Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

".....Na huyo polisi atakayemnyang'anya jambazi silaha msimpeleke mahakamani bali mpandisheni cheo...!'
Polisi katimiza wajibu wake kafanikiwa kumnyang'anya jambazi silaha! Ni ujasiri ni jambo jema sasa kwanini apelekwe mahakamani tena?[emoji15] [emoji144]
Uone kama ni ujumbe wa kawaida uone kama ni ujumbe unaomaanisha majambazi tunayofahamu
Tafakari kifo cha Mwangosi RIP
Tafakari matendo ya Lameck M. huko alikotoka aliyoyafanya na nafasi aliyo nayo sasa
Sijawahi kuona askari akitimiza wajibu wake kwa usahihi na weledi kisha ashtakiwe. ..kuna jambo lingine baya kabisa lilimaanishwa hapa.....taratibu rangi halisi za mkakasi zinajifunua
 

mnafiki tu ww, bahati mbaya hauna madhara yeyote kwa andiko lako.
 
wewe si mwanga, endelea kujifunza uchawi,
kama una ndugu anaeyefanya ujambazi, mpatie tu mbegu za ufuta akalime
 
Siku hizi watu wanazungumza kwa "parables!" karibu mtaa huu
Hili la Polisi Kuruhusiwa 'Kuwanyanganya' Silaha Majambazi!, na Kupandishwa Vyeo, Limekaaje?!...

Pasco
 

Mkuu heshima kwako. Bila shaka una kipaji au IQ ya kipekee. Nikiri kuwa mimi ni mmoja wa wenye kufikiri kuwa kauli za rais au kiongozi yeyote wa umma lazima ziwe katika mfumo wa 1+1=2 au 2+5=7 (kwa mfano wako) ili kutoruhusu mikanganyiko yoyote ya uelewa kwa wananchi. Ndivyo tulivyozoea kwa awamu zilizopita na kwa viongozi wa nchi nyingine.

Safari hii itabidi niwe nasoma mabandiko yako kuelewa kauli za Magufuli. Lakini unao uhakika kuwa Mheshimiwa huyu hana mielekeo ya kuachia "gaffes" katika "haraka" zake za kutoa maagizo ya kuvutia wanyonge?
 
Ana maana "wananchi wenye hasira kali walimkabili jambazi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…