Uchaguzi 2020 Hili la Sheikh Ponda liacheni. Hatua ya Ponda ni kwa maslahi ya Waislam na Watanzania

Sasa swali Lina Kuja kwa sababu kuna watu wengi jela bila hatia Ndio sisi tufurahie mateso wanayo pata viongozi wetu wa dini?
Kama wewe unafurahia ili uone Kane umesoma haupo peke yako ndani ya waislamu wapo wanafiki wengi hata Enzi za MTUME SAW walikuwepo na watakuwepo
I wish unajua kusoma Quran soma surat almunafiquun
Ni sura Ina husu wanafiki
Hayo masuala ya kufurahia yanaingiaje hapa? mimi nazungumzia suala la kuwaambia waislamu wampigie kura Lissu et kisa kasema atawatoa masheikh wa uamsho wakati huko jela kuna waislamu wengine kibao tu au wewe unaona sawa tu kwa hao waislamu wengine kuwepo huko jela ila roho inakuuma kuona masheikh wa uamsho tu kuwa jela?

Mababu zetu huko walishirikiana na Nyerere ila sasa hivi zimebaki lawama tu,sasa Ponda anataka tumchague Lissu.
 
Mimi Sina uhakika kama kuna waislamu wengine jela bila hatia
Ila mimi ninauhakika kuna viongozi wetu sio tu wamuamsho Bali kuna mashekh wengi tu wapo jela kwa makosa ya ugaidi kuanzia arusha mpaka mtwara
Sasa wewe kama unaona wema ni kumpigia kura magufuli fanya hivyo ila waislamu wengi tunasikia uchungu kwa nini tunyanyasike katika nchi yetu?
 
Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu
Nawasalimien Assalam Aleikum.

Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu.

Mmepinga vikali kauli yake kuwa Waislamu wamekubaliana kumchagua Ndugu Lissu katika uchaguzi huu, naomba niwakumbushe yafuatayo.

1. Je, mnafahamu kuwa kuna waraka wa shura ya maimamu unaoelezea mtu gani anafaa kuchaguliwa?
Kabla hamjamuita Sheikh Ponda muongo kwamba eti waislamu hawana makubaliano juu ya mtu gani wa kumchagua, ningependa muurejee waraka wa majuzi wa shura ya maimamu, umetoa orodha ya Sifa nyingi sana za mtu anayefaa kuchaguliwa sifa mojawapo awe mtu anayependa HAKI.

Sasa nyie Masheikh wetu hebu tuambieni, kama kwenye waraka wa Shura maimamu wamekemea suala la kutokuwepo kwa haki nchini katika utawala huu wa rais Magufuli, hapo Shura ya Maimamu ina maana gani inaposema waislamu wachague mtu wa HAKI?, Kiufupi shura inaelezea kuhusu kubadili utawala kwenye uchaguzi huu na hicho ndicho Sheikh Ponda anachokifanya sasa hivi, Yaani kujaribu kusimamia azimio la Shura la kuondoa utawala wa dhulma na kuleta nchini utawala wa HAKI. Waislamu tunasimama na wapenda haki wote nchini bila kujali dini zao.

2. Wahadhiri na Masheikh wetu mmeonyesha double standard
Kwenye hiyo press conference mliyofanya hapo jana, mlikuwa chumba kimoja na Masheikh wanaoipigia kampeni CCM waziwazi, mlikuwa na Alhadi (huyu siyo sheikh anyway ni mjanjamjanja tu aliyesoma dini), Pia alikuwepo Sheikh Majini, wote hawa wameipigia kampeni CCM waziwazi, Tena huyo Alhadi amefanya kufuru kubwa kwa kuomba kwa jina la asiye ALLAH, na mnafahamu Qur'an imefundisha nini kuhusu wale wafanyao shirki kwana hukumu gani mbele ya ALLAH.

Kwenye hiyo press conference nilitegemea Ustaadh Mazinge umpe kwanza huyo Alhadi vifungu vya Bible na Qur'an kuonyesha kuwa amekosea kwa sababu wewe ni mtaalamu wa elimu ya Comparative religions (yaani malinganisho ya dini mbalimbali kwa kutumia vitabu vyao) na tunakupenda na kukuheshimu sana kwa kazi uliyoifanya kwa Takriban zaidi ya miaka 25 sasa. Tulitegemea umuambie Alhadi auombe radhi umma wa Waislamu kwa kuidunisha dini yetu, wakati inapaswa iwe juu na kusiwepo kuchanganya haki na batili hata kidog katika dini. Sasa utamnyoosheaje Kidole Ponda wakati pembeni yenu wamekaa wakosaji wa wazi?

