Hili ndilo kosa la wanasiasa wengi na vyama vya siasa na hasa nchi za africa. Ukosefu wa itikadi

Hili ndilo kosa la wanasiasa wengi na vyama vya siasa na hasa nchi za africa. Ukosefu wa itikadi

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
3,129
Reaction score
4,285
Kosa kubwa sana la vyama vyetu hivi ni ukosefu wa hoja au itikadi inayotofautisha baina ya chama kimoja na Kingine. Mirengo ya vyama haviko wazi sana mbele ya wananchi.

Nilifuatilia uchaguzi wa Marekani kwa karibu sana. Kiukweli ilikuwa ni rahisi sana kutofautisha Democrat ( Progressive policy)na Republican (conservative Policy)

Democrats wanataka mabadiliko ya kuruhusu masuala ya utoaji wa Mimba, wahamiaji kuingia marekani kwa Wingi, Dini ikae mbali na Serikali, Ushoga uruhusiwe na Jinsia ya mtu iwe uhuru wa mtu. Bideni akaanzisha passport yenye Jinsia ya tatu inayoitwa X. Yaani mtu ambaye siyo Mwanaume Wala siyo mwanamke. Hawa wako kwenye kundi la LGBTQ+.

Kwa upande wa Trump na Republican yake wako Kinyume na Kila kitu nilichotaja hapo. Wanapinga utoaji wa Mimba, anataka Dini ikubatiwe, amefuta Passport yenye Jinsia ya tatu, na sasa anawafukuza wahamiaji haramu wote.

Wakati wa kampeni ilikuwa rahisi kuunga mkono Chama ambacho unaipenda sera au itikadi yake.
Vyombo vya habari vilikuwa vinawauliza wamarekani kuhusu Vipaumbele vyao kwenye hizo itkikadi chache nilizotaja hapo juu. Hoja za au sera za Trump za kufukuza wahamiaji ilikuwa ya kwanza kwenye tafiti Karibu zote.
Na hii ilitokana na majanga mengi yaliyofanywa na wahamiaji haramu. Jambo la pili lililowavuta wamarekani wengi ilikuwa ni sera ya Trump kuhusu Kushusha gharama za maisha kupitia ushauru wa bidhaa kutoka nje ya ya Nchi. Kwa hiyo, kwenye agenda muhimu karibu 7 au 8 za wamarekani kwenye uchaguzi wa 2024 agenda tatu za Trump zilikuwa juu.

Kwa hiyo, ilikuwa rahisi kujua kuwa Trump atashinda kirahsi. Trump akawa Rais wa Pili Toka Marekani izaliwe kushinda urais baada ya kushindwa 2020.

Ukienda uingereza Kila mtu alijua Chama kitakachoshinda kabla ya kura na matokeo yakawa vile vile. EFF ya Malema pale Africa Kusini inajitofautisha kwa kupigania zaidi Uchumi na hasa ardhi. Iko tofauti kabisa na Vyama vingine.

Sasa turudi Tanzania. Ukiangalia vyama vyetu 19 ni ngumu sana kuviweka kwenye mirengo au itikadi ya kisiasa itakayovitofautisha Chama kimoja na Kingine. Ilani zetu zimejaa shule, maji, bara bara, Hospitali nk nk. Zaidi ya hapo tunapambania matukio yanayotokea na kupita. Hatujakaa sana kiitikadi. Matokeo yake tuna mlolongo wa VYAMA vingi ambavyo wananchi wameshindwa kuvitofautisha.

Maisha ni hatua, tunahitaji kuendelea kuboresha siasa zetu mbele ya Safari.
 
Back
Top Bottom