Historia fupi ya maisha ya Spika Ndugai aliyoitoa bungeni. Asema alikuwa na maisha ya shida na dhiki

Historia fupi ya maisha ya Spika Ndugai aliyoitoa bungeni. Asema alikuwa na maisha ya shida na dhiki

You are very right , Job ana inferiority complex syndrome , kwa waliosoma Goverment schools enzi hizo tunakumbuka namna watoto wa wafugaji na makabila ya pembezoni namna walivyokuwa wanakuja shule wakiwa wanyonge , mara nyingi walikuwa wanapenda kuwa wenyewe na ilikuwa ni nadra sana kujichanganya na wanafunzi wengine , kwanza hawakua na nguo nzuri zaidi ya sare , hawakua na pocket money , hawakuweza hata kukubaliwa kwenda disco [walikuwa wanachekwa hawajui kuvaaa ] ....na wengi shule zikifungwa walikuwa hawaendi kwao ......serikali ilikuwa ina sera maalum , hawa wengi walikuwa wakienda likizo ilihofiwa hawatarudi .....kwa kweli tumshukuru Mwalimu kwa kuleta usawa kama huo leo watoto waliokua wanyonge wamekua viongozi wakubwa, japo bahati mbaya wamejaa viburi

Nadharia sio lazima kuwa Job anamchukia Freeman bali tu pengine anataka kumuonyesha , maana kwa viwango Freeman alitoka familia ya kitajiri na pengine alikuwa kiongozi wa Starehe au michezo shuleni , watu wengi wajanja wajanja watoto wa dar au mjini walikuwa wana pilika za kuandaa miziki na kutoroka kwenda mjini...na watoto wanyonge kama Job walikuwa wanaonekana washamba na walijiona wanyonge mbele yao ....pengine sasa naye kapata mahali pa kumnyoosha mwenzake ...hata kama ni vyama tofauti huwezi kumfanyia mwenzako namna hiyo ..
Jakaya Kikwete naye alisoma Kibaha ila alikwa mkubwa kwao ...japo kwa viwango vyote yeye alikuwa mjanja mjanja akitokea Tanga School ....na hata walikuwa na urafiki mkubwa na mbowe kutokana na familia yao kuwa na ukumbi wa disco kuanzia Mbowe Club hadi Bilcanas ambapo Kikwete alikuwa mpenzi mkubwa hadi miaka akiwa waziri alikuwa akienda
Wanafunzi kutoka vijiji maskini enzi hizo waliitwa " wazalendo "
 
Amekuwa muungwana kutwambia kwanini ana hasira hasira hasa linapokuja swala la kushughulika na Mbowe na kundi lake

Nilichomsifu amekuwa muwazi mbele yetu na mbele ya familia yake

Naamini Mbowe kwa kukumbuka hali ya Spika ya enzi hizo atamsamehe bure maana waliosema maskini akipata matako hulia mbwata walimaanisha vitu vingi

Hata hivyo, Ni sahihi kuwa alivyo (uonevu, hasira, ubabe) kwa kuwa tu alipitia maisha magumu na kujificha wakati wenzake wakienda likizo?

Wa aina hiyo walikuwa wengi hata miaka ya 2000 nasisi tumesoma nao sio kwamba yeye ndo alikuwa maskini wa mwisho kuliko wote
Nimekuelewa bwashee!

Lakini maskini wa miaka ya 2000 ni tofauti sana na wale wa 70s.

Pata picha Freeman kavaa Bora shoes na Job kapiga katambuga ya matairi!

Lazima uzeeni fainali patachimbika tu!!!
 
Japo ndani ya masaa 24 yajayo mh Job Ndugai atakuwa siyo Spika tena lakini ametuaga akiwa ametutegulia kitendawili.

Tuliosoma zamani tunajua namna watoto wa maskini walivyojihisi unyonge mbele ya watoto wa maofisa wa serikali achilia mbali wafanyabiashara.

Kama Ndugai hadi anaingia Chuo alikuwa bado ni maskini basi yawezekana wakati akiwa sekondari hali yake ilikuwa mbaya zaidi.
Fikiria wakati huo ndio yuko shule moja na mtoto wa mmiliki wa Mbowe Hotels iliyopo jijini Dsm lazima alijisikia unyonge mara dufu.

Na yeye Freeman watoto wa matajiri hata wakifaulu walisoma shule za private Shaban Roberts Dsm au The Highlands kule Iringa siyo kwenda kujimwambafy kwenye shule za watoto wa wakulima.

Waswahili walisema aliye juu mngoje chini ndio hiyo sasa rungu la Job limesambaratisha Ufipa yote, kisa bifu za sekondari.

Nawatakia wabunge wote vunja jungu njema usiku wa leo.

Maendeleo hayana vyama!
nichojfunza ni kutafuta pesa kwa bidii Sana umaskini ni laaana kwakweli na shida ya umaskini ndo hii roho mbaya haswa!!!!!
 
Ok Tumekuelewa.....ok tumekuelewa....

