Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Vyovyote vile watu watakavyo elewa
Kisha sema
Kama wamebeba bunduki lengo sio kuichezea au maonyesho.

Tumechoka
Dawa ya moto ni moto

Waje sasa wale walio poteza netwerk wakati wa kuzaliwa waanze kuwatetea Majambazi waone
Naunga mkono hoja. MACHADEMA yanatokwa na mapovu kutetea majambazi.
 
ukiliangalia kwa juu juu ni jambo zuri. lakini ukienda ndani ni balaa. time will tell...
 
Matokeo yake yanaweza kuwa hayo. Na hata pia yale ya akina Abdalah Zombe kule kwenye msitu wa pande ya kuwaua akina Sabinus Chigumbi na wenziye kisha kuja kutudanganya kuwa wameua majambazi.

Wenye akili finyu hilo wataliona
Lakini sisi ni kukomesha ujambazi
Kama una ndugu jambazi muandalie shimo
 
Acha kuzuga ww hujui kauli ya rais ina impact gani ktk utekelezaji?


Ngoja nikuulize swali, tangu Raisi wa JMTZ aliposema kwamba wanaovunja Sheria kwa kupita kwenye njiia za DART wakamatwe na magari yao yang'olewe matairi, je ni wangapi ambao magari yao yameng'olewa matairi mpka leo hii? Na je madereva wanaopita br. za Dart wameongezeka au wamepungua tangu Raisi aseme vile?
 
Safi sana. Nitashangaa UKAWA watakapoanza kutetea majambazi lakini wananchi wakiuawa na majambazi wanailaumu serikali
Ni kweli..... Hata wakina mwangosi walikuwa majambazi wa demokrasia na ndo maana waliuawa na polii-ccm!!
 
Naunga mkono hoja. MACHADEMA yanatokwa na mapovu kutetea majambazi.
Tumesha yazoea Machadema
haya ni Ndumila kuwili
cc438777fbe407a5c1f35a2d0deea727.jpg
 
Nakunukuu ''Rais ameagiza kuua majambazi yenye silaha hata kama likijisalimisha''. Mkuu unauhakika Mh rais ametamka hayo maneno?. Hotuba ya rais ilikua wazi kabisa na yenye lengo la kuwapa moyo askari wakufanya kazi bila woga ili wananchi ukiwemo na wawe muwe salama. Unadhani jambazi akija na silaha kwako, anakua amekuja nayokwaajili ya maonesho?. Lakini sio mbaya kwa siasa zenu za namna hii, katika utawala huu mtakula magodoro.
 
mpaka uuziwe kesi lazima kuna jambo. kwann uwe mwoga. nyie si ndio mliokuwa mnapiga kelele kuwa china wananyonga ukifanya makosa

You are naive kama haujui maana ya kuuziwa kesi. Si lazima kuwe na kosa limetendeka. kukiwa na SABABU TU inatosha watu kutengeneza kosa kwa ajili ya mlengwa. No need to reply to this, I know you don't want to understand.
 
UKAWA KUITISHA MAANDAMANO YA KUWATETEA MAJAMBAZI YASIULIWE NA POLISI.

TAARIFA ZINASEMA UKAWA WAKO TAYARI KUUNGANA NA POLISI WAKATI WA MAPAMBANO NA MAJAMBAZI ILI WAWEZE KUWATAMBUA MAJAMBAZI YENYE SILAHA NA KUJARIBU KUWABEMBELEZA WASIVAMIE RAIA.

KATIKA HARAKATI ZAO ..UKAWA WAMEENDA MBALI NA KUANZA KULIFIKISHA MAHAKAMANI JESHI LA POLISI KISA TU LINAPAMBANA NA UHALIFU ULIOKITHIRI...

MASELA HAWA WA UKAWA PIA WANATARAJIA KUBADILI GIA ANGANI NA KUMPA MKUU WA KIKOSI CHA MAJAMBAZI UWANACHAMA WA CHADEMA FASTA FASTA ILI AWEZE KUGOMBEA URAIS WA NCHI HII MNAMO MWAKA 2020 ...

IKIWA UKAWA WATAFANIKIWA KATIKA HILI BASI ILE ADHMA YAO YA NCHI KUTOTAWALIKA ITAKUWA IMETIMIA NA WAO WATAENDA DUBAI NA UJERUMANI KULA BATA.

