Mambo ambayo yanaweza kukushangaza kuhusu JUICE WRLD
Kupitia nukuu ya mashairi yake kutoka kwenye kibao cha Legends yanayosema "
What's the 27 Club? We ain't making it past 21
I be goin through paranoia
So I always gotta keep the gun"
Mashairi hayo yamekuwa yakihusianishwa na kifo chake kwa madai alijitabiria kufa katika umri wa miaka 21
Ikumbukwe kuwa 27 club inawakilisha kundi la watu maarufu waliofariki wakiwa na umri wa miaka 27
Ukiachana na hiyo pia kuna mashairi tata ambayo nayo ni tragically kuhusiana na kifo chake
Kutoka kwenye wimbo wake wa all girls are the same nanukuu nashairi yake "
All this jealousy and agony that I sit in
I'm a jealous boy, really feel like John Lennon"
Sasa ili upate concept vizuri ngoja nikuongezee na nukuu hii ya mashairi kutoka kwenye wimbo wake wa "Too many"
The drug-abusers, codeine users that been hurt by women (Yeah)
I'm a drug-abusing, codeine using, modern-day John Lennon
Ukiangalia hizo nukuu mbili utagundua kuna jina la mtu limetajwa mara mbili hapo John Lennon
Huyu John Lennon ni nani?
John Lennon ni muimbaji na muandishi wa nyimbo za kingereza alizaliwa October 9 mwaka 1940
View attachment 2314536
John Lennon aliiuwawa tarehe 8 Disemba mwaka 1980
Hapo ndio kwenye pointi yangu
Juice Wrld ambaye katika mashairi yake amemtaja mara nyingi John Lennon ukumbuke naye alikufa tarehe 8 Disemba kama John Lennon, je hiyo ni coicidence?