Mh.Mbowe ni kijana wa mjini mstaarabu sababu hizi hela mnazogawa gawa hovyo yeye kaziona akiwa form one, na haya ma Landcruiser yenu yeye kaishi nayo toka akiwa O'level anayasukuma!! sasa unaposema kwamba eti leo kuelewa chakali...hajitambui...unatia huruma sana mbunge...!! Hata kama ni pombe hatukatai kazijua leo Dodoma?

Ok, laah ila pole sana mbunge...ni familly Background problem....wewe ni kama mimi nilikuwa nafua nguo za wenzangu ili ka sabuni kabakie nifue za kwangu enzi za Olevel . nafikiri tutunge sheria kuthibiti hii hali..I mean famill background ni matatizo mengine ya nchi hii...

Unapata kiongozi ambaye hata hajui kujichanganya na viongozi wenzake....hasara kwa taifa...tena kubwa mno
Hapo kwa Mbowe ungemalizia alichokifanya shuleni ni nini? Ndo utalaumu background ya mtu!
 
Spika Ndugai amesema haya,

Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza wala kuota kama nitakuwa Mwanasiasa, Mbunge na hata Spika ni Mungu tu ambaye katika uumbaji wake hutujua na kutupangia safari kadri anavyoona ni vyema, asanteni sana wana Kongwa, chama changu na Rais

Nakumbuka miaka niliyosoma Shule ya Msingi nilikuwa natembea Km 16 kwa siku 1, nimekulia maisha ya shida na dhiki, nikiwa mdogo nililala kwenye kitanda cha kamba na nyumba ya tembe, lakini baadaye nimesoma vyuo mbalimbali ndani na hata nje ya nchi

Nilipokuwa chuo cha MWEKA Moshi, nilikuwa mmoja wa Wanafunzi maskini sana, baadhi ya likizo sikuwa na nauli za kurudi Kongwa, nakumbuka jinsi ambavyo wenzangu walivyokuwa wakipanda magari kuondoka mimi nilikuwa najificha kwa aibu ya kuulizwa huna kwenu?

Mimi nyumbani nilikuwa mtoto wa pekee wa Mama yangu, tunapomaliza Bunge hili natamani ni-revenge sasa nirudi akanipokee, lakini bahati mbaya Mungu alishamchukua, kwahiyo wakati mwingine mnisamehe huwa napata hasira ninapokutana na mtu mjinga

Leo nimekuja na rafiki yangu, Mama umenivumilia sana, hata nilipokuwa ICU India alikuwa analala pembeni yangu masaa 24 amekaa kwenye kiti, amekuwa Daktari wangu muda wote, hakika wewe ni mke mwema, kwa kukopa maneno ya Dk Mpango, Asante sana kwa kunipa raha.

Hilo lilifahamika mapema sana ! Ukiona mtu yeyote ana madaraka na ana roho mbaya fahamu kwamba amekulia familia duni na kapuku
 
Hakika Mungu sio mchezo kila moja anamtaja, hata awe muovu kivipi. In reality God is truly great.
 
Pongera Job Ndugai kwa kupambana hadi ukajikwamua kutoka katika Familia yenye hali Duni na Maskini
 
Spika Ndugai amesema haya,

Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza wala kuota kama nitakuwa Mwanasiasa, Mbunge na hata Spika ni Mungu tu ambaye katika uumbaji wake hutujua na kutupangia safari kadri anavyoona ni vyema, asanteni sana wana Kongwa, chama changu na Rais

Nakumbuka miaka niliyosoma Shule ya Msingi nilikuwa natembea Km 16 kwa siku 1, nimekulia maisha ya shida na dhiki, nikiwa mdogo nililala kwenye kitanda cha kamba na nyumba ya tembe, lakini baadaye nimesoma vyuo mbalimbali ndani na hata nje ya nchi

Nilipokuwa chuo cha MWEKA Moshi, nilikuwa mmoja wa Wanafunzi maskini sana, baadhi ya likizo sikuwa na nauli za kurudi Kongwa, nakumbuka jinsi ambavyo wenzangu walivyokuwa wakipanda magari kuondoka mimi nilikuwa najificha kwa aibu ya kuulizwa huna kwenu?

Mimi nyumbani nilikuwa mtoto wa pekee wa Mama yangu, tunapomaliza Bunge hili natamani ni-revenge sasa nirudi akanipokee, lakini bahati mbaya Mungu alishamchukua, kwahiyo wakati mwingine mnisamehe huwa napata hasira ninapokutana na mtu mjinga

Leo nimekuja na rafiki yangu, Mama umenivumilia sana, hata nilipokuwa ICU India alikuwa analala pembeni yangu masaa 24 amekaa kwenye kiti, amekuwa Daktari wangu muda wote, hakika wewe ni mke mwema, kwa kukopa maneno ya Dk Mpango, Asante sana kwa kunipa raha.

Ili utoboe siasa za bongo, story yako inatakiwa iwe hivi 😀😀
 
Hapendi watu wajinga lakini yeye ni mjinga. Kwa hiyo huyu alimchapa gongo la kichwa kidogo afe kwa sababu ni mjinga?
Kwa nini sasa Magufuli akamteua u DC MTU huyu mjinga. Hapo sasa finally nani ndio mjinga?

Mpigaji, mpigwaji au mteuzi?

Tumbo baba tumbo...
 
Back
Top Bottom