba na kibinadamu inaonekana jambo la hatari.
 
Siwafichi ndugu zangu
Kwa akili kama hizi CCM itaongoza nyumbu hadi mwisho wa dunia

What happened on October 29 was a state sponsor mass genocide, The govt hire mercenaries from country X na taarifa za kuingia kwao, makontena ya silaha za maangamizi zote zilikuwa wazi kumaanisha walipanga kuuwa

Either ways you cannot justify killing your own citizens to stay in Power

Poleni sana watanzania, we have a long way to go as a country.
 
Hata wewe Kiranga unajua habari za kanisa,wewe si ni Atheist?

Au umeungana na Wanaharakati mkidai Tanganyika yenu😂
 
Mkuu bora hata umeelezea
Ashakum si matusi ila Tanzania tuna watu wanaulewa mdogo sana wa mambo

Kwa tuliowahi tembea na kuishi nchi tofauti tunaelewa, kuna nchi watu wanaandamana karibia kila mwezi kwa agenda tofauti tofauti ikiwemo kuishinikiza serikali na hatuoni mass killings

Ila kibongo bongo kuandamana tunashaaminishwa ni ugaidi na wanaoandamana wanaonekana waharifu

We have a long way to go as a country
 


Hii imeenda.....
 
Yumkin Kanisa Kotoliki limevamiwa na Pepo chafu la Chuki

Wangemuomba tu Mwamposa akayapunge mashetani mapepo yote
Kabla Kanisa kukimbiwa na Waumini wake muhimu wasiopenda alakati alakati !!!!!!

Matendo yasasa ya Kanisa katoliki ni sawa kabisa na Matendo ya baadhi ya Misikiti miaka ya 2000+

Hasara kubwa zilipatikana
sababu
kilichotokea baadhi ya Waumini wake muhimu
kukimbia Misikiti yenye alakati alakati

Mpaka leo kuna Waumini baadhi ya Misikiti wanaipita kusali ijumaah !!!
kukwepa mambo ya alakati alakati kukimbizana na Mapolisi ✍️
 
Hata wewe Kiranga unajua habari za kanisa,wewe si ni Atheist?

Au umeungana na Wanaharakati mkidai Tanganyika yenu😂
Kujua habari za kanisa ni sehemu ya cultural intelligence.

Kanisa ni sehemu ya utamaduni wa dunia, mtu hawezi kuwa msomi anayeijua dunia bila kujua habari za kanisa.

Pia, mimi kama atheist, hata ninapolikosoa kanisa, ni muhimu na vizuri nilikosoe kanisa wakati nalijua, kwa sababu kulikosoa wakati nalijua ndiyo kulikosoa kwa weledi.

Sasa ulitaka atheist nilikosoe kanisa kijinga wakati silijui?

Zaidi, mimi najua mambo mengi ya dini kuliko kanisa tu. Najua faksafa pia, utaona natumia logical fallacies sana kuhoni mambo.

Hivi karibuni nilikuwa natoa somo la kuweza kuishi kwa amani katika dunia yenye mambo mengi yanayosumbua akili, kwa kutumia masomo yaliyomo katika Buddhism na Dhammapada kuhusu equanimity.

Kwa hiyo najua mengi, si habari za kanisa tu. Ila hapa mada ni habari za kanisa, ndiyo maana ninechangia habari za kanisa.

Kuhusu kudai Tanganyika yetu, lete ushahidi kwamba nimedai Tanganyika yetu acha kuharisha ujinga tu hapa.
 
"Hivi karibuni nilikuwa natoa somo linalohusu kuishi Kwa Amani"

Hii sentensi nimeinukuu kutoka kwenye quote yako,sasa kama ulitoa somo kuhusu Amani ,unawazungumzia vipi wanaopangq kuvuruga Amani.

Mfano tutakinukisha,n.k
 
Tanzania ina watu wajinga wengi sana.

