Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Wenye akili finyu hilo wataliona
Lakini sisi ni kukomesha ujambazi
Kama una ndugu jambazi muandalie shimo



Una kumbukumbu yoyote juu ya kuuliwa kwa wafanyabiashara watatu wa madini toka Mahenge(hapa soma majambazi)pale Sinza?Pamoja na kazi nzuri ya jeshi letu la polisi ya kukabiliana na wahalifu na uhalifu,lakini yapo makosa mengi ya kiutendaji ndani ya jeshi hilo.

Wapo wengi waliopoteza Maisha kwa kuhisiwa ni majambazi lakini hawakuwa majambazi bali ni Raia wema waliohitaji ulinzi wa jeshi badala ya kuwauwa.Imrani Kombe aliuwawa kikatiri na jeshi la polisi kwa kumdhani ni jambazi,baada ya kutekeleza mauwaji,baadae wakagundua kuwa aliyeuliwa hakuwa jambazi bali alikuwa bosi wao.

Vijana wale watatu wa madini walichomolewa roho zao kwa kudaiwa ni majambazi,kumbe walikuwa ni raia wema ambao walihitaji ulinzi wa polisi badala ya kuzawadiwa kifo na polisi wetu.Tukirudi kwenye magereza yetu,wapo wengi waliofungwa huko kwa makosa ya kusingiziwa,si kila mfungwa aliyepo gerezani alitenda uhalifu,wapo wengi humo ambao hawakupaswa kufikia huko.
Kiongozi wa nchi anapotoa kauli za nama hii alipaswa aangalie na weledi wa jeshi letu katika kukabiliana na matukio ya kihalifu na uhalifu wenyewe,polisi wetu bado wanapungukiwa mbinu za kipelelezi za kubaini uhalifu,walipaswa wajengewe uwezo wa kubaini viashiria vya uhalifu na kuvitumia kuwanasa wahalifu badala ya kuelekezwa kupambana na yeyote watakao muhisi ni muhalifu kama walivyopambana na Imrani Kombe na kuuondoa uhai wake.

Kuwapoteza ndugu zetu kwa vifo vya kikatiri vya jeshi la polisi kwa kisingizio cha kupambana na uhalifu ni jambo lisilovumilika.Kauli ya kumpandisha cheo polisi aliyempora jambazi silaha,inaweza kupelekea ujambazi feki mtu akakamatwa na kushikishwa silaha,kisha akaporwa silaha na kujeruhiwa vibaya nakutangazwa kuwa alikuwa jambazi sugu aliyekuwa anatafutwa kwa muda mrefu kumbe ni uongo ulioandaliwa mahususi ili watu wapandishwe vyeo.

Tuendelee kushangilia hotuba za viongozi wetu,lakini tuchukue tahadhari,unaweza kujikuta ni mwathirika wa kwanza wa harakati za jeshi kutafuta vyeo.Chukua tahadhari,kifo hakina Rufaa ukifa umekufa kama alivyokufa mh.Kombe na wale vijana toka Mahenge.
 
Una maana gani unaposema innocent victims? Innocent unatembea na SMG?
Mkuu naona unasahau mapema sana. Aina ya polisi tulinao ina mchanganyiko wa kila aina: majambazi, wavuta bangi, wenye vyeti feki hasa o level na a level, nk. Hii inaleta hatari kwa maisha watu. Hofu ni kwa hao wanaotamkiwa hizo kauli na rais. Wangapi wamejengeka kimaadili?! Utakumbuka visa vya akina Abdalah Zombe vya kuwaua watu wanne kule kwenye msitu wa pande. Na kisa kingine kule Mbeya. Msikariri ID na kuona siasa tu.
 
Pasco we ni senior journalist kuna baadhi ya mambo katika nchi haina hata haja ya kuyajadili,ufisadi,ujambazi,uzembe wa kazi kwa kweli nauchukia sana.
Inawezekana wengine hamjawahi kukumbwa na kadhia ya hayo mambo,mfano unamkuta mtu anampiga risasi ndugu yako halafu usubiri sheria ichukue mkondo wake,katika hili anaweza Yesu tu.
 
Mi naona Donald Triump ndo anafaa ,otherwise kushangilia polisi "kunyanganya silaha na kupandishwa cheo" heee,eeh Mungu hili niepushe,Mungu wa Israel naomba niepushe na wanaoshabikia polisi wanze kunyanganya ndugu zao silaha walau ndugu wawili alafu huu uzi utapendeza!

Maana mnashangilia hata nyuki akikuingia sikioni!
 
Pasco, kuna siku polisi wakitimiza haya, Mh. kuna mwaka atapelekwa the Hague! He has authorised the suspects to be condermed unheard! Can this justify one to face ICC for haphazard killings of suspects? (I am not a lawyer). A big point to note from your posting is MAKUNDI MENGINE YANAYOONEKANA NI KERO. TRULY THIS IS SOMETHING TO WORRY ABOUT!




Hoja yako ni ya akili sana hadi inakera,ngoja niihifadhi kwa ajili ya rejea huko mbele ya safari.
 
Majambazi yameua inocent victims wangapi?

Naona Ukawa mnatetea uhalifu sasa
Majambazi yameua but kuna mahakama iachwe ifanye kazi yake.Polisi wanavyopewa mamlaka ya kutoa hukumu kwa majambazi kuna wengine watajikuta wanauawa kisa hate.Nilivyo sema Innocent victims nilimaanisha wale wataopoteza maisha kisa uhasama wa kijamii na kifamilia.Wapo polisi wataotumia tamko hili kama loop hole ya kufanya uonevu,mtu hakutaki unabambikiziwa kesi ya ujambazi then unauawa.
Sitetei majambazi kuchukuliwa hatua,natetea ufuataji wa sheria neno la mahakama liwe final.
 

Wanabodi,

Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.

Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.

Agizo hilo limepokelewa kwa shangwe na makofi kwa kila aliyekuwe pale.

Rais huku akisema kwa msisitizo kwa kutumia fasihi ya "kuwanyanganya silaha", kwa vile majambazi wanatumia silaha, zenye risasi kufanya ujambazi, na jeshi la polisi nalo wanazo silaha zenye risasi, haoni kwa nini majambazi hayo yasinyang'anywe silaha zao!. Namna pekee ya kunyanganya silaha jambazi mwenye silaha, ni kumalizana nao, papo kwa papo!.

Sina shaka kabisa na nia ya dhati ya rais Magufuli, kutoa amri, hiyo, kufuatia nchi na wananchi kuchoshwa na vitendo vya ujambazi kuongezeka, hivyo majambazi wakijua kuwa wakikamatwa watauwawa right away, then, amri hii badala ya kupunguza ujambazi wa kutumia silaha, ndio kwanza utaongeza impunity kwa majambazi wanaotumia silaha, na wakati huo huo kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!.

Sio majambazi wote wanaotumia silaha, zile silaha zao zina risasi!, wengine huzitumia kutishia tuu, lakini hawana nia ya kufanya mauaji, na kuna wengine hubeba silaha ambazo hazina risasi, na wengine hutumia toy pisto!, lakini kufuatia amri hii, polisi ndio kwanza wamekuwa licenced to kill!.

Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleke majambazi wanaotumia silaha, mbele ya sheria, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubirria kupandishwa vyeo!. Just imagine mashindano ya kupanda vyeo miongoni mwa polisi wetu!.

Kama wanasheria wetu, hawatashitushwa na amri hii ya rais, nitaamini sasa Watanzania wameanza kumwelewa rais wetu, na ukiisha elewa, huna haja ya kuhoji!.

Angalizo: Sitetei vitendo vyovyote vya uhalifu wa aina yoyote, bali natetea utoaji wa haki!, hata jambazi anayetumia silaha, anastahili kutendewa haki!. Natolea mfano wa nchi mbili za Maekani na Uingeeza. Miaka ya nyuma nchi zote hizi zilikubwa na vitendo vingi vya mauaji. Uingeeza ikafuta adhabu ya kifo!, vitendo vya mauaji, vikapungua kwa kiasi kikubwa!. Maekani ikaendelea na adhabu ya kifo, vitendo vya mauaji bado vimeongezeka!.

