Hili suala la posho ya mbunge ya siku moja kuzidi mshahara wa mwezi wa Mwalimu, HALIKUBALIKI!

Hii ni dharau kubwa.Don't go this far.Msisahau kwamba kila kipindi anachofundisha Mwalimu kuna maandalizi yanayohitajika,haingii kwenye kipindi kichwa kichwa tu.
 
.Msisahau kwamba kila kipindi anachofundisha Mwalimu kuna maandalizi yanayohitajika,haingii kwenye kipindi kichwa kichwa tu.
Walimu wa mwaka gani au wa nchi gani unaongelea? Hawa hawa tunaoshinda nao kwenye vibanda-umiza , kwenye mnazi na gongo, kwenye betting, n.k?
 
Natamani tufike mahali ubunge uwe swala la wito,sio kazi,hii itapunguza au kuondoa kabisa huu utitiri wa mchwa unaotafuna rasilimali za Watanzania katika ubunge.Mbunge awe na kazi yake,ikitokea ni kipindi cha Bunge apewe kiasi tu cha posho kumuwezesha kuishi.Ilivyo sasa there are thousands of question marks.
 
Ajabu haya mambo tunaongea sana humu ila hatujawahi hata mara moja japo kumbananisha mbunge mmoja tu atoe ufafanuzi kwa nini walipwe malipo makubwa kiasi hicho? Aeleze ni ugumu gani wa kazi yao wenye kufanya wastahili kulipwa malipo ya kiasi hicho? Wanasiasa wetu wapo kimya katika hili si wa chama tawala wala upinzani.
 
Na nasikia kuna wanaotaka idadi iongezwe kila jimbo liwe na wabumge wawili wa kike na kiume ikiwa na maana bunge litakuwa na wabunge kama 800. Tz kweli channel ya vichekesho
Sasa hivi tu ukihoji tija yao hao wabunge, mambo mengi utaambiwa sio katika jukumu la mbunge japokuwa hayo hayo yasiyo katika majukumu yao ndio huyatumia kuombea kura. Sasa sijui wakiongezwa wanaenda kufanya kazi ipi ambayo wanaona inahitaji ongezeko la wabunge zaidi?

Binafsi mie hata sielewi hata hawa wabunge wa upinzani huwa tunatumia vigezo vipi kuwachagua au sijui ndio kwa wao kuwa wapinzani ndio kigezo?
 
Kwahiyo mkuu kwa sababu kupata ubunge ni ngumu au ni gharama hivyo walipa kodi ndio tunawajibika kufidia hizo gharama?
Waondoe hizo posho na mishahara mikubwa, aone kama ubunge utakuwa mgumu kama ilivyo sasa. Kwanza faida tutakayoupata kwa kuondoa miposho na mishahara mikubwa ni kuwa tutapata wabunge wazalendo wenye mapenzi na nchi yao toka ndani kuliko ilivyo sasa..
 
Madiwani hawana mishahara.
Wabunge nao hawatakiwi kuwa nayo.
 

Hii sio nchi salama kwa wananchi 😅🙌🙌
 
Hiyo ni hongo mkuu,it is obvious and this happens only in Tanzania.Lakini si unaona,it is working for the government and CCM,they literally have an empty cheque from MPs.
 
Unao watetea wenyewe HAWAJITAMBUI.....ndo kwanza wanamlisha Malkia
 
Madiwani hawana mishahara.
Wabunge nao hawatakiwi kuwa nayo.
Hawana mishahara ni kweli,lakini posho wanazopata za vikao na assignments mbali mbali za chama ni zaidi ya mishahara mkuu.CCM inatambua kwamba madiwani ndio mtaji wao mkubwa,so lazima ifanye kila inaloweza kuwafurahisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…