Sababu kubwa ya kutofanya military mobilization ni kukwepa madhara ya kisiasa yatokanayo na vita. Ukifuatilia kila vita inayoisha duniani inasababisha madhara kisiasa na kijamii, baada ya WW2 wapiganaji waliotokea Kenya wakaanzisha Maumau, Marekani ikapata housing crisis, nchi nyingi Afrika zikataka uhuru. Urusi ndio kabisa hao mabadiliko yote hutokea baada ya vita. Bolsheviks walipata nguvu baada ya Russian empire kushindwa vita ya kwanza ya dunia na wa kulaumiwa alikuwa Tsar Nicholas II ambaye baadae wanamapinduzi walimuua na familia yake.
Vita ya pili ya dunia Soviets walivamiwa, hiyo haina budi mpigane ila ilipoisha ikaacha ideologies mbili na kusababisha Cold war. Campaign ya Soviets nchini Afghanistan dhidi ya Mujahideen ilileta madhara kiuchumi na kuishawishi duniani kwa Soviet Union, walipoamua kuondoka wakakaa miaka miwili muungano ukavunjika.
Inasemekana Waziri wa Ulinzi wa Urusi alishapendekeza mara nyingi wafanye mobilization ambayo kijeshi ni sahihi ila kisiasa sio sahihi. Putin kakaa madarakani miaka 22 sasa, ukifuatilia kwanini baada ya Iran - Iraq war Saddam Hussein aliua majenerali wake wengi wa vita, na ukifuatilia kwanini Stalin alifanya The Great Purge na kuua majenerali wake miaka ya 1930s utajua kwanini autocrats huwa wanapata shida sana na jeshi lililotoka kuwa active.