Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
Watz tuna akili na roho za kimaskini sana! Wivu umetujaa! Ndiyo maana kila tajiri tunamwita fisadi! Itachukua muda sana Tz kuendelea kwa aina ya wananchi tulionao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikikumbuka pale mjengoni walivyojipanga balaa, kikwete mkewe bungeni, mwanaye riziwani bungeni, mkwe na mwana wa bi mkubwa mjengoni.duh sijui sisi masikini tutaishia wapi.Genge la watawala wameteka uongozi wa nchiHii thread natamani viongozi wetu na wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama wakiwemo na maaskar wetu wote waje wapitie hapa kuna kitu watajifunza maana wametufanya kama watumwa kweny nchi yetu wanasahau kabisaa kama sisi ndo wenye nchi yetu na ndo tuko wengi wao niwachane mno sisi raia ndo wengi kuliko wao kwa iyo wawe makini kuna siku hayo majeshi yao, vifaru,na bunduki hazitafanya kazi kuwalinda wala kuwaokoa ikiwa wenye nchi tukiamua kwa umoja wetu.. maana wamekosa hata huruma na utu kwa wananchi bila kujali umaskini tulionao,
fikiria ni wizi kiasi gani na kujirimbikizia mali wanafanya na wengi wao hawafanywi chochote hata makamani hawapelekwi zaidi ya kulindana na kumahishana na kubadilishana vituo vya kazi mfano kama ameharibu kigoma anapelekwa singida au mwanza nk na maisha yanendelea
kuna viongozi wazazi wao wote baba na mama walikuwa viongozi tena wakubwa nchi hii wao pia ni viongozi na wnafabya chini juu na watoto wao pia wawe viongozi nao pia wanafanya kila liwezekalo na wanao pia watakuwa Viongozi sasa unaziuliza hii kamba ya kuwekana, kuteuana wao kwa wao sisi wengine ambao hatuna ndugu walioko juu tunakosa ajira na kazi kisa hatuna wa kutupendelea wala kutusaidia
Kweli kabisa wabongo tunatabia ya kusahau haraka sana. Huyu mama alitudanganya eti Magufuli mzima kumbe amekufa. Tuelezeni mmemuua kwa nini????Wanafanya wanalotaka muda wowote kwakuwa wananchi wapumbavu na wengine ni wajinga.
Over
Mbunge wa Lindi vijijini , kumbe anaishi Masaki.stupidity yetuNikikumbuka pale mjengoni walivyojipanga balaa, kikwete mkewe bungeni, mwanaye riziwani bungeni, mkwe na mwana wa bi mkubwa mjengoni.duh sijui sisi masikini tutaishia wapi.Genge la watawala wameteka uongozi wa nchi
Mimi siekewi, miaka 15 ya Samia, JPM Rest In Peace. I propose Zanzibar should be the capital, forget Dodoma, who lives there, they seem to be in DSM everydayNpo gizani
Hivi kati ya mbongo na kuku nani mwepesi wa kusahau zaidi?Kweli kabisa wabongo tunatabia ya kusahau haraka sana. Huyu mama alitudanganya eti Magufuli mzima kumbe amekufa. Tuelezeni mmemuua kwa nini????
Hivi jambo hili sidhani linatoka kwa Rais ni wale wapambe wanaojipendekeza kwa viongozi, Ati rais apewe nyumba Mbona hawasemi hiyo nyumba inagharimu kiasi gani. Hivi ni sawa kweli? Kama ni hivyo viongozi wengine wakipewa zawadi ya nyumba na mashirika yao, wataitwa wahujumu uchumi?Katika kizungumkuti hiki kinachoendelea leo, Wakubwa wanapeana Mahekalu na Mabenzi wakati wanananchi mamilioni kwa mamilioni wanatopea kwenye lindi la umasikini, Imenikumbusha kauli ya mwalimu Nyerere kuwa ipo siku wananchi Watasimama na kulidai tena Azimio la Arusha!
Binafsi ninajua kuwa azimio kama kazi yoyote ya mwanadamu halikuwa perfect lakini lilikuwa na misingi mizuri sana ya kung'oa unyonyaji haswa wa tabaka linalotawala!
Azimio lilikuwa kali mno kwa viongozi wa kisiasa, liliwabana kwelikweli, liliweka masharti magumu kwa wanasiasa kiasi kwamba walikuwa hawapumui. There is no way ungekuwa kiongozi wa kisiasa enzi za azimio kisha ukapeleka hoja za kujijengea Mahekalu na kupeana Benzi ukasurvive tena kisiasa.
Miongoni mwa mambo mazuri ya Azimio la Arusha ilikuwa ni Maadili ya viongozi. Ndani ya Azimio waliweka kanuni kuwa ni Marufuku kwa kiongozi kuwa hata na nyumba ya kupangisha! Na likaenda mbali kumdefine kiongozi ni nani, likasema kiongozi ni mtu yeyote mwenye wadhifa serikalini na chama, na Azimio likasema kuwa Kiongozi maana yake ni mtu na mkewe!, Kwa hiyo unaona wazi kuwa mtu alipigwa pini kujitajirisha kwa kujigicha kupitia identity ya mke/mumewe.
Hivyo ndivyo Jinsi Azimio lilivyokuwa serious, halikutaka kabisa tabia hizi za kuchomeka mirija na kunyonya wananchi kwa kisingizio cha "alikuwa rais, anastahilo ajengewe"
Pia azimio lilitaka mtu ajitegemee, Kama ni mfanyakazi, basi jenga nyumba kwa jasho na kipato chako au pensheni yako!
