Hiroo Onoda: Askari wa Kijapan aliyeendelea kupigana WW2 kwa miaka 29 baada ya vita kuisha

Hiroo Onoda: Askari wa Kijapan aliyeendelea kupigana WW2 kwa miaka 29 baada ya vita kuisha

huyu jamaa alipew oda akae huko huko sasa mpaka vita inaisha hakujua.alikua ana surviving skills zote za pori.na hakuweka silaha chin mpaka amri ilviotoka kwa emperor hikito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnamo Desemba mwaka 1944, moja ya miezi ya mwisho ya Vita vya Pili vya Dunia, Meja Jenerali Gute wa Japani aliyeitwa Hiroo Onoda alihamishiwa Lubang, kisiwa kidogo huko Ufilipino.
Wiki chache baada ya kuwasili, wapiganaji wa Japan waliokimbia mashambulizi ya Marekani walikimbilia msituni.
Lakini tofauti na marafiki zake wengi, Onoda amekuwa akijificha kwenye kisiwa cha Japan kwa miaka 30.
Serikali ya Japani ilitangaza kwamba Onoda alikufa mwaka wa 1959, lakini alikuwa hai na akifanya kazi ya siri iliyopewa jukumu la kulinda kisiwa hicho hadi askari warudi.
Aliporudi Japani mnamo mwaka 1974, Onoda alikaribishwa kama shujaa mwingine yeyote wa Japani.
Alikuwa mwanajeshi wa mwisho wa Japani kurudi katika nchi yake baada ya vita.
Shajara yake, iliyochapishwa muda mfupi baadaye, ikawa kitabu kilichouzwa zaidi.
Katika mahojiano na nakala baada ya kurejea Japan, Onoda alisema hakukubali kwamba Japan ilikuwa imepoteza vita.
Watu wengi nje ya Japani wanaona hadithi ya Onoda ya kushangaza.
Lakini mfalme wa Japani aliona matendo yake kuwa yenye mantiki.
Onoda aliapa kutojisalimisha na kufariki kwa ajili ya mfalme wake, lakini hilo halikufanyika.
Katika operesheni, Onoda ilikuwa aharibu njia ya ndege katika bandari ya Lubang, lakini ilishindikana, na wakati majeshi ya adui yalipochukua udhibiti wa kisiwa hicho, yeye na wenzake walikimbilia msituni.
Mapigano hayo yaliisha muda mfupi baadaye, lakini Onoda na wengine watatu walibaki msituni na hawakuamini habari hiyo, wakidhania kuwa karatasi zilizotupwa Lubang zilikuwa uzushi tu.
Waliendelea kujificha porini huku wakiwa wamezungukwa na nyoka na mchwa wakijilisha ndizi, nazi na wali walioiba ili waendelee kuishi, wakiamini kwamba adui alidhani wamekufa.
Onoda aliandika katika kumbukumbu zake kwamba mwaka wa 1959 yeye na rafiki yake Kinshichi Kozuka ‘’walikuwa na mawazo kiasi kwamba hatukuweza kuelewa chochote ambacho hakikuwafaa.’’
Hatimaye Kozuka alipigwa risasi na kuuawa na polisi wa eneo hilo mnamo Oktoba mwaka 1972, lakini Onoda alibaki peke yake katika kisiwa hicho na kubaki huko kwa miezi 18, hadi alipokutana na mvumbuzi wa Kijapani Norio Suzuki.
Mnamo Agosti 15, 1945, Mfalme wa Japani, Hirohito, alifanya jambo ambalo hakuna mfalme mwingine aliyekuwa amefanya.
Aliambia redio kwamba silaha za atomiki zimeharibiwa huko Hiroshima na Nagasaki.
Siku ya mlipuko wa pili wa bomu la atomiki huko Japani, Joseph Stalin alitangaza vita dhidi ya Japani.
Mara moja, askari wa Soviet walifika Manchuria.
Baada ya majuma machache walifika kwenye kisiwa cha kaskazini cha Hokkaido.
Mfalme Hirohito wa Japani alikubali kwamba kujisalimisha kwa Marekani ndilo chaguo pekee lililokuwa wazi kwake.
Operesheni ya Suzuki ilifanikiwa na vita vya Onoda vilimalizika mnamo Machi 9, 1974.
Picha: Hiroo Onoda, ambaye alitoka katika msitu wa Lubang mwaka wa 1974, ambako alikuwa amejificha kwa miaka 30.
Muungano ulioshinda Vita vya Pili vya Dunia uliwafungulia mashitaka watu 28, wakiwemo wanachama wa uongozi wa Vita vya Pili vya Dunia huko Japan, maafisa saba, akiwemo Waziri Mkuu wa Japan Hideki Tojo, walinyongwa.
Hata hivyo, wapo pia maafisa wengine ambao hawajafunguliwa mashitaka, akiwemo mrithi Yasuhiko Asaka, mpwa wa Mfalme wa Japani, pamoja na afisa aliyeongoza jeshi la Japan katika ubakaji wa kikatili katika mji mkuu wa China, Nanjing.
MacArthur anawachukulia maafisa hao kutofunguliwa mashitaka kama hatua ya lazima.
Mtu mwingine ambaye alitoroka mashtaka alikuwa Nobusuke Kishi.
Kufuatia kifo cha Hiroo Onoda mnamo mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 91, msemaji wa Waziri Mkuu Abe alielezea rambirambi zake nyingi.
Msemaji huyo hakuzungumzia madhara yaliyosababishwa na vita pekee bali hata mauaji ya watu katika vijiji vya Ufilipino baada ya Japan kujisalimisha.
 
