Tulizoea bidhaa kama ngozi ya ng'ombe ikitumika katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama vile mikanda, Mabegi nk.
Nna mwezi mzima na zaidi naweka oda ya ngozi ya ng'ombe kwa ajili ya kuchemshia mbwa nakosa nashindwa kujua kwanini.
Basi Ikabidi nimuulize huyo muuza bucha kwanini zimekuwa adimu hivyo au soko la Nje ya nchi limekuwa kubwa
Jibu alilonipa sikuamini kwani aliniambia ya Kuwa oda nyingi zinachukuliwa kwa ajili ya kwenda kutengenezea supu ya kuuza na wachache hubeba majumbani kwa matumizi ya nyama ya kula Wao.
Wateja wengi wa supu hiyo ni wale wa hali ya chini na walevi wa Pombe za bei rahisi na matatap kutokana na kutoweza kumudu gharama za kununua nyama au supu ya nyingine tuzijuazo
Wanachofanya ni kuchoma /kuunguza yale manyoa yote na baada ya hapo hubandika jikoni tayari kwa kuchemsha supu hiyo.
Bado sijajua kama ulaji wa aina hiyo ya supu ya ngozi una madhara kiafya kwa walaji hao au ni sawa tu. Na mtu anaekula nyama.
Supu hiyo imekuwa ikiuzwa kibakuli kwa. Sh 500.
Naahidi kuja na Picha na tukio hili nimejionea mwenyewe hapa Kilimanjaro