Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Tumeona picha ya ujumbe wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa katika kikao huko China unavibao viwili. Kimoja kimeandikwa Tanzania na zingine kina wajumbe wameweka Bangor akiwa kibao cha Zanzibar. Hizi ndio Sera ya Nchi yetu sasa, baada ya kupata Waziri Mpya wa Mambo ya Nje au ilikuwepo kabla. Na nini tafsiri yake kimataifa na ndani ya nchi

Pia soma:Nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar, kwanini Zanzibar ipo na sisi ni Tanzania bara, kwanini wasioitwe Tanzania Visiwani?
CHAWA wasio na dogo watakuja kuharisha humu
 
Tanganyika
Kivipi? Labda nikujulishet tu: Kama Tanganyika iliibwa, basi mwizi alikuwa Nyerere - Mtanganyika. Huenda utauliza aliiba vipi? Ni hivi: Kwenye ule muungano - 1964 -Tanganyika, chini ya uongozi wake, ndiyo iliyotayarisha mkataba wa muungano. Sasa kama mwizi ni huyo. Usiwadanganye watu. Sisi wengine tunajua.
 
Maza ni mtu wa wapi?
1. Maza ni mtu wa Zanzibar.
2. Maza kaiibia Tanganyika?
3. Ukisema kaiba, kaiba nini?
4. Itokee kaiba. Kuiba kwake kunawafanya Wazanzibari kuwa wezi?
5. Mimi nikisema wewe Benjamin Netanyahu - Mtanganyika - huna akili, huna heshima itakuwa Watanganyika hawana akili, hawana heshima?
6. Tujifunze kuzungumza. Kiburi, ujeuri, majivuno na aina yoyote ya matendo maovu hayasaidii na wala si sifa kufanya hivyo.
 
NCHI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ni muunganiko wa nchi mbili(Tanganyika na zanzibar)
so,unataka kusema kuna katiba ya zanzibar na katiba ya bara?
ninachojua katiba iliundwa 1967 kwenye azimio la arusha,badae ikarekebishwa 1977 ndio tunatumia hadi leo
hii katiba ya 1977 ni ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania(katika hii katiba hakuna sehemu inayorefer katiba nyingne ya bara au visiwani)
so kiujumla kwa ninavyojua mimi kikatiba zanzibar ni tanzania visiwani
tofaut ni kwamba wana serikali yao.....
hii ni tofaut na USA
kule wote wapo ndani ya USA ila nevada na washington kila mtu ana katiba yake
jamaa unaandka maelezo meng sn halafu yote n pumba tu. Hata umeshndwa ku google kujua kwmb zanzibar wana katiba yao na inasema zanzibar n nchi miongon mwa nchi znazounda tz. Haya kama hujui nakujuza wana mpk wimbo wa taifa, bendera, rais, mashirika yao, taasisi zao nk.
 
1. Maza ni mtu wa Zanzibar.
2. Maza kaiibia Tanganyika?
3. Ukisema kaiba, kaiba nini?
4. Itokee kaiba. Kuiba kwake kunawafanya Wazanzibari kuwa wezi?
5. Mimi nikisema wewe Benjamin Netanyahu - Mtanganyika - huna akili, huna heshima itakuwa Watanganyika hawana akili, hawana heshima?
6. Tujifunze kuzungumza. Kiburi, ujeuri, majivuno na aina yoyote ya matendo maovu hayasaidii na wala si sifa kufanya hivyo.
Hizo hela anazonunua magoli ya Yanga zipo kwenye budget ipi? fedha anazompa Abdul kuwahonga wanasiasa zinatoka kwenye budget ipi? kama ni uongo kwaninni Abdul hajaenda kumshitaki Lisu mahakamani kwa kumchafua? wizi unaofanyika serikalini una baraka za nani?
 
