Hili la mbunge baraza la wawakilishi kuwadharau samaki aina ya Kambale na Sato wa ziwa Victoria lisipite pasipo mjadala. Linatoa picha mbaya

Sio wabaguzi! Na hasa ukiangalia suala zima la kambale hapa kisiwani.

Ufugaji na uuzaji wa kambale bado ni kitu kigeni sana, na kwa wenyeji ambao hawajawaji kuvuka bahari ni jambo linalowastua sana!
Jamaa mbaguzi sana
 
Jamani kama taifa tuna kazi ya kufanya kweli kweli.

Wakati viongozi wakuu wa wizara zinazo husika na muungano wakiumiza vichwa kuimarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado kuna wabunge wanaharibu juhudi hizo.

Sikikizeni hapo ili kwa umoja wetu tunajadili.

View attachment 2252519
Nimemsikiliza, amesema kitu gani kibaya?. Serikali ya Zanzibar imetenga billions of money kuanzisha ufugaji wa samaki Zanzibar. Samaki wanaofugika ni sato na kambale, Wanzanzibari hawali samaki hao, hivyo mradi huo ni kwa ajili ya wageni waishio Zanzibar, Mbunge huyo ana hoja ya msingi kabisa na haina tatizo lolote na huu muungano wetu adhimu.

Huyu jamaa ni Mhe. Hassan Hamisi Harish, ni Mwakilshi wa jimbo la Welezo, ni mzalendo sana msikilize hapo ni mzungumzaji wa pili katika video hii.

P
 
Mh! Sasa hapo Muungano au ubaguzi unaingiaje?

Ni kweli Zanzibar wamezoea Samaki wa baharini. Serikali kutenga mabilioni ya pesa kuwekeza kwenye mradi wa Samaki wa maji baridi inaweza kuwa matumizi mabaya ya rasirimali.

Kama bara wanafugwa na kupatikana Kwa wingi, kwanini wasisafirishwe kuuzwa Zanzibar kama soko lipo?

Binafsi sijaona jinsi ubaguzi na Muungano unavyoingia kwenye kauli ya Mheshimiwa.
 
Jamani kama taifa tuna kazi ya kufanya kweli kweli.

Wakati viongozi wakuu wa wizara zinazo husika na muungano wakiumiza vichwa kuimarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado kuna wabunge wanaharibu juhudi hizo.

Sikikizeni hapo ili kwa umoja wetu tunajadili.

View attachment 2252519
Sijaona ubaguzi wowote hapo,ni Swala la kibiashara tu,unazalisha vipi kitu kisichokuwa na soko kwenye nchi yako?kama Kuna soko la nje la hao samaki Sawa,kwamba wazalishwe harafu wakauzwe nje,lakini kwanini wasiendeleze samaki wanaopatikana huko huko kama inawezekana?vile vile kama Kuna fulsa ya kuzalisha sato na kambale,Ili waingize pesa za kigeni,why not?
 
Huwezi kukiita chakula wanacho kula ndugu zako kuwa ni chakula cha HOVYO HOVYO.
 
Mh! Sasa hapo Muungano au ubaguzi unaingiaje?

Ni kweli Zanzibar wamezoea Samaki wa baharini. Serikali kutenga mabilioni ya pesa kuwekeza kwenye mradi wa Samaki wa maji baridi inaweza kuwa matumizi mabaya ya rasirimali.

Kama bara wanafugwa na kupatikana Kwa wingi, kwanini wasisafirishwe kuuzwa Zanzibar kama solo lipo?

Binafsi sijaona jinsi ubaguzi na Muungano unavyoingia kwenye kauli ya Mheshimiwa.
Kwanini akiite chakula wanacho kula ndugu zake wa upande wa pili wa muungano kuwa ni CHAKULA CHA HOVYO HOVYO?

Ukishafikia ngazi fulani ya uongozi lazima uwe na uchaguzi wa maneno ya kusema mbele ya jamii unayo iongoza.
 