MAELEKEZO YA KAMATI KUU YAO KWA SASA NI KUSUSIA SHUGHULI ZOTE ZA POLISI IKIWEMO KUTOKUPIGA SIMU POLISU KWA KUTUMIA KITUO KIPYA CHA POLICE CALL CENTER PALE WANAPOVAMIWA MAJUMBANI MWAO WAMEWAASA WANANCHI KUFANYA HIVYI HIVYO ILI KUWALINDA WAPIGA KURA WAO YAANI MAJAMBAZI VIBAKA NA WALA NDUMU.

NIKIRIPOTI KUTOKA UFIPA NI MIMI MWANDISHI WENU NILIYESOMEA SPECIAL DIPLOMA
 
mtu ukifuatilia vzr mauaji ya polisi na raia yaliyotokea "Mkuranga" na "bunju" hyo ni hapa dar tu kamwe huwez kuja na judgement za kijinga hivo kupinga uamuz wa rais,,,,
ID yako inaonesha kabisa ww team pinzani wale wenye tabia ya kutafutw kiki kupitia hoja za watawala,kwa taarifa yako mnafeli sana safar hii,nyumbu ni nyumbu tu.
 
UKAWA KUITISHA MAANDAMANO YA KUWATETEA MAJAMBAZI YASIULIWE NA POLISI.

TAARIFA ZINASEMA UKAWA WAKO TAYARI KUUNGANA NA POLISI WAKATI WA MAPAMBANO NA MAJAMBAZI ILI WAWEZE KUWATAMBUA MAJAMBAZI YENYE SILAHA NA KUJARIBU KUWABEMBELEZA WASIVAMIE RAIA.

KATIKA HARAKATI ZAO ..UKAWA WAMEENDA MBALI NA KUANZA KULIFIKISHA MAHAKAMANI JESHI LA POLISI KISA TU LINAPAMBANA NA UHALIFU ULIOKITHIRI...

MASELA HAWA WA UKAWA PIA WANATARAJIA KUBADILI GIA ANGANI NA KUMPA MKUU WA KIKOSI CHA MAJAMBAZI UWANACHAMA WA CHADEMA FASTA FASTA ILI AWEZE KUGOMBEA URAIS WA NCHI HII MNAMO MWAKA 2020 ...

IKIWA UKAWA WATAFANIKIWA KATIKA HILI BASI ILE ADHMA YAO YA NCHI KUTOTAWALIKA ITAKUWA IMETIMIA NA WAO WATAENDA DUBAI NA UJERUMANI KULA BATA.

MAELEKEZO YA KAMATI KUU YAO KWA SASA NI KUSUSIA SHUGHULI ZOTE ZA POLISI IKIWEMO KUTOKUPIGA SIMU POLISU KWA KUTUMIA KITUO KIPYA CHA POLICE CALL CENTER PALE WANAPOVAMIWA MAJUMBANI MWAO WAMEWAASA WANANCHI KUFANYA HIVYI HIVYO ILI KUWALINDA WAPIGA KURA WAO YAANI MAJAMBAZI VIBAKA NA WALA NDUMU.

NIKIRIPOTI KUTOKA UFIPA NI MIMI MWANDISHI WENU NILIYESOMEA SPECIAL DIPLOMA
Hahaha basi kazi ipo
 
mtu ukifuatilia vzr mauaji ya polisi na raia yaliyotokea "Mkuranga" na "bunju" hyo ni hapa dar tu kamwe huwez kuja na judgement za kijinga hivo kupinga uamuz wa rais,,,,
ID yako inaonesha kabisa ww team pinzani wale wenye tabia ya kutafutw kiki kupitia hoja za watawala,kwa taarifa yako mnafeli sana safar hii,nyumbu ni nyumbu tu.
7e31e18e7c69a672865586cd3adcec47.jpg
 
Hii Magu tumuunge mkono! Je Majambazi wasio na bunduki walijilimbikizia Mali na wamejificha serikalini? je hao vp?
 

Wanabodi,

Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.

Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.

Agizo hilo limepokelewa kwa shangwe na makofi kwa kila aliyekuwe pale.

