Historia kuhusu asili, tamaduni na aina za Wachaga

Historia kuhusu asili, tamaduni na aina za Wachaga

Ndugu wana Jf na Watanzania wenzangu

Naomba kwa makusudi kabisa nilete hii hoja mbele yenu kwa nia na makusudi mazima ya kuwasaidia baadhi ya wana Jf na Watanzania kwa ujumla walio na maswali juu ya watu wa kabila la kichaga,

Mara baada ya kuleta kwenu hili bandiko asiwepo tena wa kuleta hoja inayohusu wachaga,kwani tukiendelea kuleta hoja hizi inaonyesha ni jinsi gani kabila hili lilivyo tishio kwa makabila yote katika nchi yetu,

Ndugu Watanzania wenzangu nchi yetu ni kubwa na ina makabila mengi sana,ni kwa nini muendelee kuliandama kabila hili dogo?liliwakosea nini?tumeandamwa tangu enzi ya Mwalimu mpaka leo mnatuandama?tukatambike wapi ili tuwe huru kama watanzania wenzetu

Wachaga ni wachapa kazi na watu wasio na tabia ya kulala mpaka kieleweke,kwa maana nyingine ni kwamba wachaga ni hard workers ambao hawapimiki,ningefurahi sana kama makabila mengine yangejifunza kwa wachaga ili tuweze kujikwamua kiuchumi na tuweze kusaidia taifa letu kukua haraka

Naomba kabisa nisingependa tena kuona mambo ya wachaga yanaletwa humu kila siku kwanza mnaharibu sifa za dada zetu ambao ni wachapa kazi na big thinkers

Mkitaka kujua hilo waulizeni viongozi wenu Salmin Amoor,Benjamin Mkapa na Mhando wa Tanesco jinsi walivyopata maendeleo haraka kwa kuoa wachaga na wewe tafuta mchaga oa acha ujinga wa kudhalilisha kabila letu
mwenye kuongeza aongeze
 
@episodes,

Hujaeleweka unaongelea nini kwamba mmezuiwa kuingia ikulu au wale vijana wenu kule gereji hawapewagi hela ya kununulia spea au kwamba dada zenu ni dhulumati. Hebu funguka chalii yangu
 
Waambie hao maana kila siku Wachaga hivi mara wachaga vile eboh kwani hawana kazi za kufanya hadi waishie kutudis?
 
Owaneni nyie kwa nyie mtwangane risasi vzr nani afundishwe winzi kwa kuoa uchangani? Hivi kuna tofauti gani ya Mkikuyu wa Kenya na Mchaga? Acha kuleta comment za dharau kama hii mkuundugu yangu.
 
Unajidhalilisha Mkuu. Subiri kisa cha Ufoo Saro na Mushi kipite, ndo ulete promo hapa!!
 
Owaneni nyie kwa nyie mtwangane risasi vzr nani afundishwe winzi kwa kuoa uchangani? Hivi kuna tofauti gani ya Mkikuyu wa Kenya na Mchaga? Acha kuleta comment za dharau kama hii mkuundugu yangu.

Ekambeee!
 
na vipi kuhusu ile tabia yao ya kupenda sana pesa,wamerithishwa na mababu zao?.
 
Kabila la Wachaga linafahamika kwa wengi kuwa linapatikana mkoani Kilimanjaro. Kwa asili, Wachaga ni mchanganyiko wa Wamasai, Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe.

Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya 17. Walipofika wakiwa katika vikundi vidogovidogo waliwakuta wakazi, wenyeji kwenye Misitu ya Mlima Kilimanjaro walioitwa Wakonyingo.

Wenyeji hawa ambao huitwa Mbilikimo hawakupenda kuchanganyika na wahamiaji wageni, hivyo wakahama na kuanzisha makao yao ya kudumu kwenye misitu minene iliyopo nchini Kongo. Watu wengi wanafikiria kwamba Wachaga
wanatokana na asili moja. Ukweli ni kwamba wamegawanyika katika himaya 15, wanatofautiana kwa lafudhi, lugha, rangi na mwonekano wa miili yao. Wachaga wapo katika makundi makuu matatu ya Hai, Vunjo na Rombo.

Wale wanaopatikana eneo la Hai ni Wasiha, Wamasama, Wamachame,Wangíuni, Wakibosho, Wauru na Wamoshi. Kwa wale wanaopatikana eneo la Vunjo ni Wakirua, Wakilema, Wamarangu, Wamamba na Wamwika. Kutoka eneo la Rombo ni Wamkuu, Wamashati na Wasseri.

