Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Shida ni kwamba, hata kama ukielezea vipi, maswali hayaishi.

Huu muungano mwishowe utakuja kufanywa kama dini. Ukiuliza asili yake ni dhambi au unakufuru.

Kuna maswali mengi sana lakini mwisho wa siku unaambiwa jibu hilohilo moja kwa maswali yote…

Kwamba Zanzibar siyo nchi.

Kuna shida kubwa sana.

Kuna viashiria vingi sana vinavyoonyesha tofauti na kauli zenu ndo maana hizi back and forth hazitaweza kwisha.
Ndiyo sababu uhai wa muungano wetu unategemea kulindwa kwa nguvu zote.
 
Ndiyo sababu uhai wa muungano wetu unategemea kulindwa kwa nguvu zote.
Uhai wake unalindwa kivipi?

Kitu kisichoeleweka utaweza kujilinda kwa usahihi?

Nguvu gani unazungumzia zitumike zote?
 
Tumeona picha ya ujumbe wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa katika kikao huko China unavibao viwili. Kimoja kimeandikwa Tanzania na zingine kina wajumbe wameweka Bangor akiwa kibao cha Zanzibar. Hizi ndio Sera ya Nchi yetu sasa, baada ya kupata Waziri Mpya wa Mambo ya Nje au ilikuwepo kabla. Na nini tafsiri yake kimataifa na ndani ya nchi

Pia soma:Nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar, kwanini Zanzibar ipo na sisi ni Tanzania bara, kwanini wasioitwe Tanzania Visiwani?
Uyaratibu ni kwamba, kama ni mkopo, Seriksli ya Muungano itaenda yenyewe kukopa halafu Zanzibar lazima wapate sehemu yao ya mkopo sababu Zanzibar ni sehemu ya Muungano, na Serikali ya Muungano ndiyo itakayolipa.
Kama ni msaada ni lazima ziende serikali zote mbili, ya Muungano na Zanzibar sababu Zanzibar ni nchi kamili hivyo inatakiwa ikachukue fungu lake, pia itatakiwa ipewe sehemu yake kwenye ule msaada uliochukuliwa na Serikali ya Muungano sababu zanzibar ni sehemu ya Muungano
 
Hakika. Miaka yote nimekaa Unguja na Pemba huo ndo msimamo wa wenyeji!
Sijui kwanini wadanganyika hawaamki usingizini!
Au ni Raha sana kuwa na koloni?
Wanasheria Mzee Warioba na wengineo wanaelea ndio maana wakaja na Muungano wa sirikali tatu.
 
Uyaratibu ni kwamba, kama ni mkopo, Seriksli ya Muungano itaenda yenyewe kukopa halafu Zanzibar lazima wapate sehemu yao ya mkopo sababu Zanzibar ni sehemu ya Muungano, na Serikali ya Muungano ndiyo itakayolipa.
Kama ni msaada ni lazima ziende serikali zote mbili, ya Muungano na Zanzibar sababu Zanzibar ni nchi kamili hivyo inatakiwa ikachukue fungu lake, pia itatakiwa ipewe sehemu yake kwenye ule msaada uliochukuliwa na Serikali ya Muungano sababu zanzibar ni sehemu ya Muungano
Jibu lako linahitaji tafakari kubwa Sana.
Kwenye mkopo ambao kuna kulipa Zanzibar haiendi maana sio nchi.

Kwenye msaada ambao hauna kulipa Zanzibar wanafuata mzigo wao maana ni nchi.
 
Jibu lako linahitaji tafakari kubwa Sana.
Kwenye mkopo ambao kuna kulipa Zanzibar haiendi maana sio nchi.

Kwenye msaada ambao hauna kulipa Zanzibar wanafuata mzigo wao maana ni nchi.
Katika serikali ya Jamhuri ya Muungano kuna Wizara za Muungano na kuna Wizara zisizo za Muungano.
Wizara za Muungano huwa zinafanya kazi pande zote za Muungano, hivyo huwa moja tu mfano Wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Wizara ya mambo ya nje n.k. Mawaziri wa Wizara hizi wanaweza wakatika upande wowote wa Muungano.