Wajapani wa miaka hiyo walikua hatari na wababe hawa wa miaka hii Wanamuogopa Hadi N Korea
 

Wakati mwaka 1944 ukiwa unaelekea tamati, hii ni baada ya miaka zaidi ya saba ya vita, mambo yalikuwa yanaiendea kombo Japan.⁣⁣⁣

Uchumi wake ulikuwa umeharibika vibaya, jeshi lake lilikuwa limetapakaa karibia kila kona ya Asia bila kuwa na mfumo thabiti wa kimawasiliano na mipaka iliyokuwa inamiliki ilikuwa inachukuliwa na majeshi ya USA kwa kasi ya ajabu kama moto wa nyika.⁣⁣⁣⁣

Kupoteza vita ilikuwa haizuiliki.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Tarehe 26 December 1944 maafisa wa kijeshi wa Japan waliamua kufanya jaribio la mwisho kabisa la kimkakati kuinusuru Japan kudondokea kwenye mikono ya Marekani.⁣⁣⁣⁣

Luteni Usu(Second Lieutenant) Hiroo Onoda alipewa kikosi kwenda katika kisiwa cha Lubang nchini Ufilipino.⁣⁣⁣⁣
Onoda ndio alikuwa kamanda wa kikosi na alipewa amri mbili.⁣⁣⁣⁣

