Hili suala la wastaafu kupeana Mahekalu, Mwalimu alisema ipo siku Watanzania watalidai Azimio la Arusha

Hapana..ilitungwa wakati wa Mkapa kama kumbukumbu zangu ziko vizuri
In short, Nyerere hakuwa mtu wa tamaa za mali.

Hata Mkapa nahisi hivyo, ila kilichomponza Mkapa ni kuwa na lundo la wachagga( wanafamilia) karibu yake hasa kupitia mke wake.
 
Duh hapo kwa wachagga mkuu naona unachokoza watu. Watakushukia kama mvua ya radi, wamejaa humu.
 
Mkuu mimi sijawahi kumwogopa mtu.

Hakuna asiyejua jinsi wachagga wakivyojichomeka vitengo nyeti enzi za Mkapa kupitia mke wake.

Huyo Anna Mkapa alimkontrol Mkapa hata kurudi kwao Lupaso akashindwa, wakaenda kuishi Lushoto, njiapanda ya kwenda Moshi.
 
Zawadi zote mbili walizopewa wastaafu ilikuwa wapewe na Hayati JPM kwa mujibu wa sheria. Mama Samia imebidi awape kwani ndio rais kwa sasa. Huku kulialia mitandaoni hakuna msaada wowote.
Katika kutunga hizo sheria wananchi walipakodi wanashirikishwa? Au ni genge fulani linajifungia na kuamua?
 
Azimio likasema kuwa Kiongozi maana yake ni mtu na mkewe!, Kwa hiyo unaona wazi kuwa mtu alipigwa pini kujitajirisha kwa kujigicha kupitia identity ya mke/mumewe.

Hivyo ndivyo Jinsi Azimio lilivyokuwa serious, halikutaka kabisa tabia hizi za kuchomeka mirija na kunyonya wananchi kwa kisingizio cha "alikuwa rais, anastahilo ajengewe"

Pia azimio lilitaka mtu ajitegemee, Kama ni mfanyakazi, basi jenga nyumba kwa jasho na kipato chako au pensheni yako!
1621842354980.png
 
Katika kutunga hizo sheria wananchi walipakodi wanashirikishwa? Au ni genge fulani linajifungia na kuamua?
Wabunge wanawawakilisha hao walipo kodi, wapo Dodoma muda huu wakitunga sheria na kupitisha bajeti kwa kutumia kodi hizo hizo.
 
Katika kizungumkuti hiki kinachoendelea leo, Wakubwa wanapeana Mahekalu na Mabenzi wakati wanananchi mamilioni kwa mamilioni wanatopea kwenye lindi la umasikini, Imenikumbusha kauli ya mwalimu Nyerere kuwa ipo siku wananchi Watasimama na kulidai tena Azimio la Arusha!

Binafsi ninajua kuwa azimio kama kazi yoyote ya mwanadamu halikuwa perfect lakini lilikuwa na misingi mizuri sana ya kung'oa unyonyaji haswa wa tabaka linalotawala!

Azimio lilikuwa kali mno kwa viongozi wa kisiasa, liliwabana kwelikweli, liliweka masharti magumu kwa wanasiasa kiasi kwamba walikuwa hawapumui. There is no way ungekuwa kiongozi wa kisiasa enzi za azimio kisha ukapeleka hoja za kujijengea Mahekalu na kupeana Benzi ukasurvive tena kisiasa.

Miongoni mwa mambo mazuri ya Azimio la Arusha ilikuwa ni Maadili ya viongozi. Ndani ya Azimio waliweka kanuni kuwa ni Marufuku kwa kiongozi kuwa hata na nyumba ya kupangisha! Na likaenda mbali kumdefine kiongozi ni nani, likasema kiongozi ni mtu yeyote mwenye wadhifa serikalini na chama, na Azimio likasema kuwa Kiongozi maana yake ni mtu na mkewe!, Kwa hiyo unaona wazi kuwa mtu alipigwa pini kujitajirisha kwa kujigicha kupitia identity ya mke/mumewe.

