Hamisi mistari
Wanasema ukipenda hauoni, japo unamacho umewekewa usoni.../
Mbele yangu mwema unanitenda kisogoni, napata hasira zaidi ya mtu aliyetenda wema halafu anaenda motoni.../
Skia hapa mtaani unavijana wangapi, nilikuta meseji tukutane sijui mlikutana saa ngapi.../
Au ndio wale hawapo wcb ila wanajiita wasafi, unaniacha mimi unaenda kuwafata walafi.../
Tukiwa pamoja hauna hata ile stimu, una mambo mengi yani upo bize na simu.../
Kama ni mwili basi unauza lejaleja, kila mtu ana namba yako zaidi ya wahudumu kwa wateja.../
Kumbuka juzi tulilala ukajitoa kifuani, baada ya simu kupigwa ukajiondoa chumbani.../
Unavyofanya hivyo unahisi unamkomoa nani, jamaa yako anajiita sudi mi nisha muondoa duniani.../
Yaani sijamaanisha kukupa talaka, ila namaanisha kukupa walaka.../
Upendo wangu kwako najikuta nadata, yani mpagani huna dini halafu nakupa sadaka.../
Unajiona mjanja yani unajikuta wasasa, mwisho wako upo utajikuta umenasa.../
Siku narudi home nakuta kundi la watu, wadada wembamba mithili ya kundi la wafu.../
Walikusuta unatembea na wanaume za watu, acha hiyo walikubaka ulikunywa pomne za watu.../
Usidhani kwamba nilikua nazikosa tetesi, unatangaza nakibamia we u ajipoza fenesi.../
Haukua mzito nilikuona mwepesi, siku nashughulika kitandani we unasoma gazeti.../
Song: nashindwa