Hiroo Onoda: Askari wa Kijapan aliyeendelea kupigana WW2 kwa miaka 29 baada ya vita kuisha

Hiroo Onoda: Askari wa Kijapan aliyeendelea kupigana WW2 kwa miaka 29 baada ya vita kuisha

Bwana Mkubwa9

Member
Joined
Oct 15, 2016
Posts
61
Reaction score
182
Hiroo-Onoda.png.jpg

Wakati mwaka 1944 ukiwa unaelekea tamati, hii ni baada ya miaka zaidi ya saba ya vita, mambo yalikuwa yanaiendea kombo Japan.⁣⁣⁣

Uchumi wake ulikuwa umeharibika vibaya, jeshi lake lilikuwa limetapakaa karibia kila kona ya Asia bila kuwa na mfumo thabiti wa kimawasiliano na mipaka iliyokuwa inamiliki ilikuwa inachukuliwa na majeshi ya USA kwa kasi ya ajabu kama moto wa nyika.⁣⁣⁣⁣

Kupoteza vita ilikuwa haizuiliki.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Tarehe 26 December 1944 maafisa wa kijeshi wa Japan waliamua kufanya jaribio la mwisho kabisa la kimkakati kuinusuru Japan kudondokea kwenye mikono ya Marekani.⁣⁣⁣⁣

Luteni Usu(Second Lieutenant) Hiroo Onoda alipewa kikosi kwenda katika kisiwa cha Lubang nchini Ufilipino.⁣⁣⁣⁣
Onoda ndio alikuwa kamanda wa kikosi na alipewa amri mbili.⁣⁣⁣⁣