3. Waislamu tunaumizwa sana na Masheikh wetu walioko jela kiuonevu
Leo hii sisi ni wakiwa, Masheikh wetu wako jela, wako jela Dar, Arusha, Mtwara, wako Jela kila mahali. Sisi waumini tunaumia, nyoyo zetu zimepigwa ganzi, tumejishika tama, tunahuzunika sana. Ni nani atakayetufundisha neno la ALLAH, ni nani atakayetupa faraja ya mtume wetu, ni nani atakayetufundisha mema tupate faida za duniani na mbinguni kama siyo Masheikh wetu walio jela?. Wamewekwa ndani na serikali ya CCM, wananyakuliwa mmoja mmoja kama mwewe anyakuavyo kifaranga na kuswekwa ndani. Sasa kweli nyie wahadhiri Mnamnyooshea kidole Ponda mtu anayetaka aingie madarakani mtu wa HAKI ili awatoe jela Masheikh wetu?.
Uislamu umefundisha, ukiona Jambo baya liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea, na ukishindwa hata kukemea basi chukia, ila hiyo option ya mwisho ni udhaifu wa Imani. Hebu nyie wahadhiri wetu mnaomnyooshea kidole Sheikh Ponda leo, Mmekemea lini mbele ya hadhara ya Watanzania suala la Masheikh wetu kukaa ndani bila haki?

4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu
Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20.

Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote?

Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki.

5. Masheikh na wahadhiri wetu tunaomba mtuache, tarehe 28 tuna jambo letu
Dhulma huondolewa kwa mkono na kauli. Kauli yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU na mkono wetu ni Kura zetu. Tunawaomba wahadhiri wetu mtuache, hii ni nafasi adimu na adhimu ya kuondoa Dhulma na Uonevu katika nchi. Huyu Tundu Lissu anayetetea haki zetu Si Muislamu lakini ni Mtu wa Haki, huyu hana tofauti na Annaajashi (King Negus of the ancient Ethiopia), alikuwa ni Mfalme Mkiristo lakini mpenda Haki na muadilifu, huyu ndiye aliyeunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuwapa hifadhi katika himaya yake wanafunzi wa mtume waliokimbia mateso na manyanyaso ya wapagani wa Makka. Tundu Lissu ni mkiristo mpenda haki, huyu ndiye anayetufaa na siyo yule ambaye hatupi nafasi za kutosha kwenye serikali yake halafu anatuhadaa kutujengea misikiti, lini sisi tumewahi kuwa na shida ya kujengewa msikiti na mtawala?. Sisi Shida yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU!

Mwisho kabisa nitoe nasaha kwa Watanzania wenzangu
Hatua ya Sheikh Ponda ni hatua ya kizalendo sana, Si hatua ya Udini hata kidogo, Maana kama Ponda angekuwa mdini maana yake angemuunga mkono Hashim Rungwe au Lipumba ambao ni waislamu wenzie. Ponda kamuunga mkono Lissu ambaye yeye Lissu na Magufuli ni wa Imani moja na dhehebu moja ila tofauti yao kuu ni kuwa Lissu ni mtu wa Haki wakati Mgombea wa CCM si mtu wa haki hata kidogo (Ana double standard na ndimi mbili). Tuungane kumuweka Lissu madarakani ili atuondolee dhulma ya kutisha katika nchi!
Huyu shehe ni mtata tu
 
Kuna sehemu nimezungumzia kuendesha serikali? mie nimemzungumzia Lissu kama mgombea urais,sasa hayo mengine sijui umeyatoa wapi.
Umeuliza Mh Lissu kafanya nini ? Sasa afanye kama nani? Kumbuka alikuwa mbunge tu je kipi hajafanya ? Naamini uko timamu na unajua kazi ya mbunge na pia unapata taarifa za jiwe kuwa hapeleki maendele kwenye jimbo walikochagua upinzani wakati huko huo anasema maendeleo hayana chama
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Nakuheshimugi sana Mkuu. Mungu akubariki kwa maandiko yako yaliyojaa busara na hofu ya Mungu.
 
Hahahaha

Kipozeo kazi yake kuzungumzia m*#$&%o.