Kuna wizara zisizo za Muungano, hizi hufanya kazi upande mmoja tu Muungano. Mfano wizara ya ardhi, Kilimo, TAMISEMI, Elimu, Afya, Fedha.
Wizara hizi zanzibar pia wanazo zao kwa mifumo yao, sababu Zanzibar ni nchi kamiki na ili kuwa waziri katika hizo wizara ni lazima uwe Mzanzibar.
Pamoja na kwamba Wizara hizo siyo za Muungano, lakini kwa upande wa bara Mzanzibar naye ana haki sawa ya kuziongoza wizara hizi sababu ingawa si za Muungano lakini zipo kwenye serikali ya Muungano na Zanzibar ni sehemu ya Muungano na wao pia ni wa Tanzania na seriksli ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndivyo ilivyo kwa wakuubwa mikoa na wakuu wa wilsya.
Kwa Kifupi Muungano huu unamfanya Mtanganyika ainekane ni kubwa Junga lililoamua kuuza Uhuru wake na ndiyo maana hata viongozi hawana ile feeling patriotism sanabu nchi (Tanganyika) walishaiua, hawakuiunganisha, waliiua, huu siyo muungano.
 
Kwahiyo atatumia hayo majeshi kumlazimisha DC wa Zanzibar kutekeleza jambo ambalo amekaidi kulifanya! Basi sawa.
Mkapa akiwa rais aliingia pale Zanzibar akatandika kuanzia mesenja mpaka viongozi na amani abeid karume rais wao aliwepo na alikuwa kimya,
Usichezee mamlaka ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
Tumeona picha ya ujumbe wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa katika kikao huko China unavibao viwili. Kimoja kimeandikwa Tanzania na zingine kina wajumbe wameweka Bangor akiwa kibao cha Zanzibar. Hizi ndio Sera ya Nchi yetu sasa, baada ya kupata Waziri Mpya wa Mambo ya Nje au ilikuwepo kabla. Na nini tafsiri yake kimataifa na ndani ya nchi

Pia soma:Nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar, kwanini Zanzibar ipo na sisi ni Tanzania bara, kwanini wasioitwe Tanzania Visiwani?
Kiongezeke na cha Tanganyika hakina ubaya.
 
Mkapa akiwa rais aliingia pale Zanzibar akatandika kuanzia mesenja mpaka viongozi na amani abeid karume rais wao aliwepo na alikuwa kimya,
Usichezee mamlaka ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Nafikiri tunazungumza lugha tofauti,nikutolee mfano wa juzi tu hapo DC wa Longido alipozingua alitengua uteuzi wake mara moja sasa je ikitokea hali kama hiyo kwa DC wa Zanzibar anaweza kumtengua? Mimi sijazungumzia habari ya kupiga watu sasa naona unarukaruka kama maharage yanayochemka!
 
Mbona nilishakueleza mda tu, huyo namba moja wao tu anawajibika kwa mama ndio iwe dc?haijalishi ni wa longido au kusini magharibi wote ni mali ya mama, labda kichwa hapo juu imejaa tope au uji ndio uminyanie hili
Endelea kufrahisha baraza
 
Kumbe tunasumbuana muda wote na mtu mpumbavu! Hujui lolote.
 
Hivi ni vitu vidogo, kuna nchi nyingi kabla ya Muungano zilikuwa na ubalozi Tanganyika na ubalozi Zanzibar, baada ya Muungano, nyingi zilifunga balòzi zake za Zanzibar na kubaki za Tanganyika zilizogeuka za Tanzania, miongoni mwa nchi ambazo hazikufunga ubalozi wake Zanzibar ni pamoja na yale mataifa makubwa matano yenye veto UN, Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na China, India pia haikufunga, bali walizigeuza balozi hizo kuwa balozi ndogo. Nchi hizi zinai treat Zanzibar with a special treatment of autonomous, hivyo wakitoa mualiko Tanzania inàalikwa kama nchi Tanzania na Zanzibar inaalikwa kama autonomous part of Tanzania hivyo kila mtu na mwaliko wake na kibao chake, bali Tanzania kama nchi ni nchi moja tuu, JMT!.
P

Kuna watu wana vichwa vigumu sana kuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom