Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Nina
Nina wasiwasi kama umepitia jeshini kwani kama ungepitiaungejua maana ya Mbinu Za Medani! Sio kuua asilani!
 



Tatizo lako ni moja,huna utulivu wa fikra,una fuatilia hoja jukwaani kwa jicho la kishabiki,ukiipitia na kukosa walau sentensi moja iliyomsifu "mtakatifu wa watakatifu" unapaniki.

Kimsingi hakuna anayepingana na nia njema ya Mh.John Pombe Joseph Magufuli,Rais wa JMT na Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama katika kukabiliana na vitendo vya kihalifu nchini,ulinzi na usalama wa Taifa ni jukumu la msingi la kila Mtanzania bila kujali nafasi yake.

Hofu yetu ni namna kiongozi wetu anavyotoa matamko na maelekezo kwa vyombo vyake,na hofu yetu si ya bahati mbaya,tuna kumbukumbu ya matukio ya mauwaji yenye picha ya kupambana na uhalifu,lakini baadae ikagundulika yalikuwa ni mauwaji ya Raia wema wasio na hatia.

Hili linaweza lisionekane kuwa Tatizo,lakini ikitokea kesho ukapoteza ndugu/jamaa yako kwa kuuliwa kinyama kwa kudhaniwa ni jambazi,ndipo utakapokumbuka kwa nini tulilipinga kwa nguvu zote Tamko hili linalowahimiza polisi wetu kutumia nguvu badala ya weledi katika kupambana na uhalifu na wahalifu.

Sitaki kutumia mifano inayoleta simanzi,lakini kifo cha Mh.Imran Kombe aliyeuwawa kikatili kwa kudhaniwa ni jambazi bado nakikumbuka na ni moja ya tukio la kinyama zaidi dhidi ya haki ya kuishi ambayo ni haki namba 1 kwa mwanadamu yeyote.Kumbuka kifo hakina Rufaa,ukifa umekufa,Imran Kombe aliuwawa kimakosa lakini uhai wake haukurudi,alikufa.

Unalikumbuka tukio la kusikitisha la vijana watatu wafanyabiashara wa madini toka Mahenge?Vijana hawa nao waliuliwa kimakosa kwa kudhaniwa ni majambazi,lakini baadae iligundulika kuwa ni Raia wema waliouliwa kimakosa,ni nani aliyekikatia kifo rufaa ili vijana wale warudishiwe uhai wao?Kifo hakina rufaa.

Pamoja na nia njema ya kupambana na uhalifu,kwa kupitia mifano hiyo michache,upo uwezekano wa jeshi letu kutenda makosa wawapo Katika utekelezaji wa amri ya mkuu wao yenye motisha ya kupandishwa vyeo.Ni vema jeshi letu ambalo kwa siku za hivi karibuni limebobea sana katika intelijensia ya kuzuia haki za kisiasa,lijikite sasa kukabiliana na changamoto za uhalifu nchini kwa kuwa na mbinu za kisasa za kiintelejensia zitakazowawezesha kuitambua Mipango ya kihalifu mapema na kuidhibiti,badala ya kujipangu kumrukia jambazi ili wapandishwe vyeo.
 

hatari..!
 
Wanabodi,
Usikute kifo cha Akwilina, ni utekelezaji wa agizo hili!. Yule polisi aliyefyatua risasi aliona jambazi fulani lenye silaha miongoni wa waandamanaji wale, na akalifyatulia risasi ili kulinyanganya silaha, lakini risasi hiyo ikapinda na kuingia kwenye dala dala ya kumpata yule malaika wa Mungu.

Hobo, tusiwalaumu sana vijana wa kamanda Sirro, as if tukio la kifo cha Akwilina lilipangwa, ni bahati mbaya tuu, na limetokea katika utekelezaji wa amri halali ya Amiri Jeshi Mkuu!.

Polisi hawakuanza leo matukio kama haya, hivyo hapa ni katika kukumbushana tuu, mambo kama haya yaliishatokea huko nyuma, yametokea sasa, na yatatokea tena!. Tutakumbushana!.
P
 
Mkuu tangu lini risasi ikapinda au kukata kona?kwa nini isingepinda na kumtwanga mkuu wake?kilichotokea ni uzembe na kufanya kazi kwa mazoea,au pia inaweza kuwa makusudi jeshi LA police halifai linatakiwa liundwe upya ili tupate watu timamu,
 
Baada ya Mhe. Zitto kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kulichafua jeshi la polisi, nafanya tuu rejea ya kuangazia usafi wa jeshi letu la polisi.
Tuungane kuombea Zitto atendewe haki, lakini pia tusiache kulitaka jeshi letu la polisi, wajitathmini
Paskali.
 
Leo tarehe 21 december kauli yako pale kurasini ya kuzuia askari kuwekwa ndani wakufanya kosa na kwamba polisi akiua apandishwe cheo apewe na cheti huku ukijinasibu kuwa polisi hawezi kumuonea mtu huo ni udikteta nikitumia vyema kigezo cha kuingilia mihimili mingine hapo umefeli.
•Labda mheshimiwa huwajui polisi hawa unaowasifu kama huamini zile silaha walizokuonyesha kuwa zimenyang'anywa kwa majambazi zingine n za zamani ila umelishwa matango poli
Mheshimiwa Amirijeshi mkuu Nchi hii hakuna aliyepo juu ya sheria(kwa mujibu wa katiba)
Hivyo ni vyema ujipime kwa kauli zako kwani zinaweza kuwaletea viburi watendaji wako mheshimiwa tafadhali nakuomba sana jirekebishe.

...













naunga mkono uboreshaji wa miundombinu
 
Wakuu habari za leo?
Nimemsikia Mh Rais wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo yandani kuwa endapo askari polisi akifanikiwa kumuua mtuhumiwa wa ujambazi basi yeye hataki kusikia eti askari wake amewekwa mahabusu kwajili ya uchunguzi. Amemtaka IGP kumpandisha cheo na kumpatia zawadi zingine ikiwemo kumuongezea mshahara wake badala ya kumsweka rumande kwa uchunguzi.
Je ni sahihi kwa Mkuu wa nchi kutamka maneno yale tena hadharani??

Kila mara tumekuwa tukiwalalamikia Polisi kwa kuwabambikizia kesi raia vp kwa maneno yale kweli Mh Rais ni Mtetezi wa Wanyonge au ndiye kitanzi kwa Wanyonge??
 
Huyu atapelekwa ICC, haya yanawekwa kwenye records!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…