Amri ya kuwaua majambazi papo kwa papo, haitapunguza ujambazi, bali itawafanya hao majambazi ndio kugeua wauwaji wakuu, kwa hoja za "ama zao, ama zetu" na kwenye tukio lolote la ujambazi wa kutumia silaha, polisi wakitokea, sasa sio tena kutuliza amani bali kufanya a blood bath!, hivyo polisi sasa pia watakuwa ni target ya majambazi!.

Kwetu sisi waandishi, ikitokea polisi wakakutana na gun mike, au boom mike, au hata kamera wakaiona ni kama sihaha!, kama ilivyotokea mwa Daudi Mwangosi!, askai mhusika, atapandishwa cheo!. Kama wale vija wa Zombe, sasa watawadiwa vyeo!.

Huko nyuma niliwahi kushauri, kama katiba ni kikwazo, rais Magufuli, aiweke pembeni katiba na badala yake atawale kwa kutumia 'presidential decrees' tuu!. Hivyo kwa amri hii ya polisi kuua majambazi papo kwa papo, kama mahakama ni kikwazo, pia anaweza kuiweka pembeni, na kuwatumia polisi kutoa hukumu za kifo cha papo kwa papo, tena hili litaokoa fedha nyingi sana, maana majaji wa mahakama zetu, wanahudumiwa kwa gharama kubwa sana!.

Wasiwasi wangu kwa amri kama hizi, sio ili kuokoa maisha ya majambazi wanaotumia silaha, au kuwaacha tuu majambazi wanaotumia silaha kuua, lakini wao kuuliwa tuinawatetea!, no!, wasiwasi wangu ni utekelezaji wa amri za aina hii, zisije kuwa kwa majambazi ni mwanzo tuu, baadae amri kama hizi za 'kinyemela' zikaelekezwa kwa makundi mengine, yanayoonekana ni kero!.

Hata Adolfu alipoanza, alianza hivi hivi kwa kushangiliwa na umati wa watu!, ni baadae sana, ndipo watu wakajuta!, chonde chonde twendeni taratibu jamani tusije kujuta!.

Jumamosi Njema.

Pasco

Wakati wao wanavamia vituo na kuua askari huo utawala wa sheria uliwekwa kando siyo! Then inaonekana majambazi unayajua sana zikiwemo mbinu zao za kwenda na toy kuvamia. Anyway umenichekesha na kunihuzunisha sana, pale ARMED JAMBAZI anapopata mtetezi, labda wakivamia kwenu utapata akili
 
Hivi kwenye hotuba kuna mahala rais kasema majambazi auwawe? Tatizo letu watanzania umbeya umetuzidi ukisema neno moja unabambikiwa maneno kibao. Pasco muda wa Lowassa imeshapita kaka
 
Majambazi yameua but kuna mahakama iachwe ifanye kazi yake.Polisi wanavyopewa mamlaka ya kutoa hukumu kwa majambazi kuna wengine watajikuta wanauawa kisa hate.Nilivyo sema Innocent victims nilimaanisha wale wataopoteza maisha kisa uhasama wa kijamii na kifamilia.Wapo polisi wataotumia tamko hili kama loop hole ya kufanya uonevu,mtu hakutaki unabambikiziwa kesi ya ujambazi then unauawa.
Sitetei majambazi kuchukuliwa hatua,natetea ufuataji wa sheria neno la mahakama liwe final.
Hao polisi watakaotumia vibaya pia mahakama zipo, pili rais kasema wanyang'anywe silaha kwa mbinu, katika vita huwa hatuoni mateka? Si ni wale wanaozidiwa nguvu,
 
Mnakera... Yaani sasa hata majambazi nao wanatetewa?
Ye ashakuambia siraha ya jambazi huwa haiji kwenye field kwa maonyesho inataka ifanye kazi kwa yeyote anayetaka kukwamisha mipango ya majambazi hao,.
Sasa kwanini na yeye WASIMNYANG'ANYE siraha yake wakati yeye yuko hapo kunyang'anya maisha ya wale wanaotaka kutetea mali zao? ( wanaotaka kuharibu kupatikana kwa wanachokitaka)
Acheni hizo..... Kama mko katika hayo makundi mwaka huu lazima mnyooke..... Maana mwenye mapenzi na nchi hawezi kutetea jambazi SIO KIBAKA....
Maana kibaka just ni njaa zake tuu zinamfanya hivyo. Huyu hatumii bunduki, na ukisema umpige risasi sio sawa, huyu anatakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakanmani,,, ila JAMBAZI ambaye ana siraha tena ya Moto, na anapiga risasi kwa watu alafu eti mnataka yeye achekelewe!!!! ..... Aaaaah acheni mambo yenu bana....
 
