Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Mimi kama mtanzania nisiemfuasi wa chama chochote sipendi ushabiki wa kishamba hasa juu ya suala ambalo linagusa maslahi ya kila mtanzania bila kubagua itikadi zake.
Hapa nchini kwetu kumetokea vifo vingi kipindi cha mwezi huu wa kwanza na vifo hivi vimewashutua watu watanzania na kuwa na hofu juu ya maambukizi mapya ya Covid 19 yamevamia nchini kwetu.
Mimi binafsi nasubiri tamko la waziri wa afya,waziri mkuu au rais wa JMT ndio niwe na uhakika juu ya maambukizi haya mapya.
Lakini nini kinawasukuma baadhi ya watu kuizodoa serikali juu ya kutoweka uwazi kama kuna maambukizi mapya?
Nimeshangaa hadi mwenyekiti wa Chadema ameibuka akidai kuwa watanzania tunafichwa juu ya maambukizi ya covid 19. Na ameenda mbali akidai kuwa serikali ikiwa wazi tutapata misaada ya tiba na madakari.
Maoni; Hata hili mnaloshobobokea mkidhani litawabeba kisiasa nalo litapita,maana Mungu yupo na Tanzania. Maambukizi ya mwanzo yalipoingia nchini,mlitengeneza clip kuonyesha watu wanazikwa usiku ,lakini hamkufanikiwa kisiasa. Mungu alitulinda watanzania.