Hili tangazo la MUNIO sijui nini station sisi wahehe hatupendi

Hili tangazo la MUNIO sijui nini station sisi wahehe hatupendi

Japan, DRC na Zambia na wenyewe wana majina tatanishi sana kwenye tafsiri ya lugha yetu ya Kiswahili.
Bahati nzuri wao wako mbali...Sasa mwanakwetu anapokuja na jina tata sharti tumjulishe.....huo mfano wa njegere na bondeni kati ya Wahehe na Wanyakyusa mpaka kesho eanaheshimiana....ukiwa uheheni na wewe ni Mnyakyusa huwezi kusema kwitongo na ukiwa mhehe ukawa unyakyusani huwezi sema fiworo ukimaanisha njegere maana waisa watakutia banzi la uso!!
 
Yaani akifika huku huyo sharti la kwanza abadili jina!... ni sawa na fiworo kwa wahehe ni njegere ila kwa wanyakyusa ni kile kifanyio cha kiume...au kwitongo kwa kihehe ni bondeni ila kwa Kinyakyusa tusi
Sungwila
 
Munio abakie zake tu Arusha na Kilimanjaro. Kule wanaendana. Alijaribu kuja kuanzisha biashara yake ya mafuta Iringa, Wahehe walishindwa kulielewa hilo jina.


Nakumbuka kuna mtangazaji mmoja wa reduo ya pale Iringa mjini (Ebony Fm) Edo Bashir aliendesha kampeni kupitia kipindi alichokisimamia hadi jamaa alikimbia.

Kwa Wahehe neno MUNIO ni tusi kubwa!
Unaposema munio ni tusi kubwa sana una maana gani?
Mkund.u mbona ni kitu anacho binadamu kinakuwaje tusi kubwa?
Kwahiyo kila mtu ana tusi kubwa sana mwilini mwake?
 
Unaposema munio ni tusi kubwa sana una maana gani?
Mkund.u mbona ni kitu anacho binadamu kinakuwaje tusi kubwa?
Kwahiyo kila mtu ana tusi kubwa sana mwilini mwake?
Kwa hiyo unaweza ukaanzisha biashara yako ya mafuta sehemu na kuiita MKUND.U PETROL STATION? Ni kwamba hujui kuhusu taboo words, au unataka tu mabishano yasiyo na sababu?
 
Back
Top Bottom