HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

Boshoo ninja

Kila nikifanya wanahanya sio siri, nikichana yanapanda maruani nadhikiri.../

Natumia akili bingwa in dar, wanashangaa ni underground ila na hang ki star.../

Nikiwa bar mi ndo boss uyu mupe yule muluke, nyie matozi mmepandisha bei ndala nyeupe?...?

Eti bongo bahati mbaya halafu unavaa unapendeza, bongo kama ulaya tu uchawi uwe na fedha.../

Skiza nacheza na lugha, ntakutoa udhu wewe usicheze na mbwa.../

Unashangaa nini ndani bikini nje juba, au unashangaa kuona sheria inapindishwa na fuba.../

Fata hii acha ile ni upuuzi uliotukuka, sio bongo ya zaire usi mix na kapuka.../

Shtuka nakupa ujanja chukua kama hujaipata, we kilaza mkono wenye shombo haufukuzi paka.../

Wanaishi na chuki zao ila hawazioneshi, kama wakike kasoro maziwa hawanyonyeshi.../

Song: michano
Huyu jamaa ni hatari nimemsikiliza sahizi clouds ni hatari🙌🙌🙌🙌🙌😂😂😂😂
 
Umeshindwa kukidhi, utu unakutoka sababu umeshikwa na dhiki.../

unasahau lengo unasahau umesimamishwa na sisi, pesa inakuyumbisha nawe unayumbisha misingi.../
Mkono wa nani na unaitwaje Tafadhali?
 
Asubuhi kume pambazuka, tangazo kwa balozi tozi kama unapamba nyuka.../

Mishe mishe kibao mangi anapanga duka, mi napiga pushup we kama unakamba ruka.../

Leta chai na mkate, hilo jicho sio la ngwai mbona umelegea kama umepigwa mate.../

Nilichonacho mungu amekunyima hauna, nala ni udambwi dambwi niyonzima haruna.../

Nawala sio ngumu kuchana kama hivi, rahisi kama ndumu kupasiana kwa machizi.../

Huyo jamaa uliyemskia sio mimi, kama kwenu kuna mataa hakuna studio sio mjini.../

Usipime mkwara mi nina kilo tisa, utapigwa ngumi upotee ubaki na hiyi picha.../

Mnaojiita maraisi wa morogoro mjichunge wanangu, mkipita seginali mniache na ubunge wangu.../

Huna cha kunisumbua, labda uongee kuhusu raha ila mateso nayajua.../

Alifariki kwa ajali dada yangu kama unajali afya yangu lete leso na mafua.../


Mtu mfupi mistari mirefu (diego naladona)
 
