Hili la walimu kuchangishwa michango ya Mbio za Mwenge kwa lazima likomeshwe

Hofu na woga tuu ,Mwalimu wangu alinifundisha yupo Igunga Paul Msabila alipinga unyonyaji wa CWT amekamatwa amewekwa ndani Kwa agizo la Mkurugenzi siku 6 ,akatolewa lakini bado msimamo wake upo palepale akipinga CWT . Hamuwezi kuleta mabadiliko kama wengine kama ww ni waoga hata kuhoji
 
Sahihi kabisa
 
Walimu ni kundi la kuliombea,90%ya walimu uwezo wa kujikimu hauzidi mwezi mmoja kwa maana kuwa endapo mwalimu hatalipwa mshahara Kwa mwezi mmoja kuna probability kubwa akafa Kwa msongo wa mawazo au njaa, mishahara wamechukulia mikopo mpaka mwisho na wamekabidhi ATM card kwenye taasisi za fedha kama dhamana ya mikopo, na wanadaiwa kwenye maduka n.k,

CHAKUSHANGAZA Bado mwajiri analazimisha mchango wa mwenge,fedha hiyo inaenda kuchezewa siku ya mwenge Kwa Kuna pombe na vyakula siku ya mkesha WHILE aliyetoa mchango ameshindwa hata kuwanunulia watoto wake sukari. Huu ni uonezi mkubwa sana,jambo halipo kisheria lingekuwepo basi watumishi wangekatwa kwenye mishahara Yao,huu ni wizi wa mchana kweupe.
 
Acha kazi kwenye seriakali kajiunge na CHADEMA huko. Yaani umepanga na mwenye nyumba anapata msiba wewe unawezaje kuendelea na birth day party halafu uendelee kuwa mpangaji? Mnajitoa ufahamu wakati mwingine. Mtumishi wa serikali kweli ugomee shughuli ya serikali?
 
Kwahiyo mwenge ni msiba wa serikali?ww ni miongoni mwa watu waliolifikisha taifa hapa lilipo Kwa mawazo mfu kama hayo,Kila kitu kitu mnadifend Kwa hoja uchwara
 
Kwahiyo mwenge ni msiba wa serikali?ww ni miongoni mwa watu waliolifikisha taifa hapa lilipo Kwa mawazo mfu kama hayo,Kila kitu kitu mnadifend Kwa hoja uchwara
Sijui ulisoma wapi maana uelewa wako ni mdogo sana
 
Walimu watasema nn wakati waajiri wao wanashirikiana na majambazi kuwafilisi ndio mana walimu wanachelewa kupata maendeleo kamshahara kenyewe kadogo halafu akafiki hata mifukoni wajanja wajanja wanawaporaa very sad
Huwezi kusikia Waziri/RC/DC wamechangia mwenge hata mia wao huwa wanalipwa na hiyo michango
 
Tate mkuu
Nilifanya hayo yote nikiwa huko Halmshauri my 10 yrs nikiwa mtumishi nayajua na nimeptia mengi mkuu. Tusikutane jf watu wajifanye hapa kama ni new mesia nw huyu hajawahi kuyapitia
Kama umepitia hayo unayyosema umepitia... kuna shida gani mtu kusema hadharani kwamba kuna tatizo linaropaswa watu kulitazama...?
 
Hakuna watumishi wanaonewa kama waalimu.....na Wana Chama chao sijui kina msaada gani...... anyway acha wawanyooshe maana asilimia 90 wasimamizi wa chaguzi ni waalimu..... nadhani wanatapika vile vijisent wanavyopewa wakati wa chaguzi
 
Naomba anae fahamu faida ya mwenge kuzungushwa nchini anieleze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…