Hivyo ndivyo Jinsi Azimio lilivyokuwa serious, halikutaka kabisa tabia hizi za kuchomeka mirija na kunyonya wananchi kwa kisingizio cha "alikuwa rais, anastahilo ajengewe"

Pia azimio lilitaka mtu ajitegemee, Kama ni mfanyakazi, basi jenga nyumba kwa jasho na kipato chako au pensheni yako!

Ndiyo maana Mwalimu kakaa madarakani lakini hakuwahi kujitungia sheria akistaafu ajengewe nyumba, Hii maana yake ni kuwa aliamini suala la kujenga nyumba ya yeye kuishi ni kwa jasho lake, siyo kungoja ustaafu halafu Jasho na kodi ya wananchi ikujengee nyumba wakati pensheni unapata na unalipwa pesa kila mwezi zinazolingana na asilimia 80 ya mshahara wa raisi aliyeko madarakani! —Kwa nini usijenge mwenyewe kama unahitaji mijumba mingine hata kama unayo mijumba kedekede tayari!

Kwa hiyo ndugu zangu, huu ni kuda muafaka wa kukataa unyonyaji wa hii ruling class, kila kukicha wanafanya mambo ya kuwafanya waendelee kutunyonya huku wakitupiga kiswahili tuvumilie.

1. Wanapeana Mabenzi na Mahekalu.
2. Wamatunga sheria za kupeana Kinga wasishtakiwe kwa makosa wanayofanya madarakani.
3. Bungeni na kwenye baraza la wawakilishi wameweka watoto, wake na ndugu zao

Halafu sasa cha ajabu hawa watu walikuwepo enzi zile za azimio la arusha, Na mwalimu Nyerere masikini aliwaamini kuwa ni wenzie katika kuamini katika misingi ya kukataa dhuluma na unyonyaji katika nchi, kumbe walikuwa na lao moyoni, walikuwa wanamlia timing tu.

Tukatae mambo ya ajabuajabu haya ya watu kutuchukulia for granted!

Solution ya haya mambo ni katiba mpya, tena ya Warioba. Hii ni rasimu iliyoweka maadili ya viongozi ndani yake ili kujaribu kuondoa unyonyaji kama huu. Na hii ilitokana na wananchi kukerwa sana na mambo ya ufisadi.

Tuendeleeni kudai katiba mpya, hii lugha nzurinzuri na laini ya mama Samia ni nzuri, inatupoza lakini haitoshi kwa sababu haibadili sheria!. tunahitaji Katiba mpya yenye kuwabana hawa watawala ili wasitugeuze wananchi misukule yao, Kstiba itakayoondoa mambo ya "chuma ulete" nchini.
Hivi unajua mateso yaliyosababishwa na hilo azimio? kawaulize Babu na Bibi yako wakusimulie
 
Wabunge wanawawakilisha hao walipo kodi, wapo Dodoma muda huu wakitunga sheria na kupitisha bajeti kwa kutumia kodi hizo hizo.
Lakini hao wabunge nao ni wahuni tu, hayo maoni huwa yanakusanywa kwa wananchi gani au wanakwenda na agenda zao mifukoni ili kujitafutia sifa
 
Katika kizungumkuti hiki kinachoendelea leo, Wakubwa wanapeana Mahekalu na Mabenzi wakati wanananchi mamilioni kwa mamilioni wanatopea kwenye lindi la umasikini, Imenikumbusha kauli ya mwalimu Nyerere kuwa ipo siku wananchi Watasimama na kulidai tena Azimio la Arusha!

Binafsi ninajua kuwa azimio kama kazi yoyote ya mwanadamu halikuwa perfect lakini lilikuwa na misingi mizuri sana ya kung'oa unyonyaji haswa wa tabaka linalotawala!

Azimio lilikuwa kali mno kwa viongozi wa kisiasa, liliwabana kwelikweli, liliweka masharti magumu kwa wanasiasa kiasi kwamba walikuwa hawapumui. There is no way ungekuwa kiongozi wa kisiasa enzi za azimio kisha ukapeleka hoja za kujijengea Mahekalu na kupeana Benzi ukasurvive tena kisiasa.

