Hili la Wabunge 50 kutoka Zanzibar yenye wapiga kura wasiozidi laki tano, wakati Temeke wapiga kura 1.5M Wabunge 6 limewaliza Watanzania

Hili la Wabunge 50 kutoka Zanzibar yenye wapiga kura wasiozidi laki tano, wakati Temeke wapiga kura 1.5M Wabunge 6 limewaliza Watanzania

Hapo ni kulilia ujinga.
Hapo wako sahihi. Kwa udogo wa nchi yao hilo jimbo lenye watu 7000 ni sawa tu na temeke yenye mil. Ukilinganisha ratio ya population ya zanzibara na bara na ukubwa wa eneo.
Wewe ni mjinga!
 
Zanzibar inatakiwa iongozwe na mwenyekiti wa mtaa tu hamna haja ya kuwa na Rais, mawaziri wala mbunge ukipiga filimbi nchi nzima wanakuskia
Wewe ni mbumbumbu katika masuala ya muungano bora ungekaa kimya kuficha umbumbumbu wako pole sana
 
Wakati Watanzania wanaendelea kula Dozi ya Ubongo( Brain Vitamins) kutoka kwa Wakili Nguli na Mpigania haki Mh Makamu Mwenyenyekiti wa Chadema kwenye ziara zake.

Mh Lissu ambaye yuko ziarani ktk harakati zake za Kuendesha Maandamano mikoa yote Tanzania na mikutano ya kisiaaa ametoa Takwimu zilizoacha midomo wazi watanzania.

Hizi ni Takwimu ambazo zilikuwa hazifahamiki kwa wengi.

Kwamba Zanzibar inachangia idadi ya Wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania takribani 80 wakati ina idadi ndogo ya wapiga kura na ukubwa wa majimbo mdogo sana.

Amesema kuna baadhi ya majimbo yanawapiga kura elfu 7 tu huku Temeke jimbo moja lina wapiga kura zaidi ya Laki nne.

Taarifa hizi zimewaliza watanzania wengi waliokuwa mkutanoni na wengi waliofikiwa na taarifa hizi kupitia mitandao ya kijamii na vyomvo vya habari.

Mh Lissu hoja yake ilikuwa kufafanua namna serikali inayotumia pesa nyingi za walipa kodi kunemeesha baadhi ya watu bila sababu za msingi badala ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Haichukui nafasi ya Mhasibu Mkuu wa Benki kutambua kuwa kimahesabu Kama Nchi tunakula Hasara.

Kwamba Nchi yenye malengo inawezaje kutumia pesa nyingi kiasi hiki ku secure vyeo na anasa wakati ni Nchi maskini inayotegemea mikopo kwa asilimia kubwa?
Mkuu CCM WOTE ni majizi
 
Ila tukiweka siasa pembeni ndugu zanguni Nyerere alituingiza chaka vibaya mno kuliko MO alivyoiingiza Simba chaka😕😕😕

Nyerere aliwahi kutamka kuwa yeye na wenzake walifanya makosa mengi. Akauliza kuwa wasifanye makosa kwani wao ni malaika? Muundo huu wa Muungano, kwa vyovyote ni baadhi ya hayo makosa.
 
Shida kubwa zaidi nionavyo mimi ni kutokuwa na muendelezo wa madai ya watanzania.

Hivi sasa malalamiko yahusuyo muungano yanatolewa zaidi na watanganyika. Nadhani ni kwa sababu raisi ni mzanzibari. Akimaliza uraisi wake akaja mtanganyika malalamiko yatapunguwa.

Haipaswi kuwa hivyo. Kama tunataka mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa nchi tudai bila kujali nani mtawala kwa wakati huo.
 
Suala ya Muungano ni mtambuka hivyo KATIBA inahitaji mabadiliko makubwa sana ili kuondokana na mapungufu yaliyopo na iweze kuzuia tamaa mbaya ya baadhi ya wanasiasa.
 
Watu 400000 mbunge 1 watu 7000 mbunge 1, huku ni kubembeleza au, eti kisa nchi. Hapa ndupo umuhimu wa katiba bora.
Na si hivyo Tu, anaye lipa ni Nani , na Kama ni bara na visiwani, je visiwandi wana changia shs ngapi katika hizo gharama
 
Fikiri sawa sawa. Wewe huoni kuna umuhimu wa marekrbisho? Mfano, koo mbili zimeungana, moja ina ng'ombe 1000 nyingine 10 sasa wakiuzwa ng'ombe 100 wagawane sawasawa? Ni lazima muundo wa muungano urekebishwe kuwe na serikali 3 kuondoa huu upuuzi, period!
Hata kwenye ubia wa biashara kila mtu anapata faida kutokana na alichowekeza
 
Inauma sana mtu kutoka visiwani anauza ardhi na kuwaondoa wamiliki asilia kisa pesa na mamlaka!
 
Back
Top Bottom