Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ni dharau kubwa.Don't go this far.Msisahau kwamba kila kipindi anachofundisha Mwalimu kuna maandalizi yanayohitajika,haingii kwenye kipindi kichwa kichwa tu.Walimu pia wanafanya kazi kidogo sana ukilinganisha na wafagia barabara, wachanganya zege, wapishi wa chakula cha wanafunzi, wakulima, n.k
Mara zote equation imekaa hivyo, ukiona unatumia nguvu sana na jasho jingi linakutoka wakati wa kazi ujue wewe ni mlalahoi na malipo yako yatakuwa kidogo
Walimu wa mwaka gani au wa nchi gani unaongelea? Hawa hawa tunaoshinda nao kwenye vibanda-umiza , kwenye mnazi na gongo, kwenye betting, n.k?.Msisahau kwamba kila kipindi anachofundisha Mwalimu kuna maandalizi yanayohitajika,haingii kwenye kipindi kichwa kichwa tu.
Natamani tufike mahali ubunge uwe swala la wito,sio kazi,hii itapunguza au kuondoa kabisa huu utitiri wa mchwa unaotafuna rasilimali za Watanzania katika ubunge.Mbunge awe na kazi yake,ikitokea ni kipindi cha Bunge apewe kiasi tu cha posho kumuwezesha kuishi.Ilivyo sasa there are thousands of question marks.Salaam wapenzi wana JF.
Leo nimeamua kuwasilisha hii kero ya ukosefu wa usawa linapokuja suala la kufaidi keki ya Taifa.
Yaani haiingii akilini kabisa kwa mbunge kulipwa pesa ya posho ya siku moja ambayo ni kubwa zaidi kuliko mshahara wa Mwalimu wa mwezi mzima.
Siyo sawa kabisa.
Ahsanteni.
Huyo sio mwalimu ninayemjua,ila nawewe badili tabia.Walimu wa mwaka gani au wa nchi gani unaongelea? Hawa hawa tunaoshinda nao kwenye vibanda-umiza , kwenye mnazi na gongo, kwenye betting, n.k?
Sasa hivi tu ukihoji tija yao hao wabunge, mambo mengi utaambiwa sio katika jukumu la mbunge japokuwa hayo hayo yasiyo katika majukumu yao ndio huyatumia kuombea kura. Sasa sijui wakiongezwa wanaenda kufanya kazi ipi ambayo wanaona inahitaji ongezeko la wabunge zaidi?Na nasikia kuna wanaotaka idadi iongezwe kila jimbo liwe na wabumge wawili wa kike na kiume ikiwa na maana bunge litakuwa na wabunge kama 800. Tz kweli channel ya vichekesho
Kwahiyo mkuu kwa sababu kupata ubunge ni ngumu au ni gharama hivyo walipa kodi ndio tunawajibika kufidia hizo gharama?Katafute ubunge uone kama rahisi
Waondoe hizo posho na mishahara mikubwa, aone kama ubunge utakuwa mgumu kama ilivyo sasa. Kwanza faida tutakayoupata kwa kuondoa miposho na mishahara mikubwa ni kuwa tutapata wabunge wazalendo wenye mapenzi na nchi yao toka ndani kuliko ilivyo sasa..Kwahiyo mkuu kwa sababu kupata ubunge ni ngumu au ni gharama hivyo walipa kodi ndio tunawajibika kufidia hizo gharama?
Mzee Kinana anasema “wabunge wetu wanalipwa pesa kidogo sana”
MISHAHARA YA WABUNGE NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA HALI YA JUU KABISA TANZANIA.
Suala la Mishahara ya Wabunge analoliongea @HecheJohn linaumiza roho sana.
Mwalimu wa Tanzania mwenye TGTS D1 mwenye mshahara take home 531,000 kwa mwezi, akifanya kazi kwa miaka 38 atalipwa shilingi 242,136,000 (milioni 242).
MBUNGE wa Tanzania kwa mwaka mmoja analipwa shilingi 240,300,000 (milioni 240 bila posho za kamati).
Yani mwalimu wa Tanzania mwenye degree analazimika kufanya kazi kwa miaka 38 ili aweze kupata malipo anayopewa mbunge wake (ANAYETAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU) kwa mwaka mmoja tu. Ndio uzalendo huu?
YANI IPO HIVI,
Mbunge anayelala tu bungeni analipwa;
Jumla kwa mwaka mmoja ni sh. 240,300,000 (milioni 240, hii haihusishi posho za kamati za kudumu).