Ndiyo maana Mwalimu kakaa madarakani lakini hakuwahi kujitungia sheria akistaafu ajengewe nyumba, Hii maana yake ni kuwa aliamini suala la kujenga nyumba ya yeye kuishi ni kwa jasho lake, siyo kungoja ustaafu halafu Jasho na kodi ya wananchi ikujengee nyumba wakati pensheni unapata na unalipwa pesa kila mwezi zinazolingana na asilimia 80 ya mshahara wa raisi aliyeko madarakani! —Kwa nini usijenge mwenyewe kama unahitaji mijumba mingine hata kama unayo mijumba kedekede tayari!
Kwa hiyo ndugu zangu, huu ni kuda muafaka wa kukataa unyonyaji wa hii ruling class, kila kukicha wanafanya mambo ya kuwafanya waendelee kutunyonya huku wakitupiga kiswahili tuvumilie.
1. Wanapeana Mabenzi na Mahekalu.
2. Wamatunga sheria za kupeana Kinga wasishtakiwe kwa makosa wanayofanya madarakani.
3. Bungeni na kwenye baraza la wawakilishi wameweka watoto, wake na ndugu zao
Halafu sasa cha ajabu hawa watu walikuwepo enzi zile za azimio la arusha, Na mwalimu Nyerere masikini aliwaamini kuwa ni wenzie katika kuamini katika misingi ya kukataa dhuluma na unyonyaji katika nchi, kumbe walikuwa na lao moyoni, walikuwa wanamlia timing tu.
Tukatae mambo ya ajabuajabu haya ya watu kutuchukulia for granted!
Solution ya haya mambo ni katiba mpya, tena ya Warioba. Hii ni rasimu iliyoweka maadili ya viongozi ndani yake ili kujaribu kuondoa unyonyaji kama huu. Na hii ilitokana na wananchi kukerwa sana na mambo ya ufisadi.
Tuendeleeni kudai katiba mpya, hii lugha nzurinzuri na laini ya mama Samia ni nzuri, inatupoza lakini haitoshi kwa sababu haibadili sheria!. tunahitaji Katiba mpya yenye kuwabana hawa watawala ili wasitugeuze wananchi misukule yao, Kstiba itakayoondoa mambo ya "chuma ulete" nchini.
Tofautisha kati ya wanasiasa mafisadi na matajiri .Watz tuna akili na roho za kimaskini sana! Wivu umetujaa! Ndiyo maana kila tajiri tunamwita fisadi! Itachukua muda sana Tz kuendelea kwa aina ya wananchi tulionao
Mwalimu hakujilimbikizia mali na alikuwa na nyumba ya kawaida sana sana. Alikataa walipotaka kumjengea nyumba. Jeshi lilijenga kimya kimya na kumlazimisha aipokee. Na unajua wanajeshi wanajenga kwa jasho lao. Hapo gharama zilikuwa materials tu. Pia pensheni ya mwalimu ilikuwa ndogo sana na mshahara wake alipokuwa raisi. Baada ya kustaafu aliishi maisha ya kawaida sana. Alikuwa analima yeye mwenyewe kwa jembe la mkono. Huyu angalau alikuwa na uchungu na rasilimali za taifa hili pamoja na mapungufu yake.
wakuu acheni cheap politics, kafanye kazi familia yako istarehe kukaa kulalamikia benzi la watu ni matumizi mabaya ya vidole..
Sawa ni ya kawaida sana..swali ni je alijenga kwa pesa yake au kwa kodi za Watanzania?Nyumba ya Nyerere ni nyumba ya kawaida sana.
Alijengewa na JKT kama zawadi.Sawa ni ya kawaida sana..swali ni je alijenga kwa pesa yake au kwa kodi za Watanzania?
Basi huenda hata hawa wanopewa mahekalu ni zawadi!Alijengewa na JKT kama zawadi.
Nadhani kazibya JKT unaijua ni Ujenzi.
Vile vile Rais akistaafu huwa kuna zawadi nyingi tu huwa zinatolewa, hata wananchi wanaopenda hutoa zawadi za ng'ombe kwa hiari yao.
Kwao siyo zawadi. Hao walijitungia sheria, kwahiyo ni lazima kwa mujibu wa sheria haijalishi nchi iko katika hali gani kiuchumi au watu wengine wanaisoma namba kwa kiwango gani.Basi huenda hata hawa wanopewa mahekalu ni zawadi!
Sheria hii ilikuwepo kabla sema Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawakuitekeleza ila alipokuja Hayati Magufuli ndio akaanza kuitekeleza kwa kumjengea Mkapa, Mwinyi na Kikwete! nae pia atajengewa na SamiaKwao siyo zawadi. Hao walijitungia sheria, kwahiyo ni lazima kwa mujibu wa sheria haijalishi nchi iko katika hali gani kiuchumi au watu wengine wanaisoma namba kwa kiwango gani.
Unamaanisha ilitungwa enzi za Nyerere ?Sheria hii ilikuwepo kabla sema Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawakuitekeleza ila alipokuja Hayati Magufuli ndio akaanza kuitekeleza kwa kumjengea Mkapa, Mwinyi na Kikwete! nae pia atajengewa na Samia
Hapana..ilitungwa wakati wa Mkapa kama kumbukumbu zangu ziko vizuriUnamaanisha ilitungwa enzi za Nyerere ?