Nyenza mc Stanza

Naendelea na ufundi wa daraja, ili niepushe bundi linalotaka faraja.../

Stress hua gundi katikati ya mapaja, kama ndoto haziungi ubani hauna haja.../

Kukosa mipango ni ugonjwa wa hatari, utagonga milango kumuona daktari.../

Utaomba michango kukusanya daftari, kisa hakuna jambo ulilofanya tayari.../

Kukosa ujuzi ndio kutofika haraka, kukosa kurunzi ndio giza linavyotaka.../

Leo fanya maamuzi ya kisasa, maamuzi ya juzi tayari yaliisha chacha.../

Maswali mengi unayojiuliza, kwanini nuka yako iitwe yai viza.../

Hata wenzako walishawahi umizwa, huu ndo muda wako wa kutenda miujiza.../

Kitoe nje unachokifanya chumbani, kama kina alama ya kushika usukani.../

Vyote vyenye maana vilianzia kichwani, ndoto zako ni pana zisiishie kinywani.../

Fanya yote ila hili tafadhali, kwasiku usikose muda wa kutafakari.../

Wala usichoke kua unawaza mbali, usiogope jambo kama halina hatari.../

Usiwaafiki wanaofanya kitapeli, muwa wa usaliti ndio huzamishaga meli.../

Fanya kile na hiki hata kama vitafeli, ghafla ukifariki uwe ushafanya kweli.../

Uungwana daima uleta ndio, walishazama waliopima matamanio.../

Endapo kama utaniazima masikio, utaanza kufanya dhima za mafanikio.../

Pweza mwenye mikia ya mitaa, anayependwa na wanaoichukia sanaa.../

Anavyovieleza sisi tunapitia haswaa, sisi tuliopotezwa anatuwashia taa.../

Ni harabu kuwa fundi wa sarufi, vina vyenye adabu kwenye kundi la salute.../

Fanya kwasababu kesho huikuti, upo leo kwasababu ndo maana leo hufi.../

Mimi na nyie hakutakalika tena, madini yangu mie yanapita njia njema.../

Yanini mtumie rap kupindisha mema, maana ni mimi tu naye andika vyema.../

Nyenza bwana tumesha kua mzee, huko kupangiana jua usituletee.../

Hasara ya ujana kujichetua aisee, utataka busara ukishakua mzee.../

Beat na kinanda hua na mzuka wake, ndo maana natamba mchaga na duka lake.../

Pamoja na kwamba nayokupa ni machache, ila elewa kwamba hautajuta nifate.../


Unakwenda nje ya nchi kusaka ajira, au unakwenda tu kufata mazingira.../

Ukirudi ndani ya nchi mambo yako bila bila, ulotuacha ndani ya nchi tushazidaka ngawira.../

Bahati mbaya ndo pacha wa samahani japo kwa wengine bahati mbaya ni kejeli, sio mbaya kuweka ukweli kwenye utani ila ni mbaya ka utaleta utani kwenye ukweli.../

Dharau ndio panga yenye nongwa, chumvi ya kidonda chake haipaswi hata kuonjwa.../

Wangapi washakupanga halafu wakakuponda, umesahahu uongo wa mganga ndio nafuu ya ugonjwa.../

Vina vyenye perfume haununui, au unataka vina vyenye pumu uwe haupumui.../

Mkwepa majukumu daima hakui, mbishi hua mgumu hadi kujua hajui.../

Kipi kinaisibu hii hip hop culture, wagonjwa mpo wengi leo nawatibu cancer.../

Mnaojinasibu nyie ni freestyle masta, nadhani majibu tayari mmeshapata.../

Wengi wao hakuna kuumiza kichwa, ndo mana wanajiuliza navyo chanika.../

Vile nahimiza hii culture kuandika, nasikilizwa na wote bila kuacha rika.../

Mitaa yako wanajua we ni king, ila fikra yako tunajua we ni thing.../

Kile ambacho unajua ni ushindi, ukifumbia macho itakua ni upimbi.../

Achana na ishu za kuiga, tobo limeonekana lete kitu kuziba.../

Rap ya jana inakitu ma nigga, leo kila siku nyama kusifia kila figure.../

Vina vyao vyote vina utandu, nawaoiga chenga wote kupitia kanzu.../

Usipende niokote ukijua si chakwangu, sipendi popote kwakua nina kwangu.../

Uswazi ndo kuna mambo ya kusutwa, mademu wako shazi wanadata na sofa za kufa.../

Iko wazi we huwezi kunigusa, siwe uwe radhi useme mama nakufa.../

Nyie makaka mcheze mbali, vina vitawakata tuwacheze mwali.../

Kutoka kwa mtata overdose kali, lei tupo na papa vichwa vya habari.../
 
Skuizi wauswazi wanaji mix nyuma hawataki kubaki, dada anajiongeza anajisogeza kwa fataki.../

Utaskia naitwa cindy home masaki, kumbe ni mwasiti wa keko magulumbasi.../

Ni wavivu wezi wanajua ku act, nacho wasifu hua hawaaribu kwenye scripts.../

Hali ni tight ila mmh tunaoumia ni sisi, maskini tutakufa na ukimwi uwanja wa fisi.../

Demu wako anaku-cheat na unajua, huna kitu sa ukiwa na wivu si atakuua.../

Una ishu sasa ndo maana unashindwa kuamua, ndo maana unakumbuka ile michezo alivyo kusisimua.../
Mkonk unaitwaje na wa nani?
 
Nala mzalendo

ndugu na jamaa

Alhamdulilah mshukuru mungu amekupa pumzi, tumia kila dakika kujiepusha na upuuzi/

Amekupa leo amekupa jana alikunyima juzi, mshukuru sana mshukuru maulana ye ndo mwenye maamuzi/