- Posho za vikao kwa mwaka ni sh. 42,300,000 (milioni 42.3)
- Mshahara na marupurupu kila mwezi 16,500,000 × miezi 12 = 198,000,000 (milioni 198).
Kwa miaka mitano, mbunge wa Tanzania analipwa 1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.
TUCHANGANUE MALIPO YA MBUNGE VIZURI
Sitting Allowance - 220,000
Per Diem - 250,000
Jumla kila siku mbunge analipwa 470,000/= (haijalishi ameongea au lah).
Mshahara na marupurupu kwa mwezi - 16,500,000/=
Mshahara wa mbunge kwa mwaka mmoja ni shilingi 198,000,000 (milioni 198).
Mshahara wa mbunge kwa miaka mitano ni shilingi 990,000,000 (milioni 990).
Bado kila baada ya miaka mitano huyu mbunge analipwa kiinua mgongo milioni Mia mbili (200,000,000).
Vikao vya Bunge
Kikao cha Januari 31 - Feb 10 = siku 11
Kikao cha bajeti April 4 - June 30 = siku za vikao 59
Mkutano wa tisa wa bunge mwaka 2022 Nov 1-11 = siku 10
Mkutano wa nane kuanzia Sept 13-23 = siku 10
Jumla ya siku za vikao vya bunge ni siku 90.
Siku 90 za vikao × 470,000 = 42,300,000
42,300,000 za vikao × miaka 5 = 211,500,000
JUMLA KWA MIAKA MITANO
1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.
TUANGALIE MSHAHARA WA MWALIMU KWA MIAKA MITANO
Mwl. mwenye TGTS D1 mshahara wake basic ni shilingi 771,000 kwa mwezi, ukitoa makato, take home ya mwalimu huyu no shilingi 531,000.
Mshahara wa huyu mwalimu kwa mwaka 531,000 × miezi 12 = 6,372,000 mara miaka mitano = 31,860,000 (huu ni mshahara wa Mia I miwili wa mbunge).
Kwa miaka 38 mwalimu analipwa 6,372,000 * 38 = 242,136,000 (sawa na mshahara wa mwaka mmoja wa mbunge).
Huyu mwalimu akidai nyongeza ya mshahara anaambiwa "KUWA MZALENDO." Kama sio wizi huu ni nini????
Wakati mbunge wa Tanzania anaogelea kwenye bwawa la utajiri wa kodi za walala hoi, mtoto wa mtanzania maskini anashindwa kujengewa hata choo cha tundu kwenye shule yake; hata dawati la shilingi elfu 50 tu limeshindikana; hata kitabu cha elfu kumi tu imeshindikana.
IFIKE MAHALI TUACHE HUU UFALA WA
KUENDELEA KUFUMBIA MACHO UDHALIMU WAKATI TUNAOUMIA NI SISI NA WATOTO WETU. MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA PALE WATU WA CHINI TUTAKAPOSIMAMA KUPINGA UDHALIMU.
By mama naa
Hiyo ni hongo mkuu,it is obvious and this happens only in Tanzania.Lakini si unaona,it is working for the government and CCM,they literally have an empty cheque from MPs.Salaam wapenzi wana JF.
Leo nimeamua kuwasilisha hii kero ya ukosefu wa usawa linapokuja suala la kufaidi keki ya Taifa.
Yaani haiingii akilini kabisa kwa mbunge kulipwa pesa ya posho ya siku moja ambayo ni kubwa zaidi kuliko mshahara wa Mwalimu wa mwezi mzima.
Siyo sawa kabisa.
Ahsanteni.
Unao watetea wenyewe HAWAJITAMBUI.....ndo kwanza wanamlisha MalkiaSalaam wapenzi wana JF.
Leo nimeamua kuwasilisha hii kero ya ukosefu wa usawa linapokuja suala la kufaidi keki ya Taifa.
Yaani haiingii akilini kabisa kwa mbunge kulipwa pesa ya posho ya siku moja ambayo ni kubwa zaidi kuliko mshahara wa Mwalimu wa mwezi mzima.
Siyo sawa kabisa.
Ahsanteni.
Hawana mishahara ni kweli,lakini posho wanazopata za vikao na assignments mbali mbali za chama ni zaidi ya mishahara mkuu.CCM inatambua kwamba madiwani ndio mtaji wao mkubwa,so lazima ifanye kila inaloweza kuwafurahisha.Madiwani hawana mishahara.
Wabunge nao hawatakiwi kuwa nayo.
walimu Kila mtu anawajua na pilika zao anaziona siyo darauKwa hiyo walimu ndio walishakuwa kipimo cha kila kitu hapa nchini. Muwe na heshima na acheni dharau kwa walimu.