Kama umefuga majambazi jiandae.

Huu ni muda Wa kufanya mabadiliko na siyo muda wa kushangaa shangaa na kulialia.
Kumbuka unaweza kuzaniwa ni jambazi au ata ndugu yako afu wakaku shoot on sport kuzania begi lako lina silaha ndio utajua kuwa alichoongea Mtawala sio sahihi bali kaongea kwa jazba tu
 
mh, mbona mi naona sawa tu.

just imajin, mtu anakuvamia akiwa na silaha,anakuweka chini ya amri zake, anachukua anachotaka na ukifanya masihara anakutoa maisha mm kwa upande wangu sioni sababu za kuwachekea watu kama hawa.

kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu, i don't think so, watuwamechishwa na hali ya kutokaa kwa amani.
Maelezo ya rais ni sawa lakini yanapotolewa hadharani sababu zake zinatia mashaka! NIA ya rais inaweza kuwa njema lakin tatizo likwa kwa watekelezaji
 
Majambazi yameua but kuna mahakama iachwe ifanye kazi yake.Polisi wanavyopewa mamlaka ya kutoa hukumu kwa majambazi kuna wengine watajikuta wanauawa kisa hate.Nilivyo sema Innocent victims nilimaanisha wale wataopoteza maisha kisa uhasama wa kijamii na kifamilia.Wapo polisi wataotumia tamko hili kama loop hole ya kufanya uonevu,mtu hakutaki unabambikiziwa kesi ya ujambazi then unauawa.
Sitetei majambazi kuchukuliwa hatua,natetea ufuataji wa sheria neno la mahakama liwe final.
Yaani ubambikiziwe kesi ya ujambazi na ukutwe kwenye eneo la tukio na uwe umebeba silaha...yaani yote hayo yakukute wewe basi utakuwa na laana
 
Mod huu uzi u-pin utakuja kuwa historia baadae,take my words



Nakubaliana na wewe,hoja zilizomo kwenye huu Uzi wa mkubwa "Pasco" ukiziweka pamoja na hoja zilizomo katika Uzi wa Mkuu "Mag3 zinazopatikana katika " waya"huu:


GESTAPO yatunyemelea! Je tumerudi nyuma miaka 80?

Zikiwekwa pamoja zinaweza kuonekana kuwa kikwazo cha kumchelewesha "mkuu wa kaya" kuwaletea wadanganyika Maendeleo.Ni hoja zinazoakisi sura halisi ya Taifa letu huko tuendako,ni hoja za kizalendo mno zilizotolewa na Wazalendo wa Jf,lakini kwa Tafsiri "sisisi" ya utawala huu,zinaweza kuonekana ni hoja za kichochezi zenye lengo la kuleta "fyokofyoko" za kuizuia serikali kuwaletea wananchi Maendeleo.

Najivunia uwepo wa ma"GT" Pasco na Mag3 hapa jukwaani,Mungu awalinde hawa watu wasishambuliwe na vitu vyenye ncha Kali au wasishikishwe silaha na kunyang'anywa kwa nguvu kwa kisingizio ni majambazi kumbe ni "dili" la kusaka vyeo
 