Amri ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha kwamba majeshi ya Marekani hayavuki kisiwa cha Lubang na kuzidi kusonga mbele huku amri ya pili ilikuwa ni apambane kwa gharama yoyote ile na KAMWE asisalimu amri.⁣⁣⁣⁣ Aliambiwa kama kikitokea chochote basi atataarifiwa kwa kufuatwa.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Hiroo Onoda na kamanda wake aliyempa amri walikuwa wanajua kabisa kwamba hii ilikuwa ni mission ya kujitoa muhanga. Nafasi ya kushinda vita ilikuwa ni ndogo kuliko punje ya haradari⁣⁣⁣⁣. Ilikuwa ni kuwatoa kafara maaskari kwa ajili ya taifa lao.⁣⁣⁣⁣ Lakini hakukuwa na namna maana hayo ndiyo maisha ya askari,kufa au kupona kwa ajili ya nchi yako.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Kwa kawaida amri za kijeshi huwa zinapokelewa bila maswali wala kusitasita.⁣⁣⁣⁣ Onoda pamoja na kikosi chake wakapanda meli hadi Lubang na kuanza kazi ya kukilinda kisiwa kwa uvamizi wa Marekani na majeshi ya washirika (Allied).⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Kama ilivyotazamiwa,majeshi ya Marekani hayakukawia sana kuwasili kisiwani Lubang,yalimkuta Luteni Usu Onoda na maaskari wake na yaliwasambaratisha kiurahisi sana.⁣⁣⁣⁣ Ndani ya siku mbili tu askari wengi wa kijapan aidha walipoteza maisha, au walijisalimisha.⁣⁣⁣⁣ Lakini Onoda pamoja na askari wake watiifu watatu walifanikiwa kujificha msituni na wakaanza vita ya msituni ya mashambulizi ya kuvizia(guerilla) dhidi ya maaskari wa Kimarekani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mwezi August mwaka 1945 USA walidondosha mabomu hatari ya nyuklia katika miji ya Hiroshima na Nagasaki na tukio hilo lilikuwa ndiyo mwisho wa vita kubwa zaidi katika historia ya binadamu.⁣⁣⁣⁣ Taifa la Japan lilikubali yaishe wakatangaza wameshindwa vita.⁣⁣⁣⁣ Wakati Japan wamekubali kushindwa na kuwataka maaskari wake wote waliokuwa wametapakaa maeneo tofauti katika bara la Asia kurudi nyumbani haraka,maaskari hao wengi kama ilivyokuwa kwa Onoda hawakuwa na taarifa.⁣⁣⁣⁣ Wao waliendeleza mapambano msituni.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Maaskari hawa wa Kijapan wasiokuwa na taarifa za kumalizika kwa vita walikuwa tishio kubwa la kiusalama kwenye nchi za Mashariki ya mbali.Walikuwa wanashambulia maaskari wa Kimarekani,wananchi wa maeneo husika na Polisi.⁣⁣⁣⁣
Serikali za nchi hizo kwa kushirikiana na Marekani waliamua kufanya jambo.⁣⁣⁣⁣ Wakadondosha vipeperushi vingi kwa ndege ambavyo vilikuwa na ujumbe wa kuwataarifu maaskari kwamba vita imemalizika warejee nyumbani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Wanajeshi wengi akiwemo Onoda walivisoma vipeperushi lakini tofauti na wengi Onoda alivipuuza na akasema ni uongo wa Marekani kutaka kuwakamata kiurahisi.⁣⁣⁣⁣ Mwanaume akaendelea kupambana msituni akiwa na wenzake watatu.⁣⁣⁣⁣ Kila wakimuona askari wa kimarekani anakula shaba halafu wanakimbia mafichoni.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Hatimaye miaka mitano ikapita,majeshi ya Marekani yakaondoka Lubang lakini wajuba bado wakawa msituni wanashambulia raia wanaofanya shughuli za kilimo na uvuvi msituni,wanaiba mifugo na kuchoma moto mazao.⁣⁣⁣⁣
Hapa serikali ya Ufilipino ikaingilia kati tena.⁣⁣⁣⁣ Wakadondosha vipeperushi vinavyosomeka kwa lugha ya Kijapan "Vita imemalizika na mmeshindwa. Jitiokezeni mrudi nyumbani."⁣⁣⁣⁣ Onoda na wenzake wakavisoma na kuvichoma moto vile vipeperushi wakiamini tena ule ni mtego wa Marekani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mwaka 1952 serikali ya Japan ikajaribu kuchukua hatua ya mwisho kuwarudisha askari wake nyumbani.⁣⁣⁣⁣ Wakadondosha picha za askari waliopotea na barua kutoka kwa familia zao zikiwa na salamu kutoka kwa mtawala wa Japan.⁣⁣⁣⁣ Bado Onoda na wenzae wakaona wanategwa ili wanase.⁣⁣⁣⁣ Onoda akakataa kujitokeza na akaendeza vita akiamini ni uzushi wa Marekani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mpaka mwaka 1972 Hiroo Onoda alikuwa amebaki peke yake msituni akiendelea kutekeleza amri aliyopewa na kamanda wake.⁣⁣⁣⁣ Wenzake wawili walikuwa wameshauawa na wanachi wa maeneo ya jirani huku mmoja akijisalimisha.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Taarifa juu ya kifo cha miongoni mwa makamanda wake aliyeitwa Kozuka kilichotokea mwaka huo wa 1972 zilileta taharuki kubwa sana nchini Japan na watu wakaanza kuamini kwamba huenda hata Onoda bado yupo hai huko msituni.⁣⁣⁣⁣
Ikawa habari kubwa sana nchini Japan kwamba kuna uwezekano kukawa na askari wa mwisho wa Kijapan ambaye haelewi kama vita kuu imemalizika na anaendelea kupigana baada ya miaka 23 ya vita kuisha!⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Vyombo vya habari vililikuza sana jambo hili kiasi kwamba shauku ya kutaka kumuona Onoda anarudi Japan ikawa kubwa.⁣⁣⁣⁣ Japan na Ufilipino zikatuma vikosi vya watafutaji wazoefu wa misitu kumsaka huyu kamanda lakini hawakuambulia kitu!⁣⁣⁣⁣ Ilikuwa ni katika kipindi hiki ndipo kijana mmoja mdogo mpanda milima na mpenda matembezi ya misituni(adventurer and explorer) aliyeitwa Norio Suzuki alipata kusikia hadithi za Hiroo Onoda kwa mara ya kwanza.⁣⁣⁣⁣

