Hili la Ukosefu wa Ajira tatizo lilianzia hapa kwenye D2, wazazi tuwaambie vijana ukweli, vyuo vya ovyo ovyo elimu ovyo!

Ufundi ni low skill labour. Je wewe unashona suruali ngapi kwa mwaka ili unishawishi niwe fundi hapa mtaani?
 
Kwani hao waliosoma zamani waliunda ndege au gari?
Utaniaminishaje kuwa walihitimu vizuri wakati hawaja achieve cha maana zaidi ya ku implement/ issue office documents tu.
Mashirika mengi yaliflisiwa na watu waliosoma zamani .
Waliosoma zamani were very incompetent people, they were less informed and non innovative. Fuc#k the old school idea!!!
 
Inasikitisha sana.Kutokana na hali inayoendelea hapa nchini Ninashauri kiongozi mkuu wa serikali ajiuzulu ili kupisha kiongozi mwingine mwenye uwezo zaidi
 
Kipindi nasoma , kwa mawazo haya isingekuwa ajabu , mwalimu wangu kusema tukupigie makofi , Eko kaka natamani ningekuona hata sura nikupongeze ila ndio hivyo tena , tupo kwenye andaki ya "where we dare to talk openly " .

Natamani elimu ingepita kwanza mtaani kuwajulisha wazazi kuwa kwenda chuo sio uhakika wa ajira tena , maana wazazi wakishaona watoto wamepewa hela ya kujikimu basi wengi wao wanafikiri bila shaka ajira ni lazima , kutwa kucha kuwananga vijana waliohitimu na wapo nyumbani tu .

Poleni sana ndugu zangu wahitimu, embu kubali uhalisia wa muda wa sasa ili muendane na mtaa .
 
D2 maake kwanza apa nichekee😂😂😂😂 wew unataka D ngapi kwa mfano Elimu ya Tz ni complex kuliko ata za nchi za nje
 
Mkuu hiyo sio sababu wala nini Acha raia wawe na elimu shida ni serikali sio Degree nyingi Hebu nenda nchi zilizoendelea KAZI zinatafuta watu licha yakuwa nawasomi wengi viwanda vipo vingi , uwekezaji ndo usiseme ajira zinatafuta watu. SASA Tanzania yetu imekalia siasa tuu kipindi kile chamagu Mpaka wawekezaji wanakimbia Kwa Ujinga na uonevu Kwa wawekazaji hizo ajira zitatoka wapi.

Kama unavyoona Nchi inavyopambana kuongeza miundo mbinu ya barabara, madaraja , kuongeza njia zengine mbadala za usafiri kupunguza foleni na shida ya usafiri kutatua hayo matatizo ndivyo serikali pia inatakiwa kuwekeza zaidi katika viwanda, Miradi na masharti ya kuwekeza yawe nafuu kukabiliana na tatizo la ajira na sio kuweka vikwazo watu wasiwe naelimu.
 
Huu uzi ni madini sana ajabu watu hawataki vitu vya msingi. System ya elimu yetu na mtaala kwa ujumla inasikitisha sana na kadri siku zinavyosonga ndivyo inavyozidi kudorora.

Waliomaliza form four ndiyo tunawachukua siku hizi kufanya kazi za ndani, ufahamu wake huwezi mtofautisha na darasa la saba! Baadhi ya Graduate wa siku hizi ndio hawa wanaandika "tyu badala ya tu" "xaxa badala ya sasa"!! Unaongea nae unaona hata form 4 wa zamani alikuwa smart kuliko yeye!

Tuna safari ndefu na ya kusikitisha.
 
Mifumo hii ya elimu zetu tusitegemee kuwa na job creators bali watembeza bahasha kila kukicha. Hawa wachina, wahindi huko kwao wana home industries nyingi sana na hizo zimeajiri wengi pamoja na kutengeneza vitu mbalimbali na kuuza mpaka nje ya mipaka yao huku sie tunayo Sido kila mkoa lakini iko hoi bin taaban. Hawa wachina na Kanji bhai nowdays wanakuja huku kwetu na technology yao wengine hawana kabisa wanaanzisha projects kisha wanawapa vibarua wenye degree kwa ujira wa utumwa. Inasikitisha sana,kuwa mtumwa kwenye nchi yako mwenyewe yenye wingi wa maziwa na asali.
 
Yawezekana hujui maana ya elimu. Elimu sio degree wala vyeti.
 
Yawezekana hujui maana ya elimu. Elimu sio degree wala vyeti.
Hatujafika huko na usilazimishe tufike huko elimu zetu hazizai matunda na hazimuathiri MTU Kwa kumjengea misingi imara na uwezo wa kureason wala shida sio vikwazo Ila nimfumo wa elimu lakini usiseme elimu inaenda kutengeneza shida ya ajira.
 
Pa
Hapa kweli wa afrika tumepigwa na kitu kizeetoo kwa head.

#MaendeleoHayanaCham
Palamagamba alisoma PhD ujerumani. Nadhani alisoma kwa Kiingereza huko ujerumani.

Kimsingi ufundishaji kwa maana ya transfer of knowledge iko kwa kiwango cha chini. Hata somo la Kiswahili linafundishwa kwa kiwango cha chini.
Lawama zisielekezwe kwenye lugha tu
 
Hapa kweli wa afrika tumepigwa na kitu kizeetoo kwa head.

#MaendeleoHayanaChama
Nilipokuwa Shule ya Msingi nilikuwa natafsiri maswali ya Kiswahili kwa Kilugha.

Sekondari nilitafsiri Kiingereza kwa Kiswahili ndipo nirudi kujibu kwa Kiingereza.

Hata sasahivi nikiambiwa andaa mpango kazi kwa kiingereza. nitaanza kuhangaika kutafsiri.

Huyo jamaa katupiga sana na kitu chenye tani nyingi sana kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…