Hili suala la wastaafu kupeana Mahekalu, Mwalimu alisema ipo siku Watanzania watalidai Azimio la Arusha

Watz tuna akili na roho za kimaskini sana! Wivu umetujaa! Ndiyo maana kila tajiri tunamwita fisadi! Itachukua muda sana Tz kuendelea kwa aina ya wananchi tulionao
 
Nikikumbuka pale mjengoni walivyojipanga balaa, kikwete mkewe bungeni, mwanaye riziwani bungeni, mkwe na mwana wa bi mkubwa mjengoni.duh sijui sisi masikini tutaishia wapi.Genge la watawala wameteka uongozi wa nchi
 
Zawadi zote mbili walizopewa wastaafu ilikuwa wapewe na Hayati JPM kwa mujibu wa sheria. Mama Samia imebidi awape kwani ndio rais kwa sasa. Huku kulialia mitandaoni hakuna msaada wowote.

Huyo Mwalimu Nyerere miaka ya mwishoni alizidiwa nguvu na matakwa ya ubepari, umaskini ulikuwa mwingi na hakuweza kuwa na kipya chenye kuweza kutusaidia. Akaishia kuliongelea azimio akiwa amestaafu pale Kilimanjaro Hotel mwaka 1995.

Duniani siku zote wenye nguvu ni wenye pesa, tunawaita mabeberu tukiwa na hasira na marafiki wa maendeleo tukiwa tunataka kuomba watupe pesa.

Ushawishi wa pesa ni mkubwa na una nguvu kuliko vipengele vya azimio la Arusha.

Hawa marais wanafanya kazi nzito na ngumu, ni rahisi sana kukosoa matokeo ya kazi zao lakini sio rahisi kuvaa viatu vyao na kuja na maamuzi bora na yenye manufaa ikiwa mlalamikaji atakabidhiwa ofisi ya urais hata kwa siku moja tu.
 
Nikikumbuka pale mjengoni walivyojipanga balaa, kikwete mkewe bungeni, mwanaye riziwani bungeni, mkwe na mwana wa bi mkubwa mjengoni.duh sijui sisi masikini tutaishia wapi.Genge la watawala wameteka uongozi wa nchi
Mbunge wa Lindi vijijini , kumbe anaishi Masaki.stupidity yetu
 
Hivi jambo hili sidhani linatoka kwa Rais ni wale wapambe wanaojipendekeza kwa viongozi, Ati rais apewe nyumba Mbona hawasemi hiyo nyumba inagharimu kiasi gani. Hivi ni sawa kweli? Kama ni hivyo viongozi wengine wakipewa zawadi ya nyumba na mashirika yao, wataitwa wahujumu uchumi?
Marupurupu ya rais ni mengi sana baada ya kustaafu
.1. Analipwa mshahata wake wote mpaka atakapokufa
2. Anakuwa na ulinzi na watumishi wa kusaidia hapo nyumbani mpaka atakapokufa, serikali inalipa vyote
3. Je matibabu analipa?
4. Hakuna rais hana (ma)jumba lake labda alikuwa Nyerere.
5.Hakuna rais ambaye anaondoka madarakani bila kuwa na miradi tena mikubwa
Haya yote na mengineyo hayatoshi?
Huwa wanaotoa mawazo kama hayo huwa wanafikiri nini hasa: ni ili wapendwe zaidi au.....
Na bunge ni vigezo gani waliona jikubalike, ni kuogopa kusema ukweli?

Wananchi wanapatana vipensheni vyao kwa shida wengine wanapewa mahekalu

Hilo gari basi wakumbukwe pia walioandika vitabu huko nyuma
 
Watz tuna akili na roho za kimaskini sana! Wivu umetujaa! Ndiyo maana kila tajiri tunamwita fisadi! Itachukua muda sana Tz kuendelea kwa aina ya wananchi tulionao
Tofautisha kati ya wanasiasa mafisadi na matajiri .

Mimi na wewe tunawezaje kumuita Bakheresa fisadi
 
wakuu acheni cheap politics, kafanye kazi familia yako istarehe kukaa kulalamikia benzi la watu ni matumizi mabaya ya vidole..
 
Tazama car park yake Butiama hapo
 
Kutumia pesa za watu wanaoitwa wanyonge kumnunulia mtu anayeishi kwa starehe benzi ndio matumizi mabaya ya vidole.

Wangetumia pesa zao kufanya hayo hakuna mtu angelalamika.
wakuu acheni cheap politics, kafanye kazi familia yako istarehe kukaa kulalamikia benzi la watu ni matumizi mabaya ya vidole..
 
Sawa ni ya kawaida sana..swali ni je alijenga kwa pesa yake au kwa kodi za Watanzania?
Alijengewa na JKT kama zawadi.

Nadhani kazibya JKT unaijua ni Ujenzi.

Vile vile Rais akistaafu huwa kuna zawadi nyingi tu huwa zinatolewa, hata wananchi wanaopenda hutoa zawadi za ng'ombe kwa hiari yao.
 
Basi huenda hata hawa wanopewa mahekalu ni zawadi!
 
Basi huenda hata hawa wanopewa mahekalu ni zawadi!
Kwao siyo zawadi. Hao walijitungia sheria, kwahiyo ni lazima kwa mujibu wa sheria haijalishi nchi iko katika hali gani kiuchumi au watu wengine wanaisoma namba kwa kiwango gani.
 
Kwao siyo zawadi. Hao walijitungia sheria, kwahiyo ni lazima kwa mujibu wa sheria haijalishi nchi iko katika hali gani kiuchumi au watu wengine wanaisoma namba kwa kiwango gani.
Sheria hii ilikuwepo kabla sema Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawakuitekeleza ila alipokuja Hayati Magufuli ndio akaanza kuitekeleza kwa kumjengea Mkapa, Mwinyi na Kikwete! nae pia atajengewa na Samia
 
Unamaanisha ilitungwa enzi za Nyerere ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…