Nimemsikiliza, amesema kitu gani kibaya?. Serikali ya Zanzibar imetenga billions of money kuanzisha ufugaji wa samaki Zanzibar. Samaki wanaofugika ni sato na kambale, Wanzanzibari hawali samaki hao, hivyo mradi huo ni kwa ajili ya wageni waishio Zanzibar, Mbunge huyo ana hoja ya msingi kabisa na haina tatizo lolote na huu muungano wetu adhimu.

Huyu jamaa ni Mhe. Hassan Hamisi Harish, ni Mwakilshi wa jimbo la Welezo, ni mzalendo sana msikilize hapo ni mzungumzaji wa pili katika video hii.

P
Chakula anachokula ndugu yako kamwe huwezi kukiita ni chakula cha HOVYO HOVYO.
 
Kwa hiyo kwa maana yake, ku invest kwenye biashara ya kambare na sato, kumefanyika bila umakini, na labda ni katika nia ya kuufurahisha muungano. Hajui hao hao wapemba wamejaa kwenye masoko ya bara wakitafuta hao samaki na vyakula vingine.

Moja ya principle ya biashara ni kufanya watu watakacho, na si wewe utakacho. Kama wewe binafsi hupendi kambare lakini soko linahitaji, kwanini usiwekeze kwenye soko?

Halafu mantiki ya yeye kuwekeza kambale na sangare kwa soko la Zanzibar, ni ulofa. Hivi population ya Zanzibar inafika hata milioni moja? Kama unawekeza kitu kikubwa Zanzibar target market inapaswa kuwa sokoni la nje, sio Zanzibar yenye mtazamo sawa na huyo mbunge huyo na familia zao.
 
Chakula anachokula ndugu yako kamwe huwezi kukiita ni chakula cha HOVYO HOVYO.
Wazenji wanazarau sana,hata mapishi yetu ya bara wanayaona ni ya hovyo hovyo Kama vile tunachemsha tu nakula,lakini wao hawachemshi bali wao ndiyo wanapika chakula Safi!!!
 
Jamani kama taifa tuna kazi ya kufanya kweli kweli.

Wakati viongozi wakuu wa wizara zinazo husika na muungano wakiumiza vichwa kuimarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado kuna wabunge wanaharibu juhudi hizo.

Sikikizeni hapo ili kwa umoja wetu tunajadili.

View attachment 2252519
Huo ubaguzi uusemao mbona sijauona?

Ubaguzi wa kusemea kambare? Mbona hata Wasabato hawali kambare? Au kuna kitu mleta mada sijakielewa, maana nimeisikiliza clip uliyoileta, "mbunge" analalamika mapesa kibao kutumika (naona ni mwakilishi huyu, Zanzibar) kuanzishwa ufugaji wa kambare wakati wao hawana soko la kambare kwa kuwa hawali kambare.

Sasa ubaguzi hapo ni upi?

Tazama hii ndio utaona waziri/ mbunge alivyo mbaguzi wa wazi kabisa...

Licha ya kauli ya kibaguzi tu ni kauli ya ubaguzi wa kidini kabisa. Tena ameyasema hayo akiwa kanisani huku akoitamba. Umeshalikemea hili?

Lakini Mwenyezi Mungu ni mkubwa, haikupita muda, Mbunge na waziri huyo huyo Mwanawe wa kike akaolewa na kijana Mzanzibari, Muislam, na sasa analea watotowa Kiislam, na nna uhakika na yeye kishakuwa Muislam.

Kama haitoshi, mama Samia kamweka anapostahiki. Hasikiki kabisa, kafungwa kidomo-domo kidiplomasia.
 
Kwanini akiite chakula wanacho kula ndugu zake wa upande wa pili wa muungano kuwa ni CHAKULA CHA HOVYO HOVYO?

Ukishafikia ngazi fulani ya uongozi lazima uwe na uchaguzi wa maneno ya kusema mbele ya jamii unayo iongoza.

Ungesema Sasa kwamba tatizo ni uchaguzi wa maneno ujikite hapo. Wabunge wanaorukaruka satakasi bungeni usiwasahau pia.
 
Back
Top Bottom