Muungano wetu haujakaa sawa kuna vitu vinasumbua akili kuelewa
 
Tumeona picha ya ujumbe wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa katika kikao huko China unavibao viwili. Kimoja kimeandikwa Tanzania na zingine kina wajumbe wameweka Bangor akiwa kibao cha Zanzibar. Hizi ndio Sera ya Nchi yetu sasa, baada ya kupata Waziri Mpya wa Mambo ya Nje au ilikuwepo kabla. Na nini tafsiri yake kimataifa na ndani ya nchi

Pia soma:Nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar, kwanini Zanzibar ipo na sisi ni Tanzania bara, kwanini wasioitwe Tanzania Visiwani?
Tutaelewa baadae walioalikwa kwenye mkutano huo wote wazanzabar.
 
Muungano wa ovyo kuwahi kutokea duniani! Binafsi siupendi kabisa kwa sababu Tanganyika inatumika kuineemesha Zanzibar huku Tanganyika ikiwa haifadiki na chochote.
Leo hii Tanganyika tunatawaliwa na Mzanzibari, ardhi yetu imekuwa ya wote lakini ya Zanzibar ni Wazanzibar tu,Wazanzibar huku Tanganyika wanashika cheo chochote, wanaajiriwa kwenye kazi yoyote lakini ni marufuku Mtanganyika kugombea nafasi yoyote ya uongozi Zanzibar wala kuajiriwa, Hata kupiga kura Mtanganyika haruhusiwi labda baada ya kuishi mfululizo kwa muda usiopungua miaka 3.
Huyo Rais anayeitwa wa Muungano hana madaraka yoyote Zanzibar hata DC wa kule anaweza kumvimbia na hana ubavu wa kumtengua labda akamshitaki kwa Rais wao! Uwa nashangaa sana hata sifa wanazopewa wale wanaoitwa waasisi wa Muungano sijui wanasifiwa kwa lipi wakati waliamua kwa makusudi kuisambaratisha nchi yetu tukufu ya Tanganyika!
 
TANZANIA inawakilisha Tanganyika na Zanzbar. Kama Zanzbar inajitoa kwenye utanzania basi aipaswi rais wa Tanzania awe mzanzibari
 
Huu Muungano waliouanzisha hawakuwa na lengo zuri, Tanganyika ilikuwa ni kama mwanaume aliyekolea kwa penzi la Zanzibar kiasi cha kuacha asili yake ili kumridhisha mkewe.
 
Muungano wetu ni kama muungano wa wabunge wa CCM na COVID 19. Wasomi waliobobea wapo lakini tunaburuzwa tu kana kwamba sisi ni kondoo. Wawakilishi wa wananchi ndio jukumu lenu la kuhakikisha mambo ya nchi yanaendeshwa kwa manufaa ya wananchi sio kwa manufaa ya viongozi! Ukiweka bango la Zanzibar la Tanganyika linatakiwa liwepo kando yake sio Tanzania kwani Tanzania Zanzibar imo ndani yake.
 
jamaa unaandka maelezo meng sn halafu yote n pumba tu. Hata umeshndwa ku google kujua kwmb zanzibar wana katiba yao na inasema zanzibar n nchi miongon mwa nchi znazounda tz. Haya kama hujui nakujuza wana mpk wimbo wa taifa, bendera, rais, mashirika yao, taasisi zao nk.
basi itabidi urudie kugoogle uelewe maana ya muungano,halafu uje uniambie kama kuna nchi ya zanzibar, nchi ya tanganyika iko wapi?
 
Hizo hela anazonunua magoli ya Yanga zipo kwenye budget ipi? fedha anazompa Abdul kuwahonga wanasiasa zinatoka kwenye budget ipi? kama ni uongo kwaninni Abdul hajaenda kumshitaki Lisu mahakamani kwa kumchafua? wizi unaofanyika serikalini una baraka za nani?
Umeelewa nilichoandika? Hayo maswali niliyokuuliza imeyaona? Unajua nilipoandika nilikuwa najibu "comment" gani?
 
Back
Top Bottom