mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 7,922
- 3,618
kuna waziri mmoja somebody mwapachu aliwahi toa kauli za hivi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanabodi,
Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.
Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.
Agizo hilo limepokelewa kwa shangwe na makofi kwa kila aliyekuwe pale.
Rais huku akisema kwa msisitizo kwa kutumia fasihi ya "kuwanyanganya silaha", kwa vile majambazi wanatumia silaha, zenye risasi kufanya ujambazi, na jeshi la polisi nalo wanazo silaha zenye risasi, haoni kwa nini majambazi hayo yasinyang'anywe silaha zao!. Namna pekee ya kunyanganya silaha jambazi mwenye silaha, ni kumalizana nao, papo kwa papo!.
Sina shaka kabisa na nia ya dhati ya rais Magufuli, kutoa amri, hiyo, kufuatia nchi na wananchi kuchoshwa na vitendo vya ujambazi kuongezeka, hivyo majambazi wakijua kuwa wakikamatwa watauwawa right away, then, amri hii badala ya kupunguza ujambazi wa kutumia silaha, ndio kwanza utaongeza impunity kwa majambazi wanaotumia silaha, na wakati huo huo kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!.
Sio majambazi wote wanaotumia silaha, huzitumia silaha hizo kufanyia mauaji!, sio silaha zote zinazobebwa zinakuwa loaded!, wengine huzitumia kutishia tuu, lakini hawana nia ya kufanya mauaji, na kuna wengine hubeba silaha ambazo hazina risasi, na wengine hutumia toy pisto!,na majambazi wengine, hubeba silaha, na ziko loaded, lakini hawafanyi mauaji baada ya kupata walichotaka!, lakini kufuatia amri hii, hao majambazi wenye huruma na maisha ya watu, hawatakuwa na huruma tena, na kama polisi ndio kwanza wamekuwa licenced to kill kwa mtindo wa MM, then every encounter ya polisi na majambazi, tutegemee nothing, no justice but blood bath!.
Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleke majambazi wanaotumia silaha, mbele ya sheria, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubirria kupandishwa vyeo!. Just imagine mashindano ya kupanda vyeo miongoni mwa polisi wetu!.
Kama wanasheria wetu, hawatashitushwa na amri hii ya rais, nitaamini sasa Watanzania wameanza kumwelewa rais wetu, na ukiisha elewa, huna haja ya kuhoji!.
Angalizo: Sitetei vitendo vyovyote vya uhalifu wa aina yoyote, bali natetea utoaji wa haki!, hata jambazi anayetumia silaha, anastahili kutendewa haki!. Natolea mfano wa nchi mbili za Maekani na Uingeeza. Miaka ya nyuma nchi zote hizi zilikubwa na vitendo vingi vya mauaji. Uingeeza ikafuta adhabu ya kifo!, vitendo vya mauaji, vikapungua kwa kiasi kikubwa!. Maekani ikaendelea na adhabu ya kifo, vitendo vya mauaji bado vimeongezeka!.
Amri ya kuwaua majambazi papo kwa papo, haitapunguza ujambazi, bali itawafanya hao majambazi ndio kugeua wauwaji wakuu, kwa hoja za "ama zao, ama zetu" na kwenye tukio lolote la ujambazi wa kutumia silaha, polisi wakitokea, sasa sio tena kutuliza amani bali kufanya a blood bath!, hivyo polisi sasa pia watakuwa ni target ya majambazi!.
Kwetu sisi waandishi, ikitokea polisi wakakutana na gun mike, au boom mike, au hata kamera wakaiona ni kama sihaha!, kama ilivyotokea mwa Daudi Mwangosi!, askai mhusika, atapandishwa cheo!. Kama wale vija wa Zombe, sasa watawadiwa vyeo!.
Huko nyuma niliwahi kushauri, kama katiba ni kikwazo, rais Magufuli, aiweke pembeni katiba na badala yake atawale kwa kutumia 'presidential decrees' tuu!. Hivyo kwa amri hii ya polisi kuua majambazi papo kwa papo, kama mahakama ni kikwazo, pia anaweza kuiweka pembeni, na kuwatumia polisi kutoa hukumu za kifo cha papo kwa papo, tena hili litaokoa fedha nyingi sana, maana majaji wa mahakama zetu, wanahudumiwa kwa gharama kubwa sana!.
