Historia itakukumbuka Mbowe kwa kuyasaliti Mageuzi

Historia itakukumbuka Mbowe kwa kuyasaliti Mageuzi

Ndio maana nilikwambia utaitwa tu sukuma gang maana humu watu hawaamini kwenye kutofautiana mawazo.

Sioni tatizo lolote kuitwa sukuma gang, maana huo ndio uhuru wa maoni. Nyie sukuma gang original mnaeleweka.
 
Say it again.
FqtCSZoXwAAiYYk.jpg
 
Mbowe alizingua sana uchaguzi wa 2015. Watu wote serious wanalijua hili. Huwezi kumtoa kwenye kiti cha ugombea candidate ambaye amenadi sera za chama kwa miaka yote ya awali unakuja mreplace na mgombea ambaye ameshindwana na wenzake huko CCM halafu unafanya maamuzi ya pekee yako huko chumbani.

Mimi nilimdharau sana Mbowe pale na safu yake ya uongozi maana walifanya upumbavu na mzaha mkubwa sana na fursa ya upinzani kuwapiga hawa matapeli chini na kuwaondoa madarakani. Mbowe hayupo serious.

Hata sasa ukimsikiliza mambo anayoongea ni kama amelogwa. Anamwita rais kwa jina MAMA, hivi ni wapi katika katiba huwa inamwita raisi aliyepo madarakani kwa jina nje ya raisi?

At least akimaliza muda wake wa uongozi ndipo aitwe kwa majina kama Mama na kadhalika sio mama kwenye kiti cha uraisi. Mimi haya mahaba kati ya Mbowe na Samia hata siyaelewi na hapa ndipo najua kuwa Chadema haitaweza toboa katika mikono ya huyu jamaa hata iweje.
Acha uwivu wa kike ulitaka wewe ndio uitwe Mama ?
 
Sioni tatizo lolote kuitwa sukuma gang, maana huo ndio uhuru wa maoni. Nyie sukuma gang original mnaeleweka.
Nyie sukuma gang anzisheni chama chenu kwani mlitaka kuharibu chama pendwa CCM na sasa mnapiga mayowe kuhusu cdm ,achaneni na cdm hiki chama kina mwenyewe
 
Sioni tatizo lolote kuitwa sukuma gang, maana huo ndio uhuru wa maoni. Nyie sukuma gang original mnaeleweka.
Hata mimi sioni tatizo kunita sukuma gang maana naelewa humu watu hawaamini kwenye kutofautiana mawazo wao wanaamini kila mtu ni ana chama cha siasa na hakuna kuwa na mawazo tofauti kinyume na chama.

Naona sasa umenitoa kwenye sukuma gang umekaa wewe kisha umenisogeza kwenye usukuma gang halisi, hii ndio JF inaburudisha sana, karibu kwenye usukuma gang.
 
Nyie sukuma gang anzisheni chama chenu kwani mlitaka kuharibu chama pendwa CCM na sasa mnapiga mayowe kuhusu cdm ,achaneni na cdm hiki chama kina mwenyewe
Mwambie huyo sio anashobokea vyama vya watu, chama chao hadi leo kimebuma kusajiliwa.
 
Ubaya wake kwa hiyo hatua waliyofika ukimkosoa Samia moja kwa moja au kwa jambo lenye kumuhusu moja kwa moja basi inakuwa ni sawa na kutia doa huo uhusiano mzuri waliyo nao na Samia.
Huo ujumbe aliotoa hapo ni tofauti na hiki ulichoandika hapa, angekuwa anamwambia Samia kila apendacho, asingemwambia habari za Katiba Mpya.
 
Huo ujumbe aliotoa hapo ni tofauti na hiki ulichoandika hapa, angekuwa anamwambia Samia kila apendacho, asingemwambia habari za Katiba Mpya.
Katiba mpya ni kitu ambacho hata Samia mwenyewe anakizungumza hakihusiani na kumkosoa Samia na wala sijasema kwamba wamwambie kile apendacho tu bali nazungumzia ugumu wa kumkosoa Samia kwa jambo lenye kumuhusu moja kwa moja.
 
Ni rahisi sana kupiga kelele na kulalamika nyuma ya keyboard kuliko kwenda front.
 
Ni rahisi sana kupiga kelele na kulalamika nyuma ya keyboard kuliko kwenda front.
Nani aende front? Tena ningekuwa na uwezo familia yangu ningeipeleka nje huko wakaungane na familia ya Lissu,Mbowe na Lema.
 
Nani aende front? Tena ningekuwa na uwezo familia yangu ningeipeleka nje huko wakaungane na familia ya Lissu,Mbowe na Lema.
Hawa majamaa bana ,yako busy kupiga mayowe tu ,kama huyu Lema ukimuuliza shughuli yake kuu ni nini wala hajui
 
Back
Top Bottom