Ulie ni mkusanyiko wa waganga wa kienyeji na waganga njaa wa kindengereko, kisambaa na manyema

Huu mwaka CCM kupitia kile kijamaa kinaitwa Polepole sijui , mmeamua kuongea ukweli toka mioyoni kwa kukubali kuwa nyie hampo kwa ajili ya wananchi maskini. Kamwe hamjawahi kuwa. Zaidi ni kwamba mnastahili kuondoka madarani. Mmekula mmevimbiwa, hamna UTU. Hadharani mnawatweza walalahoi walipakodi mnazofuja!
 
Ndio umeongea nini hapo? bado unawazungumzia masheikh tu yani kana kwamba hao masheikh ndio tatizo pekee la waislamu Tz.

Yani wewe hao masheikh tu ndio roho inakuuma kuwa huko jela wakati kuna waislamu wengine kibao tu huko ila huna habari nao.
😂😂😂 jamii forum bhan hadi raha, nakutana na vichwa vina majibu hadi vinafurahisha 💪
 
😂😂😂 unajua nashindwa kuelewa kwanini baadhi ya watu mna hasira as if Magufuli kakwamisha maisha yenu sana, inabidi mkajengwe kisaikolojia nyie mkae sawa
Tumechoka kuona damu za watu
Hatupendi mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana
Hatupendi kuona watu wanafilisiwa
Hatupendi kuona masheikh wanateswa na kufia jela
Haya mambo watanzania hatujawahi kuona tangu uhuru
 
Mtu anyependa haki anatukana wazee kuwa ni professorial rubush, anashiriki ndege na mali za nchi zikamatwe, anashiriki kwa wezi wa madini yetu, anashiriki nchi isipate misaada muhimu, anadharau kwa watu wengine na kujiona yeye ni msomi kuliko wengine, anataka kujitenga na zanziba, aliyemtukana babawa taiga na kumzodoa.

Anapendelea ndoa ya jinsia moja.

Je, huyo ndi mnamtaka?
Hujui wanaomtaka ni wala Tako mtu mwenye akili timamu hawezi kuchagua mtu anaetetea ulaji wa tako.
 
Kwenu Masheikh na wahadhiri wetu
Nawasalimien Assalam Aleikum.

Jana mmefanya press conference, mmezungumza na kutoa kauli yenu kuhusu hatua ya Sheikh Ponda kusimama na kuwataka Waislamu na wananchi wamchague mheshimiwa Lissu katika uchaguzi huu.

Mmepinga vikali kauli yake kuwa Waislamu wamekubaliana kumchagua Ndugu Lissu katika uchaguzi huu, naomba niwakumbushe yafuatayo.

1. Je, mnafahamu kuwa kuna waraka wa shura ya maimamu unaoelezea mtu gani anafaa kuchaguliwa?
Kabla hamjamuita Sheikh Ponda muongo kwamba eti waislamu hawana makubaliano juu ya mtu gani wa kumchagua, ningependa muurejee waraka wa majuzi wa shura ya maimamu, umetoa orodha ya Sifa nyingi sana za mtu anayefaa kuchaguliwa sifa mojawapo awe mtu anayependa HAKI.

Sasa nyie Masheikh wetu hebu tuambieni, kama kwenye waraka wa Shura maimamu wamekemea suala la kutokuwepo kwa haki nchini katika utawala huu wa rais Magufuli, hapo Shura ya Maimamu ina maana gani inaposema waislamu wachague mtu wa HAKI?, Kiufupi shura inaelezea kuhusu kubadili utawala kwenye uchaguzi huu na hicho ndicho Sheikh Ponda anachokifanya sasa hivi, Yaani kujaribu kusimamia azimio la Shura la kuondoa utawala wa dhulma na kuleta nchini utawala wa HAKI. Waislamu tunasimama na wapenda haki wote nchini bila kujali dini zao.

2. Wahadhiri na Masheikh wetu mmeonyesha double standard
Kwenye hiyo press conference mliyofanya hapo jana, mlikuwa chumba kimoja na Masheikh wanaoipigia kampeni CCM waziwazi, mlikuwa na Alhadi (huyu siyo sheikh anyway ni mjanjamjanja tu aliyesoma dini), Pia alikuwepo Sheikh Majini, wote hawa wameipigia kampeni CCM waziwazi, Tena huyo Alhadi amefanya kufuru kubwa kwa kuomba kwa jina la asiye ALLAH, na mnafahamu Qur'an imefundisha nini kuhusu wale wafanyao shirki kwana hukumu gani mbele ya ALLAH.

