HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

Tuanzie hapa kwanza [emoji117] Young Lunya anaimba mziki gani?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Shaolin senetor

Baada ya kuzama naibuka na mada, tega skio fatilia simu ya dada/

Sio mwingine huyu ni dada tele, anasimu unaweza piga mpaka mbele/

Na shimo moja la kuchomekei chaji, anaijali sana anaitumia kama mtaji/

Simu yake inafanya apate mabwana, anavyolinga nayo utadhani wenzake hawana/

Wajanja wanaiminya kwa vidole, ilivyokali mpaka wenzie wanataka wampole//

Alipiga baba alipiga mjomba, dada alidata ile siku alivyopiga kaka//

Simu ya dada hua haipigwi na maboya, maana ni kali na nje inakava la manyoya//

Aliniambia bila simu haiishi mjini, haiachi nyumbani mda mwingi inakaa mwilini/

Inajicho la kamera kali kinoma, fungua bluetooth muone anavyorusha ngoma/

Walipiga watu kumi alivyolewa cham, nilidata simu ya dada hata mimi siifahamu//

Song: simu ya dada
 
Mbeya boy chuma

Napiga taya vibao stair ngumi chek mitindo, mapigo mabaya wote wako chini ya ulingo/

Nilivyosugu demu gani wakunivunja shingo, mistari tindo wako chini ya ukingo/

Nikisimama sioni mdada wakutamba, uliza wenzako nilichomfanya sholi mwamba/

Bila nguvu porini navuta kitu, moshi unatoka mwingi kama nachoma msitu/

Nazika marapa walijua mazishi, nilivyo kaligraph yo wakajua madishi/

Kichwani raga maphy nabugi nipo rumba, rap yangu kama choo kwaiyo nipo kila nyumba/

Cheza kibaiskel si unamiguu ya peda, mi nagonga demu yeyote hata akae kwenye zebra/

Rhymes sio matusi ila zinawachanganya, mfano we sio hesabu na nina uwezo wa kukufanya/

Song: hasi na chanya
 
Nikki mbishi sio underground japokua hata yeye anapenda aitwe hivyo

So mimi ni nani hata kupingana naye, kuwa underground haina maana tunayoijenga hapa.... ni aina fulani ya hiphop chimbuko na ndo hasa inazingatia misingi.
 
So mimi ni nani hata kupingana naye, kuwa underground haina maana tunayoijenga hapa.... ni aina fulani ya hiphop chimbuko na ndo hasa inazingatia misingi.
Basi tumetofautiana kimaana, mi nilimaanisha wasanii wasiosikika au chipukizi ambao hawana majina makubwa ambayo yanawafanya wasijulikane na wengi kulingana na mziki wanaoufanya
 
Boshoo nilimwelewa kwenye 10 za Maangamizi, kwa michano safi na punchlines konki.... ila ‘official tracks’ ni kawaida mno sijui kwa nini..!!
Hii naona ipo kwa mbeya boy. Mneya boy kwenye 10 za maangamizi sidhani kama kuna msanii kamzidi pale lakini ukija kwenye track zake zakawaida sana
 
Hamisi mistari

Wanasema ukipenda hauoni, japo unamacho umewekewa usoni.../

Mbele yangu mwema unanitenda kisogoni, napata hasira zaidi ya mtu aliyetenda wema halafu anaenda motoni.../

Skia hapa mtaani unavijana wangapi, nilikuta meseji tukutane sijui mlikutana saa ngapi.../

Au ndio wale hawapo wcb ila wanajiita wasafi, unaniacha mimi unaenda kuwafata walafi.../

Tukiwa pamoja hauna hata ile stimu, una mambo mengi yani upo bize na simu.../

Kama ni mwili basi unauza lejaleja, kila mtu ana namba yako zaidi ya wahudumu kwa wateja.../

Kumbuka juzi tulilala ukajitoa kifuani, baada ya simu kupigwa ukajiondoa chumbani.../

Unavyofanya hivyo unahisi unamkomoa nani, jamaa yako anajiita sudi mi nisha muondoa duniani.../

Yaani sijamaanisha kukupa talaka, ila namaanisha kukupa walaka.../

Upendo wangu kwako najikuta nadata, yani mpagani huna dini halafu nakupa sadaka.../

Unajiona mjanja yani unajikuta wasasa, mwisho wako upo utajikuta umenasa.../

Siku narudi home nakuta kundi la watu, wadada wembamba mithili ya kundi la wafu.../

Walikusuta unatembea na wanaume za watu, acha hiyo walikubaka ulikunywa pomne za watu.../

Usidhani kwamba nilikua nazikosa tetesi, unatangaza nakibamia we u ajipoza fenesi.../

Haukua mzito nilikuona mwepesi, siku nashughulika kitandani we unasoma gazeti.../

Song: nashindwa
 
Unamaanisha nini ukisema underground?

Nina miaka karibia kumi sasa nasikiliza ngoma za Kadgo, naye ni underground?

Kwa hao uliowataja namkubali Dizasta Vina na Kadgo.

Huyu Dizasta ni balaa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa wafatiliaji wa hip hop kindaki ndaki basi kadgo lazima wamjue.

Napozungumzia underground namaanisha wasanii wasiojulikana na wengi. Leo hii ukiwauliza watu kadgo ni nani sio wote watakao mjua mara nyingi wasanii hawa wanajulikana sana na watu wanaofatilia hip hop in deeper
 
Back
Top Bottom