Hili suala la Bongo Zozo kujipenyeza kila mahali hadi chumbani kwa baba limekaaje?

Hili suala la Bongo Zozo kujipenyeza kila mahali hadi chumbani kwa baba limekaaje?

Sio rahisi kufahamu malengo halisi ya mtu mpaka upate muda wa kuwa nae karibu.

Huyu jamaa anatuzuga tu hana jema lolote.
Wazungu wengi wanaokuja huku kwetu ni majasusi au utoa taarifa kusaidia majasusi.
 
Halafu sijui ni kwanini hawa raia wenye asili ya nje wanapenda sana kusema ni wahehe. Mfano Hans Poppe, Harbinder Seth Singh, huyu Bongo zozo etc.
Hans Pope wamechanganya damu ya Kihehe, yule Singasinga amezaliwa Uheheni, ila Bongo Zozo nadhani ana demu wa Kihehe
 
Na matokeo yake wanafwata mkia!uoga na ubinafsi, mimi ni mzaliwa na mkulia wa huku lingusenguse sio mgeni na always ninapenda facts

Sasa mbona huongei ukweli bali unawakilisha hisia zako tu?
 
Tanzania sio ya kipuuzi kiasi hiko, angekuwa ana madhara zamani tu asharudi kwao. Uimara wa idara ya usalama wa Taifa haitoshi kuilezea kwa masimulizi ya kwenye mitandao.

Rudia stori ya Mohamed Emwazi(Jihad John-mchinjaji wa Isis) aliyerudishwa kwao U.K baada ya kukamatwa JKNIA kushukiwa akiwa na nia ovu ya kwenda kujiunga Alshabab kupitia Tanzania.
 
Hahah hahah hahahah kama tu hawana majibu ya maswali mepesi tutawezaje kuwaamini kwenye mambo magumu?

Wewe kama nani. Ukiona umekaa na unapata muda wa kula na kwenda chooni kwa utulivu ujue Kuna wanaume na wanawake wa Taifa Hili wanafanya kazi. Tuendelee kuwashukuru. Shida ya mitandaoni kila mtu Kocha. Professor. Dr. Tajiri. Mwalimu. Nk.
 
Wivu tu.
Unadhani wewe una akili kuliko vyombo vya usalama?Au hapo ndio unajiona una akili sana kuhisi hisi tu?
Kwa taarifa yako mojawapo ya watu waliopo kitengo nyeti cha Usalama Wa nchi ni Kingai Na Mahita kama ulikuwa unafuatilia kesi ya Mbowe utakuwa umenielewa, kiufupi tupo naked .
 
Wivu tu.
Unadhani wewe una akili kuliko vyombo vya usalama?Au hapo ndio unajiona una akili sana kuhisi hisi tu?
Hayo ni maneno yako, na hofu yako tu. Hata hivyo huu mwezi mchanga bado.
Hii ndio picha ya leo ya mwezi, watu wengi wana hasira, wakali kupindukia.

Screenshot_20220227-154133_The Moon.jpg
 
Huyu jamaa huenda ni shushushu VIP , lakini sisi tunamchukulia poa huku tukijidanganya kuwa msemo usemao KIKULACHO KI NGUONI MWAKO umepitwa na wakati
View attachment 2129177
Ni kuikosea nchi heshima
Hata kama ameoa amezidi khe
Huwa najiuliza kwani Hana shughuli za kufanya zaidi ya kupiga kelele
Kumbukeni huyo ni South African wale wanaitwa makaburu
Apunguze kelele mtu mzima ov....
 
Tanzania suala la usalama halitiliwi maanani kabisa. Mfano, kuna mzungu mmoja anaitwa Gerret Rene, huyu jamaa kwa mwaka anaingia Tz kama mara mbili au tatu. Huingia Tz kwa kigezo cha kufanya miradi ya afya, hupewa vibali bila shida. Miradi yake anaifanyia Rufiji, Kibiti, Zanzibar na Amani huko Muheza. Sidhani kama serikali huwa wanam track ili kuona kama kweli anafanya hiyo miradi ya afya. Kwani akifika huko hufanya mambo mengine kabisa, wajaribu kumfatilia watabaini.
Huyu jamaa ni Tapeli tu...hapa Rufiji hakuna mradi aliofanya, ana raise hela kwao huko then anajifanya kuja kutekeleza miradi huku ....
 
Huyu jamaa ni Tapeli tu...hapa Rufiji hakuna mradi aliofanya, ana raise hela kwao huko then anajifanya kuja kutekeleza miradi huku ....
Matapeli wapo wengi sana na hao ndio wanaitwa wawekezaji.

Wamejaa kwenye mahoteli ya kitalii wanatumbua tu hela walizofanyia utapeli wao.
 
Hivi msela kama mimi nianze tu kuwa shabiki wa Stars,kesho naweza kukutanishwa na Rais? au kwa sababu huyu ni mzungu?
Utofauti wake ndio unafanya azingatiwe kuliko wewe.

Kwa kuwa yuko tofauti watu watamfuatilia hivyo anakuwa katutangaza, sasa wewe ukivaa uzalendo haishtui sababu ni kawaida mwenye nchi kuwa mzalendo
 
Back
Top Bottom