Miongoni mwa mambo mazuri ya Azimio la Arusha ilikuwa ni Maadili ya viongozi. Ndani ya Azimio waliweka kanuni kuwa ni Marufuku kwa kiongozi kuwa hata na nyumba ya kupangisha! Na likaenda mbali kumdefine kiongozi ni nani, likasema kiongozi ni mtu yeyote mwenye wadhifa serikalini na chama, na Azimio likasema kuwa Kiongozi maana yake ni mtu na mkewe!, Kwa hiyo unaona wazi kuwa mtu alipigwa pini kujitajirisha kwa kujigicha kupitia identity ya mke/mumewe.

Hivyo ndivyo Jinsi Azimio lilivyokuwa serious, halikutaka kabisa tabia hizi za kuchomeka mirija na kunyonya wananchi kwa kisingizio cha "alikuwa rais, anastahilo ajengewe"

Pia azimio lilitaka mtu ajitegemee, Kama ni mfanyakazi, basi jenga nyumba kwa jasho na kipato chako au pensheni yako!

Ndiyo maana Mwalimu kakaa madarakani lakini hakuwahi kujitungia sheria akistaafu ajengewe nyumba, Hii maana yake ni kuwa aliamini suala la kujenga nyumba ya yeye kuishi ni kwa jasho lake, siyo kungoja ustaafu halafu Jasho na kodi ya wananchi ikujengee nyumba wakati pensheni unapata na unalipwa pesa kila mwezi zinazolingana na asilimia 80 ya mshahara wa raisi aliyeko madarakani! —Kwa nini usijenge mwenyewe kama unahitaji mijumba mingine hata kama unayo mijumba kedekede tayari!

Kwa hiyo ndugu zangu, huu ni kuda muafaka wa kukataa unyonyaji wa hii ruling class, kila kukicha wanafanya mambo ya kuwafanya waendelee kutunyonya huku wakitupiga kiswahili tuvumilie.

1. Wanapeana Mabenzi na Mahekalu.
2. Wamatunga sheria za kupeana Kinga wasishtakiwe kwa makosa wanayofanya madarakani.
3. Bungeni na kwenye baraza la wawakilishi wameweka watoto, wake na ndugu zao

Halafu sasa cha ajabu hawa watu walikuwepo enzi zile za azimio la arusha, Na mwalimu Nyerere masikini aliwaamini kuwa ni wenzie katika kuamini katika misingi ya kukataa dhuluma na unyonyaji katika nchi, kumbe walikuwa na lao moyoni, walikuwa wanamlia timing tu.

Tukatae mambo ya ajabuajabu haya ya watu kutuchukulia for granted!

Solution ya haya mambo ni katiba mpya, tena ya Warioba. Hii ni rasimu iliyoweka maadili ya viongozi ndani yake ili kujaribu kuondoa unyonyaji kama huu. Na hii ilitokana na wananchi kukerwa sana na mambo ya ufisadi.

Tuendeleeni kudai katiba mpya, hii lugha nzurinzuri na laini ya mama Samia ni nzuri, inatupoza lakini haitoshi kwa sababu haibadili sheria!. tunahitaji Katiba mpya yenye kuwabana hawa watawala ili wasitugeuze wananchi misukule yao, Kstiba itakayoondoa mambo ya "chuma ulete" nchini.
Watz hawa hawa wanaovimbiwa ugali na kuridhika kwa kanga za ccm au watz gani ?
 
In short, Nyerere hakuwa mtu wa tamaa za mali.

Hata Mkapa nahisi hivyo, ila kilichomponza Mkapa ni kuwa na lundo la wachagga( wanafamilia) karibu yake hasa kupitia mke wake.
Hayati mwalimu alikuwa mzalendo wa kweli kama wanamajumui wengine wa Afrika kina hayati Kwame Nkurumah, Samora Machel, Thomas Sankara, Keneth Kaunda, Patrice Lumumba, Sekou Troure and the like, ambao walikuwa a nia ya dhati ya kuwakomboa waafrika...bahati mbaya sana waliwasomesha vijana ambao waliiga maisha ya wazungu na kuingiwa tamaa ya ubinafsi, na ndio hawa wamekuja kuwa viongozi wetu wa sasa! Angalia hapa kwetu kuna kitu kina itwa Tume ya maadili ya viongozi....moja ya kazi zake ni kufuatilia mali za viongozi, lini ulisikia imehoji maadili ya kiongozi yeyote?
 
Back
Top Bottom