Hili ni swali langu kwenu mnaosema Israel ni ya wapelestina, Acheni kujitia upofu mtazame uhalisia

Israel ni taifa limeasisiwa mwaka 1948 wala sio la kale kihivyo, mleta mada anazungumzia taifa la palestine na hapa ndipo msingi wa mzozo upo, hiyo israeli hata babu yangu ameitangulia zaidi ya miaka 40.
 
Hapa umetudanganya mkuu.
 
Nyie ambao mnaliwa na bwana yesu
Mkuu usitukane watu kwasababu wao watamtukana muumba wa mbingu na ardhi, jibu watu kwa hoja na ufafanuzi wakinaishe watu kwa hoja, ama matusi na kulipiza tusi kwa tusi wakati huyo unayemtaja ni mtume miongoni mwa mitume, huku ni kuikosea adabu dini ya kiislamu, sisi hatukulelewa kutukana watu bali kuwabainishia na wakitaka wafuate wakitaka waache.
 
Kelele za Free Palestine nyingi nizamlengo kidini.
Nikupe taarifa tu kama ni mvivu wa kusoma kuwa Wapalestina wakristo na waislamu ni asilimia hawakupishana sana.

Na wao ni wakristo orginal siyo ya kupitia Rome wala Ujerumani. Hanaan Ashrawi aliyekuwa mke wa Arafat ni mkristo wakati Arafat mwenyewe alikuwa muislamu.

Hiyo homa ya udini munajipaka nyinyi watetezi wa Israel musiotambuliwa
 

Your browser is not able to display this video.
 
Unataka kuniambia hao Waisrael walitoka utumwani 1940s' ?, miaka yote hiyo walikuwa wakiishi wapi? Usichanganye Israel iliyoandikaa kwenye hivyo vitabu vyenu na hii iliyoioundwa kimkakati
 
Kwa misingi hiyo Wahindu wakisema kwa mujibu wa vitabu vyao vya kidini mungu wao amewaambia Tanzania ni nchi yao ya ahadi watanzania wote kuanzia sasa hamna haki na nchi yenu wewe utakubali kuondoka kwenye hii ardhi na kumuachia Mhindu hii nchi?
Kwani wahindi ardhi yao ya asili ni Tanzania.

vitu vingine jiongeze tu mkuu
 
Kwa misingi hiyo Wahindu wakisema kwa mujibu wa vitabu vyao vya kidini mungu wao amewaambia Tanzania ni nchi yao ya ahadi watanzania wote kuanzia sasa hamna haki na nchi yenu wewe utakubali kuondoka kwenye hii ardhi na kumuachia Mhindu hii nchi?
Hao wahindu waliishi Tanzania kabla ya wakazi weusi wa sasa hivi?
 
Kwani wahindi ardhi yao ya asili ni Tanzania.

vitu vingine jiongeze tu mkuu
Mstari wa kwanza wa maandishi yako umeweka nukta (.)
Unashadadia au muktadha ulikuwa unataka kuuliza swali? Yaani; badala ya kutaka kuweka alama ya kiulizo (?) kwa bahati mbaya ukaweka alama ya nukta (.)

Liweke sawa hilo kisha turudi kwenye mada.
 
Hao wahindu waliishi Tanzania kabla ya wakazi weusi wa sasa hivi?
Labda twende kwenye mfano halisi kwa sababu naona logic unataka kuiweka kando.

Ushahidi wa kihistoria mamlaka ya zanzibar yana maeneo mpaka huku kwetu bara.

Unafahamu kuwa Kigamboni ni ya Zanzibar? Na haikuishia hapo, mpaka bandari ya bara Dar es Salaam ni ya wazanzibar. Upo tayari kuwapa eneo lao?

Wazanzibar wakidai hayo maeneo kwa kitumia huo ushahidi wa kihistoria upo tayari kuwapa hayo maeneo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…