HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

Kadgo Kadtwende.

What's up Mecko South fellas.

-Kaveli-
 
Najua wengi ni mashabiki wa wasanii fulani fulani wa mziki pendwa wa hip hop ila leo nataka tuangazie kidogo hawa ma underground hip hop.

Katika tansina ya muziki huu wa hip hop tunaona jinsi gani evolution ilivyobadili ladha ya mziki huu kiasi cha wasanii kuimba nyimbo ambazo hazina lyrical wala critical.

List yangu ni hii hapa na wewe unaweza kuweka yako.

1. Dizasta vina
2. Nala mzalendo
3. Kadgo
4. Boshoo ninja
5. Kinya mistari
6. Shaolin senetor
7. Mbeya boy chuma
8. Hamis mistari
9. Ado gado
10. Nyenza MC

Wapo wengi ila kwasasa nianze na hao halafu chini nitanukuu mistari yao katika baadhi ya nyimbo zao
Big up kwa kudadavua !!!
 
Najua wengi ni mashabiki wa wasanii fulani fulani wa mziki pendwa wa hip hop ila leo nataka tuangazie kidogo hawa ma underground hip hop.

Katika tansina ya muziki huu wa hip hop tunaona jinsi gani evolution ilivyobadili ladha ya mziki huu kiasi cha wasanii kuimba nyimbo ambazo hazina lyrical wala critical.

List yangu ni hii hapa na wewe unaweza kuweka yako.

1. Dizasta vina
2. Nala mzalendo
3. Kadgo
4. Boshoo ninja
5. Kinya mistari
6. Shaolin senetor
7. Mbeya boy chuma
8. Hamis mistari
9. Ado gado
10. Nyenza MC

Wapo wengi ila kwasasa nianze na hao halafu chini nitanukuu mistari yao katika baadhi ya nyimbo zao
Hakuna anayeimba hip pop apo wote wapga kelele ila fundi wao ni SALMIN SWAGZ
 
kwenye beat hii mi sitembei hua na nyatanyata, ommy dimpo na nandy ndio wana kata kata/

ukiwapa hata salaam wana natanata, halafu wakiniona natoka bank mnanifuata fuata/

hutambui ubaya wangu ebu nicheki home, wanaotaka kujiua embu wapeni sumu/

usishangae mi ndo nilivyo na' verse ngumu, sio konde boy welcome to my bedroom/

marapa wako wakiniona hawafoki foki, kawaida yangu nikichana hua sichoki choki/

studio kubwa nikifika hapatoshi toshi, njoo geto yani sina kuni ila mimoshi moshi/

sijui lini mi ntatoka mzee, toka kitambo mi nina foka mzee/

mademu zao nawakosha mzee, wananifata hadi nachoka mzee/

hamjui nilipotoka mzee, nasema ukweli sio naropoka mzee/

demu wa t.i.d kaninunulie zeze, sina pesa sijui nikagongee veve/

hamisi mistari
 
nikichana hivi nyie sijui mnachana vipi,mnachana nini wala sielewi mnachana kipi/

sista duu hivi unataka nini, sina pesa na' mistari au we ndo unantaka mimi/

toka ndani habari kumesha kucha, serekali moja kuna serikali ya mizuka/

naendesha beat nimeishafika suka, nina mistari hatari uliza na kama unabisha vuka/

natapeli kama mjinga kwenye jiji, mifugo inapata hofu zaidi ya simba kwenye zizi/

na niko fresh zaidi ya fid, nikichana wanatikisa kichwa nawapa stimu ka ya weed/

navyo nata kwenye beat zaidi ya mnato wa ruba, sina msamaha wananiita hamisi mgambo wa quba/

wasiojua uandishi nawafunza kwa kuchora, vile na' barz takatifu ka zimetungwa na mola/

credits: hamis mistari
 
hata mkija kundi mi sijali, sina wasi sina wenge nimeshafika fundi mistari/

wanaoleta chuki na habari, natema laana na mikosi ndo yule bundi hatari/

verse nagawa bure sa uloho wa nini, njia inamiba kwahiyo njoo makini/

nakuchana wewe unaleta ukoo wa nini, unakosea unapo nifananisha na joh makini/

na hii ni nchi ndogo kama togo, ukigeuka nyuma hunioni kama chogo/

hatua ndefu kama bolti kwenye foto, hawataki kuniona dzaini ya koti kwenye joto/

kwa hizi rythms hata fid anaisoma fresh, nimefika jaji hamisi naisoma kesi/

mshtakiwa vipi ulipata kesi, nashangaa ulikua mgonjwa sa vipi ukambaka nesi/

credits: hasmis mistari
 
ni mimi mwanajeshi ambaye nimeaminiwa, nikirudi bila ushindi naamini nitahukumiwa.../

nimekuja kupigana sio kupiganiwa, mlioikacha misingi na mzidi kulaaniwa.../

beba pen na paper, skiza nachosema beba maarifa kisha sepa.../

muda wa sala vitani jada tandika mkeka, wanajeshi wenye amani tunacheka na mateka.../

na hii sifanyi tuchukulie poa, msituzoee kiasi cha kutuchukulia ndoa.../

ni mimi na taifa langu, ukitoa hip hop kuna mimi na maisha yangu.../

taifa la rap, ni zaidi ya chuo kizazi cha trap utabaki taifa la sup.../

hip hop ndo mchongo, na hauna wakunitisha najua wote ni watu wa udongo.../

ninae jithamini kabla sijathaminiwa, amini nilijiamini kabla sijaaminiwa.../

namuona mfalanyongo kwa mbali akila miwa, tupo chini under kini bado hatujafukiwa.../

taifa langu lina vikosi vya kutosha, msishangae hatuogopi tunaogopwa.../
 
Unamaanisha nini ukisema underground?

