Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Hili la Prof. Assad kumaliza kipindi chake limekaa kisiasa zaidi na siyo kisheria

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo. Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"
_
Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.

Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti.

Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?

Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.

Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je, hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.

Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof. Assad amezaliwa tarehe 06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected!
Mkuu unafikiri kila kitu kinaandikwa kwenye Katiba tuuu?? Nenda kasome sheria iliyoanzisha ofisi ya CAG. Nafikiri wameshaiweka humu jamvini.
 
Mnayaona tu yale mnayooneshwa lakini yaliyofichwa nyuma hamuwezi kuyaona kwasababu ya umbumbumbu wenu!! Huko nyuma msikokuona ndio kumejaa uchafu usiosafishika!!!
Hahaha wewee hii sio Kama chadome..yanayofichwa nyuma Yana madhara yapi labda tuambie basi..kwa sababu haya tunayoyaona tuu ni makubwa kuzidi kawaida..sasa yaliyofichwa Kama yapo hayana impact..umensoma
 
Kisheria CAG anatumikia miaka 5, na yuko open for reappointed kwa miaka 5 mingine ila akifikisha miaka 60 ndio amestaafu

Kwenye reappointiment, rais halazimishwi kum reappoint, hivyo Rais Magufuli yuko right kumteua mtu mwingine yoyote na CAG Prof. Assad is sent to early retirement. Ataendelea kulipwa mshahara na marupurupu yote ya CAG hadi atakapotimiza umri wa miaka 60, ndipo atastaafu rasmi na kulipwa mafao yake na kiinua mgongo cha 80% ya the current CAG.
P
Pasco umekuwa bush lawyer siku hizi
Unajua maana ya neno "shall" kwenye context ya kisheria?
Najua unajua ila siku hizi akili zako zimepotelea kwenye kunyemelea uteuzi
 
Mnayaona tu yale mnayooneshwa lakini yaliyofichwa nyuma hamuwezi kuyaona kwasababu ya umbumbumbu wenu!! Huko nyuma msikokuona ndio kumejaa uchafu usiosafishika!!!
Jomba huwezi tudanganya wananchi kwa biashara za kufikirika..tafuta mbinu nyingine..hii imefeli
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Km wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata upotevu wa pesa
CAG ana miaka 58, sheria inasema umri Wa kustaafu, hivi kila anayepinga uvunjwaji Wa katiba Ni upinzani tu?
 
...........In this context, Section 53 (2) of
the Interpretation of Laws Act (CAP 1 R.E. 2002) is important. It
provides:-
(2) Where in a written law the word “shall” is
used in conferring a function, such word
shall be interpreted to mean that the
function so conferred must be performed.
Do you know the word "eligible" means in law?
 
Iko hivi, tenure ni miaka 5. Iwapo CAG akiwa chini ya any kind of investigation (yeye Bunge lilimuita kujieleza/kujibu tuhuma), sasa huwezi jua recommendation ya huo muhimili ilikuwaje. Be matured, na mamlaka hailazimiki kuendelea na mtu kama inaona ana kiuka miiko ya kazi zake.
Na umri Wa kustaafu vipi? Umri Wa kustaafu Ni miaka 60 Na CAG Assad kwa sasa ana 58.
 
Wanasheria pamoja na asasi za kijamii kama LHRC waombe Mahakama Mkuu itoe tafsiri ya katiba kuhusu muda wa utumishi wa CAG baada ya kuteuliwa uko kinyume na vifungu vya katiba tajwa hapo #32
Pia hata wabunge wetu kama wako serious wamfungulie rais mashtaka ya kuvunja katiba, hasa wabunge wetu Wa upinzani.
 
Pascal umesoma sheria hilo neno ‘SHALL’ kwenye sheria lina maana kuwa ni uamuzi wa mteuaji kuongeza au kutoongeza mkataba? Au halina maana nyingine ambayo haijazingatiwa.

Kwasaaa wanajitoa ufahamu.
Anajua sana analoliongea na anajua walio weka hilo neno SHALL walimaaisha nini . Ni basi tu amechagua ujinga kwenye hili ili kutafua teuzi.
 
...........In this context, Section 53 (2) of
the Interpretation of Laws Act (CAP 1 R.E. 2002) is important. It
provides:-
(2) Where in a written law the word “shall” is
used in conferring a function, such word
shall be interpreted to mean that the
function so conferred must be performed.
Ha ha ha ha ha, unachekesha sana bro, sijui nikuite bush lawyer, doo! Mbona hiyo Article ipo very clear. C.A.G atahudumu kwa miaka mitano
...........In this context, Section 53 (2) of
the Interpretation of Laws Act (CAP 1 R.E. 2002) is important. It
provides:-
(2) Where in a written law the word “shall” is
used in conferring a function, such word
shall be interpreted to mean that the
function so conferred must be performed.
The Controller and Auditor General shall hold office for the fixed term of five years and shall be elligible for renewal for one term only.
Kwa wale tuliosoma Legal drafting tena ile ya Prof. Humud Majamba pale nyuma ya Mawasiliano a.k.a SIM2000 Aarticle hii ina sentence mbili ambazo zenye maana mbili kama ifuatavyo na hapa ni kwa kuzingatia neno "Shall" ambalo limetumika mara2.
1. C.A.G lazima atumikie nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano( unless zitokee sababu zilizoainishwa ambazo zinaweza kufanya aondolewe kabla ya miaka hiyo.
2.C.A.G anaweza kuongezewa muda wa miaka mingine mitano tu baada ya miaka mitano ya kwanza kuisha.
 
Unamuuliza Nani sasa jomba..aliyemteua ndio anajua undani na kwanini..wewe inakuhusu. Usipoteze muda wako jomba..mpigie simu aliyemteua akuambie sababu..sisi huku tutakuwa tunaongopeana tu
Hapana mkuu.Mimi ni mtanzania.Na Assad aliteuliwa atulindie mali yetu ya umma.Nina haki kujua mkuu.
 
Kisheria CAG anatumikia miaka 5, na yuko open for reappointed kwa miaka 5 mingine ila akifikisha miaka 60 ndio amestaafu

Kwenye reappointiment, rais halazimishwi kum reappoint, hivyo Rais Magufuli yuko right kumteua mtu mwingine yoyote na CAG Prof. Assad is sent to early retirement. Ataendelea kulipwa mshahara na marupurupu yote ya CAG hadi atakapotimiza umri wa miaka 60, ndipo atastaafu rasmi na kulipwa mafao yake na kiinua mgongo cha 80% ya the current CAG.
P
Safi sana kwa kasomo kafupi
 
Angekuwa Hana Nia ya dhati hivi ingewezekana vipi akanunua madege karibu kumi ndani ya miaka minne..hujiulizi..wewe...hata kidogo..haya mapesa si yote angeyatia ndani..angeyalamba yote, wee vipi bana..
Pole ndugu, huko kwenye manunuzi ndo watu hasa viongozi wanakojipatia 10%
 
Hahaha wewee hii sio Kama chadome..yanayofichwa nyuma Yana madhara yapi labda tuambie basi..kwa sababu haya tunayoyaona tuu ni makubwa kuzidi kawaida..sasa yaliyofichwa Kama yapo hayana impact..umensoma

Si mnafurahia na kushangilia ndege hata kama hamna uwezo wa kununua tiketi za kupanda hizo ndege; ombeni basi muoneshwe mahesabu ya mapato na matumizi toka hizo ndege zilipoanza biashara. Mbona JIWE anaficha hayo mahesabu na yeye mwenyewe alisema angekwenda kuzikagua ingawa sina hakika kama anaujuzi huo!!
 
Back
Top Bottom