Hili suala la posho ya mbunge ya siku moja kuzidi mshahara wa mwezi wa Mwalimu, HALIKUBALIKI!

Ila Walimu nao wajitambue, si ndio wao wanachangia fedha ya form [emoji28][emoji28] ila hii nchi ina watu fulani hivi ambao mindset zao zimeyumba kidogo
Njaa hudhoofisha uwezo wa kufikiri
 
Exactly
 
Magufuri ndiye alieharibu utaratibu wa nyoneza mishahara kwa watumishi wa umma.
Mwacheni apumzike.
Hata hivyo hawezi kutusaidia kwa lolote kwa sasa.
Hawezi kujitetea.
Tuhangaike na waliopo
 
Labda ni kwa sababu hujajua posho wanazolipana BOT na TANAPA, labda utaona Wabunge wana afadhali. Hii nchi inajua kutoa posho.

Ova
 
Twende tukagombee ubunge mkuu. Aliye juu mfuate.

Hatma ya mwalimu ipo mkononi mwa serikali. Ikiamua itaboresha maslahi yao. Ukiona unaongea ila serikali haikusikii ujue huna la kuitisha.
 
Sheria wanatunga wao, posho wanajipitishia wao, afu mtu analipwa posho hata bungeni hajafika, akaunti inasoma tu mtu yupo lodge anapiga Tako tatu
Si Bora awe anapiga Tako tatu, wengine naskia wanapelekewa wao wenyewe Moto,just imagine,anapelekewa moto huku balance inasoma
 
Wabunge wapo 393 jumla, walimu idadi yao inacheza kwenye million kasoro. Haiwezekani kulipwa sawa.
 
Mbunge akiwa bungeni ndipo huweza kutimiza majukumu yake ya kazi. Bunge ni sehemu yake ya kazi kama ilivyo kwa mwalimu akiwa shuleni.

Ni vyema serikali ikaangalia kutotoa posho kwa mfanyakazi wa umma anapotekeleza majukumu yake katika eneo lake la kazi. Pengine posho zingetolewa kwa kuangalia mazingira hatarishi ya kazi ya mtumishi.

Wote wabunge na walimu pasipo kujali ukubwa wa posho, hawatekelezi majukumu yao ya kazi katika mazingira hatarishi. Kwa hiyo hawapaswi kulipwa posho yoyote ile. Ni Tanzania tu kila kitu kinawezekana kwa mwanasiasa aliyepo madarakani hata kama ni cha kipuuzi namna gani!
 
Sitaki kutetea sana, Ila twende kwenye majukumu, mbunge anawakilisha jimbo la uchaguzi na kutunga sheria za nchi, mwalimu anafundisha masomo mawili au matatu
 
Mkuu huo ni mpango mkakati wa serikali wa kuwanunua Wabunge ili waunge mkono hoja zake.Hii ilikuwa wazi sana katika swala la DP World.Kimsingi wananchi tuna hali mbaya sana, tuliyedhani ni mtetezi wetu katugeuka na sasa ana collude na our enemy kutumaliza.Inatisha sana.
 
Yaani nchi hii ina maajabu sana.
Wanaofanya kazi sana, ndo wanalipwa kidogo ilhali wanaofanya kazi ndogo (kama wabunge Walio wengi ambao kazi yao ni kupiga makofi tu, kusinzia na kushabikia mambo ya hovyo) wanalipwa maradufu!
Walimu pia wanafanya kazi kidogo sana ukilinganisha na wafagia barabara, wachanganya zege, wapishi wa chakula cha wanafunzi, wakulima, n.k

Mara zote equation imekaa hivyo, ukiona unatumia nguvu sana na jasho jingi linakutoka wakati wa kazi ujue wewe ni mlalahoi na malipo yako yatakuwa kidogo
 
Na nasikia kuna wanaotaka idadi iongezwe kila jimbo liwe na wabumge wawili wa kike na kiume ikiwa na maana bunge litakuwa na wabunge kama 800. Tz kweli channel ya vichekesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…