Nina miaka karibia kumi sasa nasikiliza ngoma za Kadgo, naye ni underground?

Kwa hao uliowataja namkubali Dizasta Vina na Kadgo.

Huyu Dizasta ni balaa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Underground au Hiphop ya handakini....unafuata misingi ya hiphop siyo matakwa ya media...mfano dakika za wimbo..aina ya ujumbe na mengi tu.
Usichanganye Underground na Upcoming.
 
najiskia uchovu na mihayo napiga, uliza hizi nyayo na nyika/

nimetoka mbali fanya maamuzi tuhitimishe kikao, maana hata mimi nina mishe kibao.../

mishe hata wewe unazo mishe unazo badili, fafanua eleza na uweke mifano isawili.../

huo ubishi wa kujikweza weka kando ukatiii, leo ndio mwisho vina navunja ndoa yako batili.../

andika talaka ili tuondoke, maana maamuzi ni yako au chukua panga unichome.../

haukuitendea haki kura yako, kuchagua ndoa wakati sio jambo kubwa kwako.../

utakapochukua wasaa utagundua ulimpa saa alipohitaji muda wako.../

anajua kua mkoa wa mbali una watoto, anajua kuhusu vikao na safari za uongo.../

anajua kuhusu kondomu ulizobana kwenye nguo, na meseji za wasichana wachuo.../

ulimkuta mwema ukamteka kiakili, ukamshawishi mpaka akakupa shehena ya mwili.../

akakupa moyo akihisi utaweka nadhiri, ukajisahau na ukamuonesha asili...ya kwamba we ni mchafu tu/

kipi unaropoka lakini, ubaya ulipwa wa ubaya unachokonda ni nini.../

mmoja ametupa mwingine ameokota yamkini, aliyetupa ni wewe na niliyeokota ni mimi.../

aah ilikua ni sababu ya msongo wa mawazo, na ndio maana uliona wife sio wamoto kama mwanzo.../

aliteseka kiasi akahisi ndoa ni sumu, na nikaamua kuchukua maamuzi magumu...dongo kwako/

nilimuokoa nikamvusha bahari, maana muungwana vitendo maneno hayata angusha jabali.../

siku mwili hautagusa sayari, utamkumbuka na pengine utajifunza kujali.../

mpunga umeyumba umeanza kujishuku mzee, umerudi nyumbani baada ya kushindwa kumudu starehe.../

haukuwepo kwenye shida ilipofuzu tarehe, ulikimbia na nilikuwepo mimi pekee.../

ngoja nikuudhi unajua mwanao ananiita daddy, nampeleka shule namrudisha nyumbani baada ya kazi.../

nalipa ada, ada usizokumbuka kutoa,, mwanao amefikia balehe nimemfunza kunyoa.../

nimemfunza ushairi nimemfunza kufanya mahesabu, nimemfunza kufunga tai kisha kamba za viatu.../

nimemfuza sheria zinazoongelewa bungeni, na nilienda kumtetea alipoonewa shuleni.../

una hoja yeyote defensively, maana hujui ka wanalala ama wanaamka safely.../

hujui kuhusu family dinner women day birthday zao hujui hata anniversary.../

Hujui kuhusu maumivu aliyopata moyoni, hujui harufu ya chakula alichopasha jikoni.../

hujui kuhusu depression, maana mara mbili nimemkuta amejifunga kamba shingoni.../

Credits: dizasta vina _ kikaoni
 
Nampenda yeye amenifanya nipate ishara, amenipa counselling amenifanya niache sigara.../

Anajua chakula nikipendacho timu niipendayo kinywaji anajua even my favorite color.../

Wenzio tunatafuta familia ili tujenge wewe yako ni nini, mkeo amesaliti ndoa sababu yake ni upweke sababu yako ni nini.../

You know what they say men what goes around comes around yeah thats true, so i wonder why you changed you used to be a good man what happened to you.../

Nakili mbele za watu nilishiriki hii dhambi, uvungu wa moyo wangu unasema usaliti ni haki.../

Nyanyua kisu chako uniue ila naomba uelewe, sijaivunja ndoa yako umeivunja ndoa yako mwenyewe.../

Credits: dizasta vina
 
Najua wengi ni mashabiki wa wasanii fulani fulani wa mziki pendwa wa hip hop ila leo nataka tuangazie kidogo hawa ma underground hip hop.

Katika tansina ya muziki huu wa hip hop tunaona jinsi gani evolution ilivyobadili ladha ya mziki huu kiasi cha wasanii kuimba nyimbo ambazo hazina lyrical wala critical.

List yangu ni hii hapa na wewe unaweza kuweka yako.

1. Dizasta vina
2. Nala mzalendo
3. Kadgo
4. Boshoo ninja
5. Kinya mistari
6. Shaolin senetor
7. Mbeya boy chuma
8. Hamis mistari
9. Ado gado
10. Nyenza MC

Wapo wengi ila kwasasa nianze na hao halafu chini nitanukuu mistari yao katika baadhi ya nyimbo zao
Mbeya boy chuma , yupo vizuri saana
 
Back
Top Bottom