Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Iwapo katika orodha ya mambo ya Muungano kuna Wizara ya mambo ya Nje, basi hili tunaloliona ni wazi KATIBA haina thamani tena kwa watawala hawa.

Tuamke Watanzania
 
tunangoja samia hatoke madarakanii iwe kivyovyote vile then tunahitaji rais mtanganyika mwenye uchungu na tanganyika yake ndio tunazishe hiyo agenda ya kuvunja huo muungano....tutaona nani huwa anamtegemea mwenzake
Kwa kauli yako hii ina maana muda bado wa kuvunja muungano, na hivyo wewe ulihemkwa tu!!
 
Mkanganyiko uko pale pale lila na fila hazi..... wacha tu ikae hivyo hivyo .Watakuja wengine watawasha tochi kuona mwanga
Zanzibar ni Nchi na Taifa ila haina Dola

Ndio sababu ACT wazalendo wanapigania Mamlaka kamili
 
Nadhani kabla hatujajadili hili swala nilazima tujiulize kwanza kama hapo awali Zanzibar ilikua na kiti cha peke yake hapo UN? Na hapa simaanishi Zanzibar ya kabla ya muungano ila ni Zanzibar ya baada ya muungano.

Na kama kilikuwepo lazima tuhoji ni kwanini wanakua nacho ilihali sisi sote ni Tanzania?

Na kama hawakuwa nacho hapo awali hapa hata mimi napata hisia kwamba yawezekana hili nalo ni miongoni mwa ile migogoro ya kimuungano kwahiyo ulisolviwa kinamna hiyo ili kuendelea kuimarisha muungano wenyewe.

Kwasababu kimsingi wote tunajua kwamba huwa kunakuaga na hoja za mara kwa mara zinaibukaga na hoja hizi huwa zinakuaga na ukakasi wakati mwingine na mara nyingi huwa kuna upande unahisi kunyonywa kwahiyo inawezekana kwenye yale malalamiko ya kimuungano Zanzibar nao walitamani waweze kutambulika na kupata kiti cha uwakilishi kwenye eneo hilo.

Ila sasa ukiangalia hapo utaona kuna upande unapata faida mara mbili moja ni hiyo ya moja kwa moja na pili ni hiyo bendera ya Tanzania kwasababu Zanzibar iko ndani ya Tanzania kwahiyo yote yatakayo tolewa kwa jina la Tanzania basi automatically nayo lazima ijumuishwe na ili haki itendeke hapo tungesema bendera ziwe tatu kwa maana ya Tanzania, Zanzibar na Tanganyika au ziwe mbili kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar.

But...

All in all ni hekima tu ndio zinazolinda huu muungano ila ingekua kwa kufuata sheria na taratibu nadhani tusingefika hapa na nnadhani kati ya mambo yanayowaumiza kichwa viongozi wengi wakuu wa nchi hii ni hilo swala la kimuungano na namna ya kutatua migogoro yake pasi na kuathiri upande wowote ili kutimiza kile kiapo cha kuutunza na kuulinda muungano.
 
Duh!
Kwa hiyo awamu hii ya sa100 Zanzibar imekuwa na wizara yake ya mambo ya nje, au?
 
lakini hii dar uliyopo ni zanzibar!, unadhani mwalimu alikuwa mjinga!
Acha ujinga wewe chawa.
Wakati baba wa Zanzibar Field Marshal John Gideon OKELLO akipambana kuikomboa Zanzibar kutoka mikononi mwa Sultani, mzee Karume na mwenzie Kassim Hanga walikimbia kuja kujificha Dar es Salaam, Tanganyika
 
nchi ni 1 inaitwa JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ina serikali mbili.......(upo sawa mkuu)
NAJAZIA...
hapo kwenye uwakilishi hiyo zanzibar imewakilishwa kama serikali
so bila kujali nia yao ni nini,hapo kuna uwakilishi wa serikali ya TANZANIA(kama kuna faida itagwana bara na visiswani)
pia kuna uwakilishi wa serikali MAPINDUZI ZANZIBAR(kama kuna faida itaenda visiwani)
sina hakika kama kuna kosa kisheria serikali ya mapinduzi ikiwakilishwa hapo au popote
ni kama wanavyoamua kwenda (IMF) au (WB) kukopa ni sawa tu
NB: uchambuzi huo kama una makosa naruhusu kukosolewa na kusahihishwa
 
Mkuu Yohana, sijapata msaada kutoka kwako!
Nasubiri maoni kutoka kwa Broo Pascal Mayalla . Sijamsoma kwenye uzi huu.
Mwishoe nitaenda kujiridhisha kwa Mzee Warioba, au Mzee Butiku, kama hili lipo sawa!
 
Halafu watanganyika walivyowapumbavu wao kibao chao wanaandika Tanzania badala ya Tanganyika.kiufupi viongozi wa Tanganyika ni majuha na majinga.safi sana Zanzibar Kwa kujitambua.ikiwezekana na umoja wa mataifa iwe hivohivo.Muungano wa kijinga kama huu ni kichaa tu ndiyo anaweza kuupenda
 
Adui wa Tanganyika na Zanzibar huru ni CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…