Hadi sasa haijulikani vizuri asili ya jina Wachaga, ila wanahistoria wanaeleza kwamba jina hilo linatokana na neno la Kiswahili linaloitwa 'Kichaka'. Inaelezwa kwamba misafara ya wafanyabiashara iliyokuwa ikiongozwa na Waswahili pamoja na Waarabu, walipokuwa wakipita maeneo ya Vunjo waliwaona wenyeji wa huko wakiwa wamejenga vibanda vya kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama waharibifu.

Wakawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi vichakani na kuanzia hapo wageni wafanyabiashara na Wamisionari walipokuwa wanakuja Kilimanjaro walielekezwa na waongozaji misafara yao kwamba wanakwenda kwenye nchi ya Uchakani, wakimaanisha kwamba kwa watu wanaoishi vichakani. Hatimaye wageni wakashindwa kulitamka vizuri
neno hili na kuliita ìUchagani, Jina hili likawekwa kwenye ramani na kuitwa nchi ya Wachaga. Hivyo ndivyo wenyeji
waliokuwa wakiishi kwenye Miteremko ya Mlima Kilimanjaro walivyopewa jina lao. Wachaga.

Maendeleo ya Wachaga

Maendeleo yao hapo awali yalitokana na zao la kahawa. Walifanikiwa kuanzisha vyama vya ushirika na hatimaye mwaka 1932 walianzisha Halmashauri ya Wachaga (Chaga Council) ambayo kwa sasa inatumiwa na Halmashauri
ya Wilaya ya Moshi. Halmashauri hii iliongozwa na Mangi Mkuu Mshumbue Thomas Marealle II.

Mwaka 1946, utawala wa Waingereza uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga. Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17 (himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo na Rombo. Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu na huduma za jamii ikiwamo uwasomesha
watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali kama Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda. Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera yake ambayo ipo hadi leo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu:

1. Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya bendera ukionyesha mandhari nzuri ya kilele cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni kielelezo cha umoja wao.

2. Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto wa bendera kuna mgomba wenye ndizi. Hiki ni chakula kikuu cha Wachaga.

3. Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni ukiwa na matunda yake. Kahawa ni zao lililowaletea maendeleo.

4. Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale' lenye matawi mawili (draceana plant). Matawi haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha Kibo, mgomba wa ndizi na tawi la zao la kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana na Wachaga wote. Ni alama ya amani. Masale hutumika katika sherehe na shughuli zote za kimila zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni kijani kibichi yanayoonyesha jinsi Kilimanjaro ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya
kila aina.

5. Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui ambaye amejipumzisha. Chui ni alama kuu ya mamlaka ya Wachaga. Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu pamoja na uharibifu wa mazingira chui hawa wametoweka.

Sikukuu ya Wachaga
Sikukuu ya Wachaga wote ilikuwa ikiadhimishwa Novemba 10 kila mwaka kama kumbukumbu ya siku ambayo Wachaga wote walipokusanyika na kumchagua Mangi Mkuu baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Uchaga. Maadhimisho ya kwanza ya mwaka 1952 yalitanguliwa na uchaguzi wa Halmashauri ya Wachaga wote kuanzia kwenye ngazi ya Uchili (kijiji), Umangi ( uchifu wa eneo) na mwisho ngazi ya baraza kuu.

Sherehe ziliadhimishwa mjini Moshi ambako Wachaga wote pamoja na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali walikusanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Uchaga (sasa ni makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya
Moshi, [Kilimanjaro District Council-KDC]) kushuhudia sherehe kubwa na yenye kusisimua sana.

Jumba la Makumbusho

Upo umuhimu mkubwa wa kuhifadhi historia ya Wachaga kama kumbukumbu sahihi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Pia, ipo haja kwa majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi pamoja na Ikulu yakarejeshwa kwa Wachaga ili yageuzwe kuwa majengo ya kuhifadhi kumbukumbu ya kabila hilo.

Katika majengo haya patahifadhiwa nyaraka zote za Chaga Council ambazo baadhi zimeshaanza kutoweka, tahifadhiwa pia shughuli za mila na kiutamaduni tangu enzi ya karne ya 18.

Halmashauri ya Wilaya ya Moshi haina budi kutafuta eneo la kujenga majengo mapya badala ya kuyatumia ya kihistoria
 
ImageUploadedByJamiiForums1402273052.004216.jpg
Mnajipa promo hadi kero
 
No source! Simply imagination. Tafuteni kitabu kinachoitwa history and life. Or east Africa through a thousand years.
 
huo mguu utakuwa ni wa mchaga kutoka mwika na rombo
 
Back
Top Bottom