Akajiwekea ahadi kwamba atakwenda Ufilipino na atampata Hiroo Onoda misituni kisha atamrudisha Japan.⁣⁣⁣⁣ Bwana mdogo huyu alizaliwa katika nyakati ambazo vita ilikuwa imeisha na aliamua kuacha shule ili awe mpanda milima na mtembezi wa misituni.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Norio Suzuki alipotangaza kwamba atakwenda Lubang kumtafuta na kumleta Hiroo Onoda watu wengi walimcheka na kumdhihaki kwamba ana matatizo ya akili.⁣⁣⁣⁣ Lakini alipofika Lubang alitumia siku nne tu ndani ya msitu kabla hajampata bwana Onoda.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mtu aliyetafutwa kwa miaka karibia 30 na maaskari wa Marekani,Japan na Ufilipino bila mafanikio leo kijana mmoja asiye na silaha wala mafunzo yoyote ya kutafuta watu misituni anampata tena haraka!⁣⁣⁣⁣ ⁣⁣Onoda alimwamini Suzuki kwasababu alikuwa anamtafuta kwa kupiga kelele na alielezea alimuona anavyohangaika tangu siku ya kwanza alipofika msituni.⁣⁣⁣⁣
Walikaa pamoja kwa siku kadhaa na wakapiga picha wakiwa pamoja (Pichani)⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Ajabu ni kwamba bado Onoda alikataa kurudi Japan!⁣⁣⁣⁣ Alimwagiza Suzuki ampe taarifa mfalme atume askari wakampe taarifa kwamba ni kweli vita imemalizika la sivyo ataendelea kupambana na hatorudi wala kusalimu amri!⁣⁣⁣⁣ Norio Suzuki aliporudi Japan na kueneza hizo habari pamoja na picha alizopiga kule msituni Lubang watu walistaajabu sana.⁣⁣⁣⁣ Mfalme alilazimika kumrejesha kazini kamanda aliyempa amri Onoda ya kwenda Lubang na kisha kumtuma mpaka huko ili akampe amri ya kurejea nyumbani Luteni Usu Hiroo Onoda.⁣⁣⁣⁣

Baada ya kamanda wake kufika huko mafichoni kwa msaada wa Suzuki alimsomea amri mpya mbili.⁣⁣⁣⁣
Moja ni ya kusitisha mapigano na mbili ni kurejea Japan haraka.⁣⁣⁣⁣ Akamwambia hizo ni amri za mfalme Hirohinto.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣Luteni Usu Hiroo Onoda alipiga saluti kama inshara ya kupokea amri na alikubali kurejea rasmi nchini kwao Japan.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Huyo ndiyo Hiroo Onoda.⁣⁣⁣⁣ Mwamba wa Kijapan!!⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Aliporudi Japan alipokelewa kama shujaa na alikuwa maarufu sana.⁣⁣⁣⁣ Alikuwa anatembelewa ma watu wengi maarufu kutaka kupiga nae picha na wanahabari walikuwa wanafurika nyumbani kwake kutaka mahojiano naye.⁣⁣⁣⁣ Maisha haya mapya hakuyapenda.⁣⁣⁣⁣

Na alikiri baadaye kwamba Wajapan wamebadilika sana,wameacha mila na tamaduni zao halisi za Kijapan ambazo wao walizipigania miaka yote na zilifanya Japan kuwa taifa lenye kuheshimika.⁣⁣⁣⁣ Alioa na akaanza maisha ya ufugaji na kilimo lakini baadaye aliamua kuhamia nchini Brazil.⁣⁣⁣⁣ Mara kadhaa alirejea Lubang na alitoa misaada kwa wanakijiji ambao aliwahi kuua ndugu wa familia zao au kuharibu mazao yao.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
⁣⁣⁣⁣Baadae alipoulizwa kwanini ulipigana vita muda wote huo? Alijibu kiurahisi tu "Ile ilikuwa ni amri! Pambana kwa namna yoyote ile na kamwe usisalimu amri."⁣⁣⁣⁣ Alielezea kwamba kwa askari wa Kijapan kushindwa vita huku ukiwa hai ni kitu kisichowezekana.⁣⁣⁣⁣ Unatakiwa ushindwe vita ukiwa tayari maiti.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Itikadi ya namna hii ndiyo ilifanya maaskari wengi wa jeshi la Kijapan kuendelea kubaki msituni hata baada ya taifa lao kutangaza kwamba wameshindwa vita.⁣⁣⁣⁣ Wapo walioamini ni uongo kwani Japan haiwezi kushindwa vita.⁣⁣⁣⁣ Pia wapo walioamini ni kweli wameshindwa lakini wao kama maaskari hawawezi kuhimili aibu ya kupoteza vita hivyo ni bora waendelee kupigana vita.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
*****************⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Hii ni kama hadhithi ya mtu mjinga lakini kila mtu huwa na kitu anachokipenda katika maisha.⁣⁣⁣ Kinachotutofautisha ni kiasi cha upendo wetu juu ya hicho kitu.⁣⁣⁣⁣

