Hili ndio jengo la Machinjio linalodaiwa kugharimu shilingi milioni 200 huko Kigoma

Hii nchi msilaumu watawala wala nini laumini wananchi wenyewe hawajitambui, ukipata nafasi wewe piga pesa kaa pembeni
 
Nioneshe chama kitakachowaletea watz maendeleo ili tuipige chini ccm!

Ubora wa chama huonekana kikiingia madarakani. Kikishindwa huondolewa na wananchi kupitia sanduku la kura. Kingine huingia. It’s a continuous/dynamic process.

Bila mfumo makini wa demokrasia tutaendelea kutawaliwa na wahuni wasio na wasiwasi wa kuwajibishwa na wananchi.
 

Issue ni watu wanadai kipindi cha mama hela zinaliwa cha mwendazake hakuna hata mia iliyoliwa ndo watu wanakuja na hizi facts.
 
Hatuwezi kuonja sumu kwa kuiramba
 
Ila CCM ni hatari sana, yani miaka sitini na kitu ya huduma mbovu za afya, maji ya kuunga unga, umeme hovyo ila bado wana wafuasi wengi tu nchi nzima?
 
Sisi wabongo tupo nyuma sana kwenye usanifu wa majengo...tushakariri kila jengo ni lazima liwe limejengwa kwa matofali n.k
 
Binafsi nakubaliana na wewe kuwa ccm imeshindwa kuleta kile wananchi wangetamani kiletwe na kwa muda mfupi, lakini kuamini kuwa Chadema ni mbadala wa ccm au itafanya vizuri kuliko ccm huo ni ujuha uliopitiliza.
Sio lazima kuwe na chama bora kingine ndo maendeleo yawepo.bali dhumuni la vyama mbadala ni ili kuleta ushindani.ukipata nafasi fanya vizuri ili uendelee kuwepo ila ukiharibu unakaa pembeni anakaa mwingine.Siku kutakapokua na ushindani wamadaraka ndio siku tutakayoanza kuona uwajibikaji na maendeleo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 

Issue hapa ni whether hii habari ni ya kweli au ya kubumba. Kama mradi ni wa zamani nadhani hata habari yenyewe nayo ilipaswa kuwa ya zamani.
 
Nilishasema kuwa nchi hii inakuwa kikwelikweli,hata hizi bado wanadai hazitoshelezi kumaliza huo mjengo.kwakuwa watanzania tunakamsemo "hakuna shida"wakati maumivu unayapata haikusaidii,hivo Basi tufike sehemu tuseme Sasa Basi inatosha ili Hawa wanaolihujumu Taifa Hilo wafikishwe mbele ya sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…