Kwenye hiyo press conference nilitegemea Ustaadh Mazinge umpe kwanza huyo Alhadi vifungu vya Bible na Qur'an kuonyesha kuwa amekosea kwa sababu wewe ni mtaalamu wa elimu ya Comparative religions (yaani malinganisho ya dini mbalimbali kwa kutumia vitabu vyao) na tunakupenda na kukuheshimu sana kwa kazi uliyoifanya kwa Takriban zaidi ya miaka 25 sasa. Tulitegemea umuambie Alhadi auombe radhi umma wa Waislamu kwa kuidunisha dini yetu, wakati inapaswa iwe juu na kusiwepo kuchanganya haki na batili hata kidog katika dini. Sasa utamnyoosheaje Kidole Ponda wakati pembeni yenu wamekaa wakosaji wa wazi?

3. Waislamu tunaumizwa sana na Masheikh wetu walioko jela kiuonevu
Leo hii sisi ni wakiwa, Masheikh wetu wako jela, wako jela Dar, Arusha, Mtwara, wako Jela kila mahali. Sisi waumini tunaumia, nyoyo zetu zimepigwa ganzi, tumejishika tama, tunahuzunika sana. Ni nani atakayetufundisha neno la ALLAH, ni nani atakayetupa faraja ya mtume wetu, ni nani atakayetufundisha mema tupate faida za duniani na mbinguni kama siyo Masheikh wetu walio jela?. Wamewekwa ndani na serikali ya CCM, wananyakuliwa mmoja mmoja kama mwewe anyakuavyo kifaranga na kuswekwa ndani. Sasa kweli nyie wahadhiri Mnamnyooshea kidole Ponda mtu anayetaka aingie madarakani mtu wa HAKI ili awatoe jela Masheikh wetu?.
Uislamu umefundisha, ukiona Jambo baya liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea, na ukishindwa hata kukemea basi chukia, ila hiyo option ya mwisho ni udhaifu wa Imani. Hebu nyie wahadhiri wetu mnaomnyooshea kidole Sheikh Ponda leo, Mmekemea lini mbele ya hadhara ya Watanzania suala la Masheikh wetu kukaa ndani bila haki?

4. Sheikh Ponda yuko sahihi, hatua yake ni kwa maslahi ya umma wa kiislamu
Katika nchi hii vyama vya siasa, chaguzi na haki za kikatiba ni vitu halali na vya kisheria. Ni mfumo wa kubadili uongozi ili kila mtu au kundi fulani la jamii kuweka utawala ambao wanahisi watanufaika au kupata ahueni, fursa na manufaa fulanifulani. Napenda kuwafahamisha wahadhiri wetu kuwa kumekuwepo kilio katika jumuia za kiislamu kuhusu Udini wa wazi katika awamu hii, Shura ya maimamu ilitoa waraka wenye kuonyesha kisayansi kabisa teuzi zilizofanywa na awamu hii zinavyonuka udini. Teuzi zimelalia upande wa imani moja mpaka aibu almost kwa uwiano wa 80:20.

Haya kwanza kabisa aliyakemea Sheikh Khalifa na baadae Shura ya maimamu ikatoa waraka mzito, wa kishujaa na wa kukumbukwa juu ya jambo hili. Sasa kwa ubaguzi huu wa dhahiri kabisa usio na aibu nyie wahadhiri wetu mnaanza kumpiga mishale mtu ambaye anatumia taratibu halali zilizoko nchini ili kusimika utawala utakaotenda haki kwa wote?

Hatua anayoichukua leo Sheikh Ponda ni hatua kama ambazo Masheikh wetu walichukua kumsaidia Nyerere ili kumtoa mkoloni ili kusimika utawala mpya utakaoheshimu maslahi yao na haki yao. Sheikh Ponda hana tofauti na masheikh akina Tambaza, Ramia, Chaurembo na wengineo waliosimama bega kwa bega na Nyerere kung'oa utawala dhalimu na kuleta utawala wa haki.

5. Masheikh na wahadhiri wetu tunaomba mtuache, tarehe 28 tuna jambo letu
Dhulma huondolewa kwa mkono na kauli. Kauli yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU na mkono wetu ni Kura zetu. Tunawaomba wahadhiri wetu mtuache, hii ni nafasi adimu na adhimu ya kuondoa Dhulma na Uonevu katika nchi. Huyu Tundu Lissu anayetetea haki zetu Si Muislamu lakini ni Mtu wa Haki, huyu hana tofauti na Annaajashi (King Negus of the ancient Ethiopia), alikuwa ni Mfalme Mkiristo lakini mpenda Haki na muadilifu, huyu ndiye aliyeunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuwapa hifadhi katika himaya yake wanafunzi wa mtume waliokimbia mateso na manyanyaso ya wapagani wa Makka. Tundu Lissu ni mkiristo mpenda haki, huyu ndiye anayetufaa na siyo yule ambaye hatupi nafasi za kutosha kwenye serikali yake halafu anatuhadaa kutujengea misikiti, lini sisi tumewahi kuwa na shida ya kujengewa msikiti na mtawala?. Sisi Shida yetu ni HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU!

