Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Wenye akili finyu hilo wataliona
Lakini sisi ni kukomesha ujambazi
Kama una ndugu jambazi muandalie shimo



Una kumbukumbu yoyote juu ya kuuliwa kwa wafanyabiashara watatu wa madini toka Mahenge(hapa soma majambazi)pale Sinza?Pamoja na kazi nzuri ya jeshi letu la polisi ya kukabiliana na wahalifu na uhalifu,lakini yapo makosa mengi ya kiutendaji ndani ya jeshi hilo.

Wapo wengi waliopoteza Maisha kwa kuhisiwa ni majambazi lakini hawakuwa majambazi bali ni Raia wema waliohitaji ulinzi wa jeshi badala ya kuwauwa.Imrani Kombe aliuwawa kikatiri na jeshi la polisi kwa kumdhani ni jambazi,baada ya kutekeleza mauwaji,baadae wakagundua kuwa aliyeuliwa hakuwa jambazi bali alikuwa bosi wao.

Vijana wale watatu wa madini walichomolewa roho zao kwa kudaiwa ni majambazi,kumbe walikuwa ni raia wema ambao walihitaji ulinzi wa polisi badala ya kuzawadiwa kifo na polisi wetu.Tukirudi kwenye magereza yetu,wapo wengi waliofungwa huko kwa makosa ya kusingiziwa,si kila mfungwa aliyepo gerezani alitenda uhalifu,wapo wengi humo ambao hawakupaswa kufikia huko.
Kiongozi wa nchi anapotoa kauli za nama hii alipaswa aangalie na weledi wa jeshi letu katika kukabiliana na matukio ya kihalifu na uhalifu wenyewe,polisi wetu bado wanapungukiwa mbinu za kipelelezi za kubaini uhalifu,walipaswa wajengewe uwezo wa kubaini viashiria vya uhalifu na kuvitumia kuwanasa wahalifu badala ya kuelekezwa kupambana na yeyote watakao muhisi ni muhalifu kama walivyopambana na Imrani Kombe na kuuondoa uhai wake.

Kuwapoteza ndugu zetu kwa vifo vya kikatiri vya jeshi la polisi kwa kisingizio cha kupambana na uhalifu ni jambo lisilovumilika.Kauli ya kumpandisha cheo polisi aliyempora jambazi silaha,inaweza kupelekea ujambazi feki mtu akakamatwa na kushikishwa silaha,kisha akaporwa silaha na kujeruhiwa vibaya nakutangazwa kuwa alikuwa jambazi sugu aliyekuwa anatafutwa kwa muda mrefu kumbe ni uongo ulioandaliwa mahususi ili watu wapandishwe vyeo.

Tuendelee kushangilia hotuba za viongozi wetu,lakini tuchukue tahadhari,unaweza kujikuta ni mwathirika wa kwanza wa harakati za jeshi kutafuta vyeo.Chukua tahadhari,kifo hakina Rufaa ukifa umekufa kama alivyokufa mh.Kombe na wale vijana toka Mahenge.
 
Una maana gani unaposema innocent victims? Innocent unatembea na SMG?
Mkuu naona unasahau mapema sana. Aina ya polisi tulinao ina mchanganyiko wa kila aina: majambazi, wavuta bangi, wenye vyeti feki hasa o level na a level, nk. Hii inaleta hatari kwa maisha watu. Hofu ni kwa hao wanaotamkiwa hizo kauli na rais. Wangapi wamejengeka kimaadili?! Utakumbuka visa vya akina Abdalah Zombe vya kuwaua watu wanne kule kwenye msitu wa pande. Na kisa kingine kule Mbeya. Msikariri ID na kuona siasa tu.
 
Pasco we ni senior journalist kuna baadhi ya mambo katika nchi haina hata haja ya kuyajadili,ufisadi,ujambazi,uzembe wa kazi kwa kweli nauchukia sana.
Inawezekana wengine hamjawahi kukumbwa na kadhia ya hayo mambo,mfano unamkuta mtu anampiga risasi ndugu yako halafu usubiri sheria ichukue mkondo wake,katika hili anaweza Yesu tu.
 
Mi naona Donald Triump ndo anafaa ,otherwise kushangilia polisi "kunyanganya silaha na kupandishwa cheo" heee,eeh Mungu hili niepushe,Mungu wa Israel naomba niepushe na wanaoshabikia polisi wanze kunyanganya ndugu zao silaha walau ndugu wawili alafu huu uzi utapendeza!

Maana mnashangilia hata nyuki akikuingia sikioni!
 




Hoja yako ni ya akili sana hadi inakera,ngoja niihifadhi kwa ajili ya rejea huko mbele ya safari.
 
Majambazi yameua inocent victims wangapi?

Naona Ukawa mnatetea uhalifu sasa
Majambazi yameua but kuna mahakama iachwe ifanye kazi yake.Polisi wanavyopewa mamlaka ya kutoa hukumu kwa majambazi kuna wengine watajikuta wanauawa kisa hate.Nilivyo sema Innocent victims nilimaanisha wale wataopoteza maisha kisa uhasama wa kijamii na kifamilia.Wapo polisi wataotumia tamko hili kama loop hole ya kufanya uonevu,mtu hakutaki unabambikiziwa kesi ya ujambazi then unauawa.
Sitetei majambazi kuchukuliwa hatua,natetea ufuataji wa sheria neno la mahakama liwe final.
 