Unajitoa kiasi gani juu ya unachokipenda?⁣⁣⁣⁣
Unajitoa kiasi gani juu ya unachokiamini?⁣⁣⁣⁣
Unaipenda biashara yako?⁣⁣⁣⁣
Upo tayari kujitolea kitu gani ili uifikishe unapotaka?⁣⁣⁣⁣
Unaipenda kazi yako?⁣⁣⁣⁣
Unaweza kujitoa kiasi gani kwa ajili ya kazi yako?⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Mwenzetu Onoda alijitoa kwa ajili ya nchi yake, alikuwa mkweli na mzalendo halisi kwa taifa lake.⁣⁣⁣⁣ Historia ya Japan inamkumbuka kama miongoni mwa mashujaaa wa taifa lao.⁣⁣⁣⁣ Je, kazi yako na biashara yako itakukumbuka kwa lipi?⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
"FIND SOMETHING WORTH ENOUGH DYING FOR"⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
@Shebinovic⁣⁣⁣⁣
0755573178⁣⁣⁣⁣
 
Miaka 23 anapigana vita alikuwa na kontena la risasi au?.... au miaka 23 alikuwa amejificha msituni?
Amepambana kwa muda wa miaka 29. Chief unaniangusha, vita sio risasi pekee. Pia kumbuka Wajapan ndio naweza kusema katika watu waliopigana vita nyingi sana pia ni utamaduni wao kutumia Panga sio risasi pekee.

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
 
Miaka 23 anapigana vita alikuwa na kontena la risasi au? Au miaka 23 alikuwa amejificha msituni?
Ni kweli kabisa mkuu.
Risasi na silaha nyingine alizipata kwa kuwaua maaskari waliokuwa wanapita kufanya doria.

Kwenye medani za kivita hata kama hupigani lakini ukiwa haujaripoti kwa waliokupa amri ya kupigana wakati vita imemalizika na hakuna taarifa za uhakika kuhusu kifo chako basi unahesababika bado upo vitani.
 
Mkmi pia nimeshangaa mkuu!!! Au labda pengine alikuwa anatumia mawe badala ya risasi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa vitani haulazimiki kuwa kwenye mapigano muda wote.
Hawa maaskari wa Kijapan walioendelea kupigana baada ya vita ya pili ya dunia siyo kwamba muda wote walikuwa wanapigana.

Muda mwingi waliutumia kujificha na kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa maaskari wa Kimarekani kabla hawajaondoka Asia,Maaskari wa nchi za Asia au hata wananchi wa vijiji vya pembezoni mwa misitu waliyojificha.
Kijeshi hao bado wanakuwa wapo vitani na wanaweza wanaua wakilazimika kufanya hivyo. Kusalimu amri huwa siyo jambo la mara moja.

Wakuu wa majeshi wakitangaza vita imemalizika taarifa huanza kutumwa kwa wakuu wa vikosi vyao ambavyo vipo deployed maeneo tofauti tofauti.

Hao wakuu wa vikosi nao huanza kutuma taarifa kwa vikundi vidogo vidogo kusitisha mapigano. Wapo ambao hukiuka makusudi au kutoiamini taarifa hivyo huendelea na vita.

Hiroo Onoda na wenzake baada ya kupigwa kikosi chake kilikosa mawasiliano ya moja kwa moja na makao makuu ya jeshi la Japan. Ndiyo maana alikataa kuamini taarifa yoyote ya kusimama kwa vita. Ku-demobilize jeshi lilipo vitani ni process ambayo sio ya mara moja.
 
Back
Top Bottom