You are very right , Job ana inferiority complex syndrome , kwa waliosoma Goverment schools enzi hizo tunakumbuka namna watoto wa wafugaji na makabila ya pembezoni namna walivyokuwa wanakuja shule wakiwa wanyonge , mara nyingi walikuwa wanapenda kuwa wenyewe na ilikuwa ni nadra sana kujichanganya na wanafunzi wengine , kwanza hawakua na nguo nzuri zaidi ya sare , hawakua na pocket money , hawakuweza hata kukubaliwa kwenda disco [walikuwa wanachekwa hawajui kuvaaa ] ....na wengi shule zikifungwa walikuwa hawaendi kwao ......serikali ilikuwa ina sera maalum , hawa wengi walikuwa wakienda likizo ilihofiwa hawatarudi .....kwa kweli tumshukuru Mwalimu kwa kuleta usawa kama huo leo watoto waliokua wanyonge wamekua viongozi wakubwa, japo bahati mbaya wamejaa viburi
Nadharia sio lazima kuwa Job anamchukia Freeman bali tu pengine anataka kumuonyesha , maana kwa viwango Freeman alitoka familia ya kitajiri na pengine alikuwa kiongozi wa Starehe au michezo shuleni , watu wengi wajanja wajanja watoto wa dar au mjini walikuwa wana pilika za kuandaa miziki na kutoroka kwenda mjini...na watoto wanyonge kama Job walikuwa wanaonekana washamba na walijiona wanyonge mbele yao ....pengine sasa naye kapata mahali pa kumnyoosha mwenzake ...hata kama ni vyama tofauti huwezi kumfanyia mwenzako namna hiyo ..
Jakaya Kikwete naye alisoma Kibaha ila alikwa mkubwa kwao ...japo kwa viwango vyote yeye alikuwa mjanja mjanja akitokea Tanga School ....na hata walikuwa na urafiki mkubwa na mbowe kutokana na familia yao kuwa na ukumbi wa disco kuanzia Mbowe Club hadi Bilcanas ambapo Kikwete alikuwa mpenzi mkubwa hadi miaka akiwa waziri alikuwa akienda