Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Siyo kila wazo la wapinzani ni baya.
Upinzani una kawaida ya kuonyesha mapungufu ya sera za chama kilicho madarakani na kuzikosoa, kwa manufaa ya nchi.
Niseme wazi, mimi ni mwana CCM, kada.
Hiki kilichoongelewa na huyu mwananchi wa chama kingine makes sense.
Viongozi waliopo sasa na waliopita sasa wanaanza kujijengea Usultani.
Sultani hafanyi kazi, anakula kodi za wananchi mpaka kufa.
Na kawaida ya Usultani, huwa wanataka kurithisha Usultani kwa wana wao.
Hili la mafao ya wastaafu ambalo limeongelewa kwenye clip siyo siri linawakera hata wana CCM wengi.
Mwalimu Nyerere alipinga ubwanyenye na unyapara, na aliishi hivyo.
Hakutaka kuishi kwa kodi za wananchi zaidi ya kile alichostahili kama mstaafu.
CCM iwe makini, tusijenge tabaka la the Haves, masultani, na kwa ukweli kabisa, Kikwete katika hili anajizolea sifa mbaya.