Conversation ya shaolin senetor na dizasta
Shaoilini kacheza kama baunsa anayechukua pesa ya viingilio kwa ajili ya show ambayo inatumbuizwa ukimbini. Wakati dizasta kacheza kama tozi ambaye anafosi kuingia ndani na hana pesa ya kiingilio
Shauli seneta X dizasta
[Shaolin]
Panga mstari hapa mpaka kule, tiketi mkononi maana hakuna wakuzama bure//
Over 18 hichi sio kiwanja cha shule, kuweni makini hii ni kazi inayotufanya tule//
Oya tozi unaenda wapi hauna hela, na unaona foleni rudi nyuma upange tela//
[Dizasta]
We boya usiniguse unanichafua, ntalipaje hela wakati boss wako ananijua//
[Shaolin]
We bishoo acha masihara na kazi, au unataka mpaka tuanze shikana mashati//
[Dizasta]
Yeah jinsi mwili wako unakulaghai, na icho kifua mkate men dawa yake chai// eeh
[Shaoulin]
Tambua kua niko hapa kama mlinzi, na hii nayo ni kazi kwaiyo nacho hitaji shilingi//
[Dizasta]
Nini kazi? Kazi yenyewe ni ubaunsa, haufiki hata nusu ya mshahara wa kaunta//
[Shaolin]
Acha wenge wewe ni mtoto wa mama, kama hauna hela uza buti ili uweze kuzama//
[Dizasta]
Kama ungejua mi nina pesa ungenipisha tu nipite, naweza kulipa hadi wenzio sita wanilinde//
Kama haujajua mi ni star basi, jua leo mtaani naheshimika ka gadafi//
Acha gari nyumba kwanza mi ni msafi, ungenipisha tu hata kunishika huna hadhi//
Nimetupia shati juu kofia raba kali halafu nina bonge la modo, naenda kwenye party nafika getini baunsa anasema hanijui hata kidogo//
Oya baunsa unazingua, tozi unazingua..Oya baunsa unazingua, nyie matozi mnazingua...Ona baunsa unazingua, hapana tozi unazingua....Oya baunsa unazingua, tozi unazingua
Yap demu wangu amechoka kusimama, sa si bora ukaniruhusa tu nikazama?// Unajibabaisha, eh unanidhalilisha ujaniskia mi ni star kwenye interview jana?
[Shaolin]
Hauna tiketi rudi nyuma, hauna hela halafu toka mbele yangu nisije nikakuonea huruma/
[Dizasta]
Kwanza nina hela kubwa sidhani kama una chenchi, ebu skiza huyo sio tundamani kwenye stage//
[Shaolin]
Elfu kumi haina chenchi ndiyo mtonyo, kama ipo chukua tiketi dogo acha mdomo//
[Dizasta]
Nitamwaga pesa nyingi hadi ujute kunidani, kama zipo basi zikae mbele kama tai//
[Shaolin]
Kuchugulia ni ruksa, panga tofali kama huwezi subiri fungulia mbwa//
[Dizasta]
Excuse me men, fungulia mbwa kivipi wakati nina track na jux mzee//
Foleni nyuma ni michosho, kukanyagana visa vipi kuhusu juma nyoso//
Halafu huko ndani kuna mchongo, lazima niingie sasa huoni nilivyonyuka mtoko//