Amri ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha kwamba majeshi ya Marekani hayavuki kisiwa cha Lubang na kuzidi kusonga mbele huku amri ya pili ilikuwa ni apambane kwa gharama yoyote ile na KAMWE asisalimu amri.⁣⁣⁣⁣ Aliambiwa kama kikitokea chochote basi atataarifiwa kwa kufuatwa.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Hiroo Onoda na kamanda wake aliyempa amri walikuwa wanajua kabisa kwamba hii ilikuwa ni mission ya kujitoa muhanga. Nafasi ya kushinda vita ilikuwa ni ndogo kuliko punje ya haradari⁣⁣⁣⁣. Ilikuwa ni kuwatoa kafara maaskari kwa ajili ya taifa lao.⁣⁣⁣⁣ Lakini hakukuwa na namna maana hayo ndiyo maisha ya askari,kufa au kupona kwa ajili ya nchi yako.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Kwa kawaida amri za kijeshi huwa zinapokelewa bila maswali wala kusitasita.⁣⁣⁣⁣ Onoda pamoja na kikosi chake wakapanda meli hadi Lubang na kuanza kazi ya kukilinda kisiwa kwa uvamizi wa Marekani na majeshi ya washirika (Allied).⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Kama ilivyotazamiwa,majeshi ya Marekani hayakukawia sana kuwasili kisiwani Lubang,yalimkuta Luteni Usu Onoda na maaskari wake na yaliwasambaratisha kiurahisi sana.⁣⁣⁣⁣ Ndani ya siku mbili tu askari wengi wa kijapan aidha walipoteza maisha, au walijisalimisha.⁣⁣⁣⁣ Lakini Onoda pamoja na askari wake watiifu watatu walifanikiwa kujificha msituni na wakaanza vita ya msituni ya mashambulizi ya kuvizia(guerilla) dhidi ya maaskari wa Kimarekani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mwezi August mwaka 1945 USA walidondosha mabomu hatari ya nyuklia katika miji ya Hiroshima na Nagasaki na tukio hilo lilikuwa ndiyo mwisho wa vita kubwa zaidi katika historia ya binadamu.⁣⁣⁣⁣ Taifa la Japan lilikubali yaishe wakatangaza wameshindwa vita.⁣⁣⁣⁣ Wakati Japan wamekubali kushindwa na kuwataka maaskari wake wote waliokuwa wametapakaa maeneo tofauti katika bara la Asia kurudi nyumbani haraka,maaskari hao wengi kama ilivyokuwa kwa Onoda hawakuwa na taarifa.⁣⁣⁣⁣ Wao waliendeleza mapambano msituni.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Maaskari hawa wa Kijapan wasiokuwa na taarifa za kumalizika kwa vita walikuwa tishio kubwa la kiusalama kwenye nchi za Mashariki ya mbali.Walikuwa wanashambulia maaskari wa Kimarekani,wananchi wa maeneo husika na Polisi.⁣⁣⁣⁣
Serikali za nchi hizo kwa kushirikiana na Marekani waliamua kufanya jambo.⁣⁣⁣⁣ Wakadondosha vipeperushi vingi kwa ndege ambavyo vilikuwa na ujumbe wa kuwataarifu maaskari kwamba vita imemalizika warejee nyumbani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Wanajeshi wengi akiwemo Onoda walivisoma vipeperushi lakini tofauti na wengi Onoda alivipuuza na akasema ni uongo wa Marekani kutaka kuwakamata kiurahisi.⁣⁣⁣⁣ Mwanaume akaendelea kupambana msituni akiwa na wenzake watatu.⁣⁣⁣⁣ Kila wakimuona askari wa kimarekani anakula shaba halafu wanakimbia mafichoni.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Hatimaye miaka mitano ikapita,majeshi ya Marekani yakaondoka Lubang lakini wajuba bado wakawa msituni wanashambulia raia wanaofanya shughuli za kilimo na uvuvi msituni,wanaiba mifugo na kuchoma moto mazao.⁣⁣⁣⁣
Hapa serikali ya Ufilipino ikaingilia kati tena.⁣⁣⁣⁣ Wakadondosha vipeperushi vinavyosomeka kwa lugha ya Kijapan "Vita imemalizika na mmeshindwa. Jitiokezeni mrudi nyumbani."⁣⁣⁣⁣ Onoda na wenzake wakavisoma na kuvichoma moto vile vipeperushi wakiamini tena ule ni mtego wa Marekani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mwaka 1952 serikali ya Japan ikajaribu kuchukua hatua ya mwisho kuwarudisha askari wake nyumbani.⁣⁣⁣⁣ Wakadondosha picha za askari waliopotea na barua kutoka kwa familia zao zikiwa na salamu kutoka kwa mtawala wa Japan.⁣⁣⁣⁣ Bado Onoda na wenzae wakaona wanategwa ili wanase.⁣⁣⁣⁣ Onoda akakataa kujitokeza na akaendeza vita akiamini ni uzushi wa Marekani.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mpaka mwaka 1972 Hiroo Onoda alikuwa amebaki peke yake msituni akiendelea kutekeleza amri aliyopewa na kamanda wake.⁣⁣⁣⁣ Wenzake wawili walikuwa wameshauawa na wanachi wa maeneo ya jirani huku mmoja akijisalimisha.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Taarifa juu ya kifo cha miongoni mwa makamanda wake aliyeitwa Kozuka kilichotokea mwaka huo wa 1972 zilileta taharuki kubwa sana nchini Japan na watu wakaanza kuamini kwamba huenda hata Onoda bado yupo hai huko msituni.⁣⁣⁣⁣
Ikawa habari kubwa sana nchini Japan kwamba kuna uwezekano kukawa na askari wa mwisho wa Kijapan ambaye haelewi kama vita kuu imemalizika na anaendelea kupigana baada ya miaka 23 ya vita kuisha!⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Vyombo vya habari vililikuza sana jambo hili kiasi kwamba shauku ya kutaka kumuona Onoda anarudi Japan ikawa kubwa.⁣⁣⁣⁣ Japan na Ufilipino zikatuma vikosi vya watafutaji wazoefu wa misitu kumsaka huyu kamanda lakini hawakuambulia kitu!⁣⁣⁣⁣ Ilikuwa ni katika kipindi hiki ndipo kijana mmoja mdogo mpanda milima na mpenda matembezi ya misituni(adventurer and explorer) aliyeitwa Norio Suzuki alipata kusikia hadithi za Hiroo Onoda kwa mara ya kwanza.⁣⁣⁣⁣

