Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Tulizoea bidhaa kama ngozi ya ng'ombe ikitumika katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama vile mikanda, Mabegi nk. Nina mwezi mzima na zaidi naweka oda ya ngozi ya ng'ombe kwa ajili ya kumchemshia mbwa nakosa nashindwa kujua kwanini. Basi ikabidi nimuulize huyo muuza bucha kwanini zimekuwa adimu hivyo au soko la nje ya nchi limekuwa kubwa?!
Jibu alilonipa sikuamini kwani aliniambia kuwa, oda nyingi zinachukuliwa kwa ajili ya kwenda kutengenezea supu ya kuuza na wachache hubeba majumbani kwa matumizi ya nyama ya kula Wao. Wateja wengi wa supu hiyo ni wale wa hali ya chini, walevi wa pombe za bei rahisi na mataptap kutokana na kutoweza kumudu gharama za kununua nyama au supu ya nyingine tuzijuazo.
Wanachofanya ni kuchoma/kuunguza yale manyoa yote na baada ya hapo hubandika jikoni tayari kwa kuchemsha supu hiyo. Bado sijajua kama ulaji wa aina hiyo ya supu ya ngozi una madhara kiafya kwa walaji hao au ni sawa tu na mtu anaekula nyama?!
Supu hiyo imekuwa ikiuzwa kibakuli kwa Shilingi 500 na wengi wamedai maisha magumu ndo yanafanya wale ngozi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kununua nyama. Nimejionea mwenyewe hapa Kilimanjaro.