Pasco, kuna siku polisi wakitimiza haya, Mh. kuna mwaka atapelekwa the Hague! He has authorised the suspects to be condermed unheard! Can this justify one to face ICC for haphazard killings of suspects? (I am not a lawyer). A big point to note from your posting is MAKUNDI MENGINE YANAYOONEKANA NI KERO. TRULY THIS IS SOMETHING TO WORRY ABOUT!
Katika biblia kuna mwandishi anaitwa Paulo maandiko yake mpk leo inawachanganya wasomi wengi wa biblia na wanazuoni wa elimu Mungu kwakuwa Paulo alikuwa bingwa wa falsafa na aliongea kwa ustadi wa hali yajuu wenye IQ ndogo ni vigumu kumwelewa vivyo ivyo mh Rais wetu ni bingwa wa falsafa watu waropokaji wasiyotakafari kwa kina wanashindwa kumuelewa maneno yake ndiyo maana kila moja anakuja na tafsiri yake. Ni vyema kabla hujaanza kufanya uchambuzi wa maneno ya Dr Magufuli unatakiwa upate tafakuri ya kutosha ili uweze kumuelewa, mh rais aliongelea suala la wanatumia barabara ya mwendokasi watu wakamtafsiri vibaya, juzi kaongelea kuhusu ushirikiano na vyama vya siasa watu wachovu wa fikra wakasema wamezuia vyama siasa kufanya siasa Jana kaongelea mapambano ya polisi na majambazi wamebadilisha kasema majambazi wauwawe. Nadhani sasa tufike wakati tuwe watafakari zaidi kabla ya kufanya uchambuzi. Mungu mbariki shujaa na mzalendo halisi Dr John Pombe Magufuli
 
Majambazi yameua but kuna mahakama iachwe ifanye kazi yake.Polisi wanavyopewa mamlaka ya kutoa hukumu kwa majambazi kuna wengine watajikuta wanauawa kisa hate.Nilivyo sema Innocent victims nilimaanisha wale wataopoteza maisha kisa uhasama wa kijamii na kifamilia.Wapo polisi wataotumia tamko hili kama loop hole ya kufanya uonevu,mtu hakutaki unabambikiziwa kesi ya ujambazi then unauawa.
Sitetei majambazi kuchukuliwa hatua,natetea ufuataji wa sheria neno la mahakama liwe final.
Kwa hiyo unasuggest polisi wawe wanatembea na mahakimu??
 
Hivi Mkuu Pasco unafahamu ni kwanini raisi JPM kataka kuona hiyo call centre?

Ni kwasababu polisi wamekuwa wakizembea kwenye suala la response kwa wananchi.

Hivyo kwa kuwa na "dedicated and state of the art call center" kama hiyo itasaidia sana wale "Arms Response Unit" kutekeleza jukumu la polisi la kupambana na majambazi.

Raisi kutoa ishara ya kuruhusu Polisi kunyang'anya majambazi silaha ni sawa kabisa.

Ujambazi wa sasa Tanzania unahusisha "well coordinated and highly organised criminals" ambao ni wa makundi mbalimbali.

Haichukui muda mwingi kutambua hilo kutokana na aina ya ujambazi unaofanyika iwe kwenye mabenki na kwenye vituo vya polisi ambapo silaha zinaporwa.

Ndio maana wale wote wanaomiliki silaha walishauriwa kuhakiki silaha zao, na Amiri Jeshi Mkuu mwenyewe akahakiki silaha zake.

"Licence to kill" ipo sehemu nyingi duniani hasa kwa hizi "organised crimes" na nchi zingine hasa hizo ulizozitaja za Uingereza na Marekani, ukiwa umeshilikia "toy gun" unawashwa tu maana kunakuwa hamna namna.

Wakati mwingine unapopiga simu polisi ya kuhusu kutishiwa maisha yako au kuna jambazi sehemu hawatakuja polisi wa kawaida bali wale wa "Arms response unit" yaani wenye silaha na hawatakuwa na simile na mshika bunduki.

Cha msingi ni kuhakikisha kuna guidelines za kufuata kuanzia simu ilipopigwa hadi "response" ilivyofanyika na kunakuwepo na uchunguzi wa tukio zima na independent body ambayo inaangalia "performance" ya polisi.

Ila hata bodi hiyo ikijatoa taarifa ya uchunguzi wake, tayari jambazi anakuwa alikwishazikwa na uhalifu umepotea mitaani.
Sijui kwanini mmechagua kuendelea kumpotosha rais wetu mpendwa!
 
Back
Top Bottom