Wakati wao wanavamia vituo na kuua askari huo utawala wa sheria uliwekwa kando siyo! Then inaonekana majambazi unayajua sana zikiwemo mbinu zao za kwenda na toy kuvamia. Anyway umenichekesha na kunihuzunisha sana, pale ARMED JAMBAZI anapopata mtetezi, labda wakivamia kwenu utapata akili
 
Hivi kwenye hotuba kuna mahala rais kasema majambazi auwawe? Tatizo letu watanzania umbeya umetuzidi ukisema neno moja unabambikiwa maneno kibao. Pasco muda wa Lowassa imeshapita kaka
 
Hao polisi watakaotumia vibaya pia mahakama zipo, pili rais kasema wanyang'anywe silaha kwa mbinu, katika vita huwa hatuoni mateka? Si ni wale wanaozidiwa nguvu,
 
Mnakera... Yaani sasa hata majambazi nao wanatetewa?
Ye ashakuambia siraha ya jambazi huwa haiji kwenye field kwa maonyesho inataka ifanye kazi kwa yeyote anayetaka kukwamisha mipango ya majambazi hao,.
Sasa kwanini na yeye WASIMNYANG'ANYE siraha yake wakati yeye yuko hapo kunyang'anya maisha ya wale wanaotaka kutetea mali zao? ( wanaotaka kuharibu kupatikana kwa wanachokitaka)
Acheni hizo..... Kama mko katika hayo makundi mwaka huu lazima mnyooke..... Maana mwenye mapenzi na nchi hawezi kutetea jambazi SIO KIBAKA....
Maana kibaka just ni njaa zake tuu zinamfanya hivyo. Huyu hatumii bunduki, na ukisema umpige risasi sio sawa, huyu anatakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakanmani,,, ila JAMBAZI ambaye ana siraha tena ya Moto, na anapiga risasi kwa watu alafu eti mnataka yeye achekelewe!!!! ..... Aaaaah acheni mambo yenu bana....
 
Kama umefuga majambazi jiandae.

Huu ni muda Wa kufanya mabadiliko na siyo muda wa kushangaa shangaa na kulialia.
Kumbuka unaweza kuzaniwa ni jambazi au ata ndugu yako afu wakaku shoot on sport kuzania begi lako lina silaha ndio utajua kuwa alichoongea Mtawala sio sahihi bali kaongea kwa jazba tu
 
Maelezo ya rais ni sawa lakini yanapotolewa hadharani sababu zake zinatia mashaka! NIA ya rais inaweza kuwa njema lakin tatizo likwa kwa watekelezaji
 
Yaani ubambikiziwe kesi ya ujambazi na ukutwe kwenye eneo la tukio na uwe umebeba silaha...yaani yote hayo yakukute wewe basi utakuwa na laana
 
Mod huu uzi u-pin utakuja kuwa historia baadae,take my words



Nakubaliana na wewe,hoja zilizomo kwenye huu Uzi wa mkubwa "Pasco" ukiziweka pamoja na hoja zilizomo katika Uzi wa Mkuu "Mag3 zinazopatikana katika " waya"huu:


GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

Zikiwekwa pamoja zinaweza kuonekana kuwa kikwazo cha kumchelewesha "mkuu wa kaya" kuwaletea wadanganyika Maendeleo.Ni hoja zinazoakisi sura halisi ya Taifa letu huko tuendako,ni hoja za kizalendo mno zilizotolewa na Wazalendo wa Jf,lakini kwa Tafsiri "sisisi" ya utawala huu,zinaweza kuonekana ni hoja za kichochezi zenye lengo la kuleta "fyokofyoko" za kuizuia serikali kuwaletea wananchi Maendeleo.

Najivunia uwepo wa ma"GT" Pasco na Mag3 hapa jukwaani,Mungu awalinde hawa watu wasishambuliwe na vitu vyenye ncha Kali au wasishikishwe silaha na kunyang'anywa kwa nguvu kwa kisingizio ni majambazi kumbe ni "dili" la kusaka vyeo
 
Katika biblia kuna mwandishi anaitwa Paulo maandiko yake mpk leo inawachanganya wasomi wengi wa biblia na wanazuoni wa elimu Mungu kwakuwa Paulo alikuwa bingwa wa falsafa na aliongea kwa ustadi wa hali yajuu wenye IQ ndogo ni vigumu kumwelewa vivyo ivyo mh Rais wetu ni bingwa wa falsafa watu waropokaji wasiyotakafari kwa kina wanashindwa kumuelewa maneno yake ndiyo maana kila moja anakuja na tafsiri yake. Ni vyema kabla hujaanza kufanya uchambuzi wa maneno ya Dr Magufuli unatakiwa upate tafakuri ya kutosha ili uweze kumuelewa, mh rais aliongelea suala la wanatumia barabara ya mwendokasi watu wakamtafsiri vibaya, juzi kaongelea kuhusu ushirikiano na vyama vya siasa watu wachovu wa fikra wakasema wamezuia vyama siasa kufanya siasa Jana kaongelea mapambano ya polisi na majambazi wamebadilisha kasema majambazi wauwawe. Nadhani sasa tufike wakati tuwe watafakari zaidi kabla ya kufanya uchambuzi. Mungu mbariki shujaa na mzalendo halisi Dr John Pombe Magufuli
 
Kwa hiyo unasuggest polisi wawe wanatembea na mahakimu??
 
Sijui kwanini mmechagua kuendelea kumpotosha rais wetu mpendwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…