Akajiwekea ahadi kwamba atakwenda Ufilipino na atampata Hiroo Onoda misituni kisha atamrudisha Japan.⁣⁣⁣⁣ Bwana mdogo huyu alizaliwa katika nyakati ambazo vita ilikuwa imeisha na aliamua kuacha shule ili awe mpanda milima na mtembezi wa misituni.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Norio Suzuki alipotangaza kwamba atakwenda Lubang kumtafuta na kumleta Hiroo Onoda watu wengi walimcheka na kumdhihaki kwamba ana matatizo ya akili.⁣⁣⁣⁣ Lakini alipofika Lubang alitumia siku nne tu ndani ya msitu kabla hajampata bwana Onoda.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Mtu aliyetafutwa kwa miaka karibia 30 na maaskari wa Marekani,Japan na Ufilipino bila mafanikio leo kijana mmoja asiye na silaha wala mafunzo yoyote ya kutafuta watu misituni anampata tena haraka!⁣⁣⁣⁣ ⁣⁣Onoda alimwamini Suzuki kwasababu alikuwa anamtafuta kwa kupiga kelele na alielezea alimuona anavyohangaika tangu siku ya kwanza alipofika msituni.⁣⁣⁣⁣
Walikaa pamoja kwa siku kadhaa na wakapiga picha wakiwa pamoja (Pichani)⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Ajabu ni kwamba bado Onoda alikataa kurudi Japan!⁣⁣⁣⁣ Alimwagiza Suzuki ampe taarifa mfalme atume askari wakampe taarifa kwamba ni kweli vita imemalizika la sivyo ataendelea kupambana na hatorudi wala kusalimu amri!⁣⁣⁣⁣ Norio Suzuki aliporudi Japan na kueneza hizo habari pamoja na picha alizopiga kule msituni Lubang watu walistaajabu sana.⁣⁣⁣⁣ Mfalme alilazimika kumrejesha kazini kamanda aliyempa amri Onoda ya kwenda Lubang na kisha kumtuma mpaka huko ili akampe amri ya kurejea nyumbani Luteni Usu Hiroo Onoda.⁣⁣⁣⁣

Baada ya kamanda wake kufika huko mafichoni kwa msaada wa Suzuki alimsomea amri mpya mbili.⁣⁣⁣⁣
Moja ni ya kusitisha mapigano na mbili ni kurejea Japan haraka.⁣⁣⁣⁣ Akamwambia hizo ni amri za mfalme Hirohinto.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣Luteni Usu Hiroo Onoda alipiga saluti kama inshara ya kupokea amri na alikubali kurejea rasmi nchini kwao Japan.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Huyo ndiyo Hiroo Onoda.⁣⁣⁣⁣ Mwamba wa Kijapan!!⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Aliporudi Japan alipokelewa kama shujaa na alikuwa maarufu sana.⁣⁣⁣⁣ Alikuwa anatembelewa ma watu wengi maarufu kutaka kupiga nae picha na wanahabari walikuwa wanafurika nyumbani kwake kutaka mahojiano naye.⁣⁣⁣⁣ Maisha haya mapya hakuyapenda.⁣⁣⁣⁣

