Historia fupi ya maisha ya Spika Ndugai aliyoitoa bungeni. Asema alikuwa na maisha ya shida na dhiki

Historia fupi ya maisha ya Spika Ndugai aliyoitoa bungeni. Asema alikuwa na maisha ya shida na dhiki

Sasa kesha kataliwa na wapiga kura wake sijui atakimbilia wapi, au labda agombee kwenye jimbo la magogoni
Pia ilikuwa wajibu wa familia ya Ndugai kutafuta hela ,hakuna aliyezaliwa na hela inatafutwa
 
Leo alikuwa analia lia ,hayo yote aliyoongea ni kutia huruma,sema ndo hivo atarudi tu bungeni kwa ubabe wa CCM jimboni
Sasa kesha kataliwa na wapiga kura wake sijui atakimbilia wapi, au labda agombee kwenye jimbo la magogoni
 
Spika Ndugai amesema haya,

Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza wala kuota kama nitakuwa Mwanasiasa, Mbunge na hata Spika ni Mungu tu ambaye katika uumbaji wake hutujua na kutupangia safari kadri anavyoona ni vyema, asanteni sana wana Kongwa, chama changu na Rais

Nakumbuka miaka niliyosoma Shule ya Msingi nilikuwa natembea Km 16 kwa siku 1, nimekulia maisha ya shida na dhiki, nikiwa mdogo nililala kwenye kitanda cha kamba na nyumba ya tembe, lakini baadaye nimesoma vyuo mbalimbali ndani na hata nje ya nchi

Nilipokuwa chuo cha MWEKA Moshi, nilikuwa mmoja wa Wanafunzi maskini sana, baadhi ya likizo sikuwa na nauli za kurudi Kongwa, nakumbuka jinsi ambavyo wenzangu walivyokuwa wakipanda magari kuondoka mimi nilikuwa najificha kwa aibu ya kuulizwa huna kwenu?

Mimi nyumbani nilikuwa mtoto wa pekee wa Mama yangu, tunapomaliza Bunge hili natamani ni-revenge sasa nirudi akanipokee, lakini bahati mbaya Mungu alishamchukua, kwahiyo wakati mwingine mnisamehe huwa napata hasira ninapokutana na mtu mjinga

Leo nimekuja na rafiki yangu, Mama umenivumilia sana, hata nilipokuwa ICU India alikuwa analala pembeni yangu masaa 24 amekaa kwenye kiti, amekuwa Daktari wangu muda wote, hakika wewe ni mke mwema, kwa kukopa maneno ya Dk Mpango, Asante sana kwa kunipa raha.

Very sad and touching story to tell, na hii vijana wengi tu tumepitia kuna watu Shule tulikua tunawaita Wanubi (Nubians).
Lakini moyoni walitamani sana kurudi makwao kuonana na familia zao. Funzo mnapopata nafasi huku ukubwani kumbukeni mlikotoka na mkumbuke mliopitia kuna watu wanapitia sasa.
Fanyeni kazi kwa kutanguliza utu.
 
Ndugai namkubali kwa ucheshi wake bungeni. pamoja na mabaya ninayoskia kuhusu yeye ila ana sense of humor safi sana, hata ule ubaya unaosikia unafunikwa na ule ucharming wake.
 
Very sad and touching story to tell, na hii vijana wengi tu tumepitia kuna watu Shule tulikua tunawaita Wanubi (Nubians).

Lakini moyoni walitamani sana kurudi makwao kuonana na familia zao. Funzo mnapopata nafasi huku ukubwani kumbukeni mlikotoka na mkumbuke mliopitia kuna watu wanapitia sasa.

Fanyeni kazi kwa kutanguliza utu.
Huyo anajikosha kwa maovu aliyofanya kupitia hicho kiti na pia anatafuta huruma ili jamii imasamehe. Hana lolote.
 
Awamu hii bila kujisifia wewe ni mnyonge/umetoka familia maskini,hutoboi kabisa.
 
Yeye mwenyewe mjinga mjinga tu,sasa historia yake inasaidiaje kukuwa kwa uchumi,jinga kabisa.
 
Amelelewa bila baba?
20200615_163802.jpg
 
Duh aiseeeeeee,, km 16 kwa wiki duh nikama kishiri na buhongwa
 
Back
Top Bottom