Nilikuwa naangalia takwimu kuna sehemu huko literacy rates zipo under 75%

Maana yake kuna mikoa mtu mmoja kati ya wanne hawajui kusoma na kuandika.

Na hata wanaojua kusoma na kuandika wengi hawawezi logical thinking, hawawezi critical thinking, hawajui abstract thinking, hawajui Kiingereza hivyo dunia yao inaishia kwenye Kiswahili, na hata hicho Kiswahili chenyewe hawakijui vizuri. Hawajatembea kuona dunia, hata kwenye mtandao hawajui mengi. I suspect hawajui chochote cha maana vizuri kwenye lugha yoyote.

Na kwa vile tumerahisisha watu kuoata mitandao, wengine ndio hawa tunakumbana nao JF.

Semi literate unwashed country bumpkins.

You can tell by how they think, the limit of their world.

Now, I don't have a problem with ignorant semi literate countty people per se. I really don't. Some of the most respectful and humble people are from this bunch.

They are our country cousins, literally. We can educate each other. Sometime they can even educate me about their country ways.

I don't even have a problem with loud argumentative obnoxious country people, if they know what they are talking about and can educate me.

I have a problem with semi literate unwashed country bumpkins who are loud argumentative and obnoxious.

These I have no time for.

Because they can't be taught anything, they can't teach me anything.

There is no point engaging them.
 
"Hivi karibuni nilikuwa natoa somo linalohusu kuishi Kwa Amani"

Hii sentensi nimeinukuu kutoka kwenye quote yako,sasa kama ulitoa somo kuhusu Amani ,unawazungumzia vipi wanaopangq kuvuruga Amani.

Mfano tutakinukisha,n.k

(Soma kwa sauti ya Tundu Lissu)

Kwanza kuvuruga amani ni nini?

Amani ni nini?

Tanzania kuna amani sasa hivi?

Tanzania kulikuwa na amani kabla ya October 29 2025?

Unafahamu tofauti ya amani na utulivu?

Sehemu yenye uonevu mwingi, kwa nini amani iwe kipaumbele zaidi ya mapinduzi?

Unaweza kumwambia mtumwa aliyefungwa minyororo asitake kufanya mapinduzi kwa sababu akifanya mapinduzi ataharibu amani?

Watu wamepotezwa, wametekwa , wameuawa, wameibiwa muda mrefu kabla ya October 29 2025. Hiyo nayo unaita amani?

Amani gani?
 
Kanisa hili katoliki tunajua tangu kipindi cha Dkt Slaa walikuwa upande wake lkn kuna kujificha kidogo wajingawajinga wenye uwelewa mdogo wasijue msimamo wa Kanisa Kotoliki

Lkn sasa kama ni Mapenzi basi ndio chongo kuitwa kengeza 😳😳

Mapenzi kikohozi 😳😳

Wameshindwa kuficha chuki zao kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Kitendo chao kimepelekea kinyume na matashi yao

Sasa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kajikuta anapokea msaada mkubwa pande nyingi zaidi kupambana na Wachochezi wake!!!

Sababu kiakili Kanisa limeshindwa kipropaganda zake
Kwanini wamechagua mapambano Sababu za msingi zipi

Kama Uchumi Taifa lipo vizuri
Kukusanya kodi huko kavunja record kabisa kutoka Trilioni 17 kufikia Trilioni 37 tofauti ya Trilioni 20

Ujenzi Taifa zima linajegwa Sekta zote

Kazi zaidi yeye ni mwenye kuajiri Watumishi wapya tofauti na Rip JPM
Na kupandisha madaraja kazini
Kuongeza mishahara ya Watumishi

Sasa Msingi wa Kanisa kumwandana ninini ‼️

Kwasasa Watanzania wengi sio Waislamu tu mpaka baadhi ya Wakristo wameshtuka
Wanamuunga mkono Rais wao
Kimya kimya
Kwasababu wamekosa msingi wa chuki za Kanisa Kotoliki 🤠

Kama yupo mwenye Sababu za msingi zenye mashiko kiakili na ki Hoja
atwambie nasisi tuungane kumchukia ❓❓
 
Kina nani wamepotea?