Wasiwasi wangu kwa amri kama hizi, sio ili kuokoa maisha ya majambazi wanaotumia silaha, au kuwaacha tuu majambazi wanaotumia silaha kuua, lakini wao kuuliwa tuinawatetea!, no!, wasiwasi wangu ni utekelezaji wa amri za aina hii, zisije kuwa kwa majambazi ni mwanzo tuu, baadae amri kama hizi za 'kinyemela' zikaelekezwa kwa makundi mengine, yanayoonekana ni kero!.
Mwaka 1976, kulifanyika mauaji ya wazee waliokuwa wakituhumiwa kuwa ni wachawi. Serikali kupitia waziri wa Mambo ya Ndani kipindi hicho, Ali Hassan Mwinyi Mwinyi, kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mwanza, chini ya RC Peter Kisumo, RSO, RPC, DSO, na OCD wakadhamiria kwa kauli moja kukomesha vitendo hivyo kwa hizo hizo MM alizoamrisha Magufuli zitumike!.
Katika Mahojiano, yaliyoendeshwa eneo la Kigoto, watuhumiwa wawili, Masanja Makula Mazengenuka, na Isaack Mwanamkoboko, walipoteza maisha!.
Mwalimu Nyerere alikasika sana, Waziri Mwinyi, IGP, Pundugu, Director wa TISS Mzena, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Kisumo, RSO, RPC, DSO na OCD wote wakastaafishwa kwa manufaa, na wengine kupandishwa kizimbani, ambapo wote walifungwa, isipokuwa mshtakiwa Mzee wangu, tena aliokoka kwa vile tuu alikuwa anatetewa na wakili Murtaza Lakha!.
Utendaji wa Jeshi la Polisi unaongozwa na kitu kinachoitwa Police General Ordes ambacho tumekirithi kutoka kwa Waingereza kama tulivyorithi sheria zetu mbalimbali, ambazo zina maelekezo yote ni kwenye mazingira gani polisi anaruhusiwa kutumia silaha kuwadhibiti wahalifu na kuna polisi maalum wa kazi hiyo wanaoitwa snipers au wadunguaji, ambao wana shabaha na uwezo wa kulenga maeneo rasmi ya kulenga ili kumdestabilize mhalifu kwa lengo la kumkamata lakini sio kwa lengo la kumua!. Agizo la jana la Rais Magufuli, ni kuwaelekeza polisi kuua tena kwa haraka bila kuchelewa, na sasa kwa kila mauaji ya polisi, polisi hao badala ya kupandishwa kizimbani, sasa watapandishwa vyeo!.
Japo lengo la agizo hilo la rais, amelitoa kwa dhamira njema,(in good faith), lakini utekelezaji wake, unaweza kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!, na hata Adofu alipoanza, alianza hivi hivi kwa kuwa a populist leader, anayeshangiliwa sana na umati wa watu!, ni baadae sana, ndipo watu wakaja kugundua, by that time, it was too little too late, wakaishia kujuta!, kwa upande wetu, chonde chonde twendeni taratibu jamani, tufungue macho mapema before it is too late, tusije kujuta!.
Jumamosi Njema.
Pasco
Rejea.
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa .
Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa ..
kwa upande wetu, chonde chonde twendeni taratibu jamani, tufungue macho mapema before it is too late, tusije kujuta
1101112131415
- Ninamshangaa sana Mpemaanavyoshabikia majambazi nayeye nimojawao nn?? Badala ya kuleta haja maendeleo unakomaa na habari zamajambazi siku wakikutembeleautaelewa vizuri umuhimu wa kauli ya raisi.
ReportEditDelete
+ QuoteReply
- Rais Magufuli, Waziri mkuu Majaliwa: Hili ni jipu Jeshi la Polisi Tanzania Jukwaa la Siasa Mar 19, 2016
Sijapata ona Jeshi la Polisi bora kama hili la sasa tangu Uhuru Jukwaa la Siasa Sep 20, 2014
Polisi epukeni sana hili Jukwaa la Siasa Sep 18, 2014
Jamboleo, uhuru,hoja mtaripoti vipi hili la polisi Jukwaa la Siasa Sep 18, 2014
Polisi, hili mbona hamlisemi hadharani ! Jukwaa la Siasa Sep 18, 2014
ForumsJukwaa la Siasa
Style Chooser
- WHO ARE WE?
JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic. You are always welcome!
Read more...- WHERE ARE WE?
We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually. For anything related to this site please Contact us.
Contact Us Now...- DISCLAIMER
JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..
Read more...- FORUM RULES
JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you. You MUST read them and comply accordingly
Read more...- PRIVACY POLICY
We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one. Read our Privacy Policy.
Proceed here...
Massenberg, sasa naanza kuelewa kwanini Marais wastaafu hawakauki Ikulu.
Mkulu ataleta shida kubwa sana kwa haya matamko yake.
Inapaswa mtu awe anamkumbusha kuwa yeye ni Rais.
Ajue kuwa kutoa order zenye utata na ambazo hazitekelezeki kunashusha hadhi yake!
Mkuu tangu lini risasi ikapinda au kukata kona?kwa nini isingepinda na kumtwanga mkuu wake?kilichotokea ni uzembe na kufanya kazi kwa mazoea,au pia inaweza kuwa makusudi jeshi LA police halifai linatakiwa liundwe upya ili tupate watu timamu,Wanabodi,
Usikute kifo cha Akwilina, ni utekelezaji wa agizo hili!. Yule polisi aliyefyatua risasi aliona jambazi fulani lenye silaha miongoni wa waandamanaji wale, na akalifyatulia risasi ili kulinyanganya silaha, lakini risasi hiyo ikapinda na kuingia kwenye dala dala ya kumpata yule malaika wa Mungu.
Hobo, tusiwalaumu sana vijana wa kamanda Sirro, as if tukio la kifo cha Akwilina lilipangwa, ni bahati mbaya tuu, na limetokea katika utekelezaji wa amri halali ya Amiri Jeshi Mkuu!.
Polisi hawakuanza leo matukio kama haya, hivyo hapa ni katika kukumbushana tuu, mambo kama haya yaliishatokea huko nyuma, yametokea sasa, na yatatokea tena!. Tutakumbushana!.
P
Kayasema hayo, tena hadharani?
Askari wamepewa liseni ya kuua yeyote 'anayetuhumiwa' kuwa jambazi?
Kutuhumiwa kuwa jambazi kipimo chake ni kipi? Hicho kipimo anacho askari pekee?
Jambazi mwenye silaha, au jambazi mkaba kabari n.k. wote hukumu zao ziwe ni kifo kwa mkono wa askari?
Mahakama, mahakimu na sheria zipo za nini kama askari wamepewa uamzi wa mwisho!
Huku ndiko kukosa busara na akili ya ubinaadam inayomwondolea heshima.
Ni mwendelezo wa mambo ambayo tayari tumeyashuhudia, askari kutowajibishwa kwa makosa wanayofanya. Aliyemuua mwanafunzi Akwilina ni mfano wa haya anayoyasemea sasa hivi kila mtu ajue.
Mwisho wake ni nini, askari akimuua mpizani wa serikali au yeye mwenyewe asisumbuliwe? Apandishwe cheo?
[emoji16][emoji16][emoji16] View attachment 973731
angalia hotuba yake wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeo maafisa wa polisi pale kurasiniMkuu sijaelewa vizuri fafanua tafadhali.....
Hahaaaaaa watatuua[emoji16][emoji16][emoji16] View attachment 973728
Huyu atapelekwa ICC, haya yanawekwa kwenye records!Wakuu habari za leo?
Nimemsikia Mh Rais wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo yandani kuwa endapo askari polisi akifanikiwa kumuua mtuhumiwa wa ujambazi basi yeye hataki kusikia eti askari wake amewekwa mahabusu kwajili ya uchunguzi. Amemtaka IGP kumpandisha cheo na kumpatia zawadi zingine ikiwemo kumuongezea mshahara wake badala ya kumsweka rumande kwa uchunguzi.
Je ni sahihi kwa Mkuu wa nchi kutamka maneno yale tena hadharani??
Kila mara tumekuwa tukiwalalamikia Polisi kwa kuwabambikizia kesi raia vp kwa maneno yale kweli Mh Rais ni Mtetezi wa Wanyonge au ndiye kitanzi kwa Wanyonge??