Na alikiri baadaye kwamba Wajapan wamebadilika sana,wameacha mila na tamaduni zao halisi za Kijapan ambazo wao walizipigania miaka yote na zilifanya Japan kuwa taifa lenye kuheshimika.⁣⁣⁣⁣ Alioa na akaanza maisha ya ufugaji na kilimo lakini baadaye aliamua kuhamia nchini Brazil.⁣⁣⁣⁣ Mara kadhaa alirejea Lubang na alitoa misaada kwa wanakijiji ambao aliwahi kuua ndugu wa familia zao au kuharibu mazao yao.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
⁣⁣⁣⁣Baadae alipoulizwa kwanini ulipigana vita muda wote huo? Alijibu kiurahisi tu "Ile ilikuwa ni amri! Pambana kwa namna yoyote ile na kamwe usisalimu amri."⁣⁣⁣⁣ Alielezea kwamba kwa askari wa Kijapan kushindwa vita huku ukiwa hai ni kitu kisichowezekana.⁣⁣⁣⁣ Unatakiwa ushindwe vita ukiwa tayari maiti.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣
Itikadi ya namna hii ndiyo ilifanya maaskari wengi wa jeshi la Kijapan kuendelea kubaki msituni hata baada ya taifa lao kutangaza kwamba wameshindwa vita.⁣⁣⁣⁣ Wapo walioamini ni uongo kwani Japan haiwezi kushindwa vita.⁣⁣⁣⁣ Pia wapo walioamini ni kweli wameshindwa lakini wao kama maaskari hawawezi kuhimili aibu ya kupoteza vita hivyo ni bora waendelee kupigana vita.⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
*****************⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Hii ni kama hadhithi ya mtu mjinga lakini kila mtu huwa na kitu anachokipenda katika maisha.⁣⁣⁣ Kinachotutofautisha ni kiasi cha upendo wetu juu ya hicho kitu.⁣⁣⁣⁣

Unajitoa kiasi gani juu ya unachokipenda?⁣⁣⁣⁣
Unajitoa kiasi gani juu ya unachokiamini?⁣⁣⁣⁣
Unaipenda biashara yako?⁣⁣⁣⁣
Upo tayari kujitolea kitu gani ili uifikishe unapotaka?⁣⁣⁣⁣
Unaipenda kazi yako?⁣⁣⁣⁣
Unaweza kujitoa kiasi gani kwa ajili ya kazi yako?⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
Mwenzetu Onoda alijitoa kwa ajili ya nchi yake, alikuwa mkweli na mzalendo halisi kwa taifa lake.⁣⁣⁣⁣ Historia ya Japan inamkumbuka kama miongoni mwa mashujaaa wa taifa lao.⁣⁣⁣⁣ Je, kazi yako na biashara yako itakukumbuka kwa lipi?⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
"FIND SOMETHING WORTH ENOUGH DYING FOR"⁣⁣⁣⁣
⁣⁣⁣⁣
@Shebinovic⁣⁣⁣⁣
0755573178⁣⁣⁣⁣
Baa da ya hapo,Onoda alistaafu akalipwa pesa ndefu.Alienda kuishi Brazil akafungua shamba kubwa La mazao no Mifugo.Baa da ya miaka kadhaa alirudi kule ufilipino kijijini akapeleka zawadi ma misaada ya haja.Mwishowe aliaga dunia kama shujaa was WWII.
 
Picha ipo wapi?
Huyu hapa

Screenshot_20240805_195329_Facebook.jpg
 
Sio Askari wa Tanzania ,baada ya vita ya Kagera baadhi yao waliacha kazi kwa sababu za uongo Mara afya ,Mara kupumzika kumbe waliwaza mtiti ukiibuka tena wanaenda kudanja
 
Back
Top Bottom