Mtukufu mtume (saw) alipokuwa anakaribishwa kula chakula, kama alikuwa hapendi chakula fulani alichokaribishwa basi yeye alikula kidogo tu licha ya kwamba hakupenda chakula hicho, hapo lazima tujifunze adabu na heshima ya vyakula halali japokuwa wewe hupendi chakula hicho, usidharau chakula alichotupatia Allah kwani inawezekana ikatokea siku njaa ikakupiga kiasi kwamba hata hicho chakula cha "ajabu ajabu" ukakikosa na ukaishia kula nguruwe aliyeharamishwa.
Heshimu chakula halali japokuwa kwako wewe hukipendi kwani ni Allah ndiye aliyeleta hivyo vyakula.