Ameshusha viumbe, dunia duara ndo maana binadamu tunazungukana kumbe/

Mwema wa sasa mbaya baada ya sekunde, kua na msimamo simama imara usiyumbe/

Watakuja wawili kwa muda tofauti, watakufanya ufikiri ujiulize we ni yupi/

Wakwanza atakuambia we ni boya sana, akija wapili atakuambia we ni bora mwana/

Kaa mbali na wanaoumiza moyo wako, ishi na wale ambao watatimiza ndoto zako/

umezaliwa kwenye mwanga hilo giza sio lako, unaweza jiamini fanya miujiza yako/

Unakaa nao kijiweni unashinda home, siajabu kukunyima chakula na kukupa kondomu/

Unafurahi unahisi upo mahala pa amani, shtuka unaishi na mawakala washetani/

Kesho mbali tafuta leo, nyota begani muombe mungu akulinde kesho unaweza ukaamka umefutwa cheo/

Unaweza kufa leo, kisa umemkuta mkeo au mmeo anjirusha na mtu kama kipepeo/

Utapata wapi upendo sikuhizi hakuna, hata ngazi ya familia kuna mambo ya utumwa/

Utaskia mjomba mwanao si amemaliza form four, mwanao ukienda kwao ye ndo wakudeki choo/
 
Eti mpende akupendae sa utajuaje kama unapendwa, hata unayempenda kuna anayempenda we unategwa..../

We unazugwa kisu unanunua kwa vumba, sa huyo mchumba au ndo chuma ulete bwana mkubwa.../

Pedeshee naskia siku hizi mapenzi pesa, onga gari utamkuta bitozi analiendesha.../

Na ukikosa kabisa ndo utachekesha, utawaita shemu chips utatumwa na utapeleka.../
 
Najua wengi ni mashabiki wa wasanii fulani fulani wa mziki pendwa wa hip hop ila leo nataka tuangazie kidogo hawa ma underground hip hop.

Katika tansina ya muziki huu wa hip hop tunaona jinsi gani evolution ilivyobadili ladha ya mziki huu kiasi cha wasanii kuimba nyimbo ambazo hazina lyrical wala critical.

List yangu ni hii hapa na wewe unaweza kuweka yako.

1. Dizasta vina
2. Nala mzalendo
3. Kadgo
4. Boshoo ninja
5. Kinya mistari
6. Shaolin senetor
7. Mbeya boy chuma
8. Hamis mistari
9. Ado gado
10. Nyenza MC

Wapo wengi ila kwasasa nianze na hao halafu chini nitanukuu mistari yao katika baadhi ya nyimbo zao
Nakuunga mkono mkuu naomba niongeze list, napenda kusikiliza hiphop , pia huwa nasikiliza kazi nyingi za Underground.
Rapcha
Sele Mentality
Ibra wa Rhymes
Rabi James
Fivara
Ambeko
Freddy Mula
Zenji Boy
Pablo aka fresh like uugh
Kado Kitengo
Mteganda
Wa Kiafrika
Jos Mwanahapa
Wussein
Black MC
Stan wa Rhymes
Category MC
Jaco Jeez
Elisha
Adam shule Kongwe
Miracle noma
Bars Writer
Sacho MC

Asee wapo wengi...
 
Eti unadhani anakupenda eh anakupeti peti, anakupa mpaka code za simu usome text, anakupost.../

unafurahi anaku-joke, Eti utalalia gogo man ukidhani ni kapeti..../

iko wazi si wanaume haturidhiki, ni ukweli uliowazi haipingiki haifichiki.../

iLa utandawazi ndio huo, demu unanitosa mimi simu inakuvua nguo, ujinga ndo huo.../

Huku mtaani kumenuna, wanawaita madanga hawa madingi wanaopunwa.../

Cha mtu hakiendi bure jichunge dada maimuna, utatengeneza ngoma kwa hiyo ngozi ulioichuna.../
 
Nakuunga mkono mkuu naomba niongeze list, napenda kusikiliza hiphop , pia huwa nasikiliza kazi nyingi za Underground.
Rapcha
Sele Mentality
Ibra wa Rhymes
Rabi James
Fivara
Ambeko
Freddy Mula
Zenji Boy
Pablo aka fresh like uugh
Kado Kitengo
Mteganda
Wa Kiafrika
Jos Mwanahapa
Wussein
Black MC
Stan wa Rhymes
Category MC
Jaco Jeez
Elisha
Adam shule Kongwe
Miracle noma
Bars Writer
Sacho MC

Asee wapo wengi...
Hapo wakiafrika na miracle noma pamoja na cado kitengo ndio ambao nimewajua ila hao wengine nimetoka kapa

Labda utuwekee verse zao hata kwa ufupi kama ikiwezekana
 
1Dizasta vina
2Mbeya boy chuma

Sent using motorola
 
Back
Top Bottom