Rais huku akisema kwa msisitizo kwa kutumia fasihi ya "kuwanyanganya silaha", kwa vile majambazi wanatumia silaha, zenye risasi kufanya ujambazi, na jeshi la polisi nalo wanazo silaha zenye risasi, haoni kwa nini majambazi hayo yasinyang'anywe silaha zao!. Namna pekee ya kunyanganya silaha jambazi mwenye silaha, ni kumalizana nao, papo kwa papo!.

Sina shaka kabisa na nia ya dhati ya rais Magufuli, kutoa amri, hiyo, kufuatia nchi na wananchi kuchoshwa na vitendo vya ujambazi kuongezeka, hivyo majambazi wakijua kuwa wakikamatwa watauwawa right away, then, amri hii badala ya kupunguza ujambazi wa kutumia silaha, ndio kwanza utaongeza impunity kwa majambazi wanaotumia silaha, na wakati huo huo kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!.

Sio majambazi wote wanaotumia silaha, zile silaha zao zina risasi!, wengine huzitumia kutishia tuu, lakini hawana nia ya kufanya mauaji, na kuna wengine hubeba silaha ambazo hazina risasi, na wengine hutumia toy pisto!, lakini kufuatia amri hii, polisi ndio kwanza wamekuwa licenced to kill!.

Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleke majambazi wanaotumia silaha, mbele ya sheria, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubirria kupandishwa vyeo!. Just imagine mashindano ya kupanda vyeo miongoni mwa polisi wetu!.

Kama wanasheria wetu, hawatashitushwa na amri hii ya rais, nitaamini sasa Watanzania wameanza kumwelewa rais wetu, na ukiisha elewa, huna haja ya kuhoji!.

Angalizo: Sitetei vitendo vyovyote vya uhalifu wa aina yoyote, bali natetea utoaji wa haki!, hata jambazi anayetumia silaha, anastahili kutendewa haki!. Natolea mfano wa nchi mbili za Maekani na Uingeeza. Miaka ya nyuma nchi zote hizi zilikubwa na vitendo vingi vya mauaji. Uingeeza ikafuta adhabu ya kifo!, vitendo vya mauaji, vikapungua kwa kiasi kikubwa!. Maekani ikaendelea na adhabu ya kifo, vitendo vya mauaji bado vimeongezeka!.

Amri ya kuwaua majambazi papo kwa papo, haitapunguza ujambazi, bali itawafanya hao majambazi ndio kugeua wauwaji wakuu, kwa hoja za "ama zao, ama zetu" na kwenye tukio lolote la ujambazi wa kutumia silaha, polisi wakitokea, sasa sio tena kutuliza amani bali kufanya a blood bath!, hivyo polisi sasa pia watakuwa ni target ya majambazi!.

Kwetu sisi waandishi, ikitokea polisi wakakutana na gun mike, au boom mike, au hata kamera wakaiona ni kama sihaha!, kama ilivyotokea mwa Daudi Mwangosi!, askai mhusika, atapandishwa cheo!. Kama wale vija wa Zombe, sasa watawadiwa vyeo!.

Huko nyuma niliwahi kushauri, kama katiba ni kikwazo, rais Magufuli, aiweke pembeni katiba na badala yake atawale kwa kutumia 'presidential decrees' tuu!. Hivyo kwa amri hii ya polisi kuua majambazi papo kwa papo, kama mahakama ni kikwazo, pia anaweza kuiweka pembeni, na kuwatumia polisi kutoa hukumu za kifo cha papo kwa papo, tena hili litaokoa fedha nyingi sana, maana majaji wa mahakama zetu, wanahudumiwa kwa gharama kubwa sana!.

Wasiwasi wangu kwa amri kama hizi, sio ili kuokoa maisha ya majambazi wanaotumia silaha, au kuwaacha tuu majambazi wanaotumia silaha kuua, lakini wao kuuliwa tuinawatetea!, no!, wasiwasi wangu ni utekelezaji wa amri za aina hii, zisije kuwa kwa majambazi ni mwanzo tuu, baadae amri kama hizi za 'kinyemela' zikaelekezwa kwa makundi mengine, yanayoonekana ni kero!.

Hata Adolfu alipoanza, alianza hivi hivi kwa kushangiliwa na umati wa watu!, ni baadae sana, ndipo watu wakajuta!, chonde chonde twendeni taratibu jamani tusije kujuta!.

Jumamosi Njema.

Pasco


Unaongea hivyo kwa vile hujawahi kukumbwa na tukio la ujambazi
 
Back
Top Bottom