Wamepotezwa na nani,Kwa ushahidi upi?

Unajua nikwambie kitu mkuu,nchi siyo kama nyumba kwamba Baba au mama wanaweza kuwatambua watoto wao wote Kwa idadi ,majina na tabia zao.

Swala la nchi ni swala gumu kiuongozi na kiutawala,yaani unamuongoza mtu ambaye humjui hujawahi kumuona.

Na inapokea siku anakuja na matamko yasiyo na kichwa wala miguu.

Maneno kama tutavuruga uchaguzi.

Ni kweli ulivurugika wewe mwenyewe uliona na kusikia wapo Raia wema walikatwa vidole kisa Wana ule wino baada ya kupiga kura wapo waliopigwa mawe (wasimamizi katika vituo vya kupiga kura)

Halafu tutakinukisha.

Ni kweli vituo vya mafuta vingi vilichomwa ,magari ya watu ,biashara na wizi wote uliofanyika.

Haya yote yalifanywa na watoto wa masikini,ambao hawajui aliyetamka haya maneno ana kusudi gani.

Kumbe ni mtu ambaye yupo tayari kuuza nchi Kwa watu wa nje Kwa manufaa ya familia yake.

Mkuu Mimi ni social engineer naijua jamii na angle zake ,naujua uovu mwingi uliofanyika mwaka Jana
 
Hata walioandamana adhabu yao ilikuwa iwe mitutu ya kichwa??
 
Damu za waliotangulia zinawatesa sanaa ,dawa ni kukiri na kutubu hakika amani haitakaa ndani yenu kama unajua uliua,uliiba kura ,na unashabikia wenzetu kupigwa risas
 

Zingatia haya ndani ya Kanisa Katoliki:

1. Tarehe 1 Novemba kila mwaka ni Siku ya kuwakumbuka Jumuiya ya Watakatifu Wote walioko mbinguni (Triumphant Church community) waliokuwa waumini wa Kanisa Katoliki. Hawa wanatuombea.

2. Tarehe 2 Novemba kila mwaka ni Siku ya Kuwakumbuka JUmuiya ya Marehemu Wote walioko toharani (Repentant church community) waliokuwa waumini wa Kanisa Katoliki. Hawa tunawaombea.

3. Sisi tulioko duniani bado tukiwa hai ni jumuiya ya kanisa la wasafiri/mahujaji (Pilgrim church community). Tunaombewa na watakatifu walioko mbinguni, tunawaombea marehemu waliko toharani.

4. Kwa lugha ya kifalsafa, kusali ni kitendo cha kufanya tafakari ya kifikra (brainstorming) kuhusu haki zetu (soma: mkate wetu wa kila siku) na majukumu yetu kwa majirani zetu ((soma: mkate wao wa kila siku)) kwa kuyapima yote mawili kupitia kizio cha kimungu kilichoko kwenye misahafu.

Mengine yoye ni nyngeza, yaani cosmetic issues.

Hope umeelimika japo kidogo.
 
Haya mauaji utajaribu ku justify ili moyo wako uwe na amani ila ni ngumu mno kama ulihusika kupata aman huwez na hautokaa kupata amani ,utawaita hao marehem kila jina baya ukihis utapata amani ila hautopata hata kidogo ,ni Bora utubu na kukiri adharan kuwa palkua na makosa mengi ya kuua na kila mtu aliona walivyokuwa wakiuawa watu ovyoo ,,hata tufanyeje na kujarbu kujustify hivyo vifo Bado nafsi zetu zitatudai hata Dunia yote ikisema marehem walikua vibaka na waporaji Bado tuu nafsi zitatudai damu za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…