Mwisho kabisa nitoe nasaha kwa Watanzania wenzangu
Hatua ya Sheikh Ponda ni hatua ya kizalendo sana, Si hatua ya Udini hata kidogo, Maana kama Ponda angekuwa mdini maana yake angemuunga mkono Hashim Rungwe au Lipumba ambao ni waislamu wenzie. Ponda kamuunga mkono Lissu ambaye yeye Lissu na Magufuli ni wa Imani moja na dhehebu moja ila tofauti yao kuu ni kuwa Lissu ni mtu wa Haki wakati Mgombea wa CCM si mtu wa haki hata kidogo (Ana double standard na ndimi mbili). Tuungane kumuweka Lissu madarakani ili atuondolee dhulma ya kutisha katika nchi!
Kwamba teuzi ni za upendeleo ?ni kweli Samia Suluhu (Makamu) ,Majaliwa Kasim(waziri Mkuu) ,Suleman Jafo(tamisemi) ,Mwinyi (ulinzi) hao wote ni Wakristo inauma sana yani tena ngazi za juu kabisa hata Jaji Mkuu wa Tanzania ni Mkristo hapa Lazima tutupe Lawama kwa Raisi John Magufuli maana walifungwa kwenye Utawala wake walitolewa Bara wakapelekwa Visiwani nakufungwa tunataka mapadre wetu waachiwe maana hata Raisi Mstaafu alikuwa Mkristo,mwaka huu tunatembea na Haki hatutaki Amani.
Mwnye akili anaelewa Libya haina Amani haki gani waliyonayo zaidi ya machafuko.

Mimi nitatembea na JPM
 
Lawama kwa Raisi John Magufuli maana walifungwa kwenye Utawala wake walitolewa Bara wakapelekwa Visiwani na kufungwa tunataka mapadre wetu waachiwe maana hata Raisi Mstaafu alikuwa Mkristo,mwaka huu tunatembea na Haki hatutaki Amani.
Mwenye akili anaelewa Libya haina Amani haki gani waliyonayo zaidi ya machafuko.

Mimi nitatembea na JPM

..Raisi Magufuli anaweza kuwaachia huru Mashekhe.

..ni kweli walifungwa wakati wa Raisi Jakaya Kikwete.

..lakini hiyo haimaanishi kwamba Raisi Magufuli hawezi kuwatoa kifungoni.

..kwa mfano, Raisi Magufuli aliwasamehe Babu Seya na Papii ambao walilawiti watoto na kufungwa na watangulizi wake.

..sasa kama Walawiti wanaweza kuachiwa, kuna ugumu gani kuwaachia Mashekhe?

..mwisho, Libya haina amani leo hii kwasababu wakati wa Gaddafi haikuwa na haki.

Kwa msingi huo, ni vizuri tukachagua utawala unaotenda haki, ili tuweze kujihakikishia amani huko mbeleni.
 
Chadema ina haki gani ?na haki ipi Walibya waliikosa nipe mifano hata miwili.
 
Haki isingekuwepo Amani ungekuwa nayo hata kuwa JF sasa hivi.

..Haki ingekuwepo Mashehe wasingeendelea kukaa mahabusu bila kufikishwa mahakamani.

..Haki ingekuwepo kungekuwa na uwanja sawa ktk shughuli za vyama vya siasa nchini.

..Haki ingekuwepo wagombea wa vyama mbadala wasingekuwa wanaenguliwa kihuni na wasimamizi makada wa ccm.

..Haki ingekuwepo wananchi wa kusini wasingenyang'anywa korosho zao kwa amri ya kidikteta ya Magufuli.

..Haki ingekuwepo wananchi tungekuwa na mamlaka zaidi ya kuamua kuhusu vipaumbele vyetu vya maendeleo.
 
Don't panic, no any value in your post even if you tried to express your self in English. Am pretty sure Sheikh Ponda will run you crazy, prior to the coming election.
Ndio shida zao hizi wakishindwa points wanatandika watu risasi 39.
 
Back
Top Bottom