Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Umeenda deep sana Mkuu wachache watakuelewa. Ila hizi tafiti na uandishi inahitajika maprofesa wa vyuo vikuu vyetu wajitafakari sana hasa juu ya nini dhima ya elimu na uwepo wao nchini.Mkubwa,
Autobiographies huwa zina tatizo la kuandika historia inayorashia rashia mambo fulani, ndiyo maana wenzetu kama Wamarekani mpaka leo wanaandika vitabu vipya kuhusu maisha ya Abraham Lincoln aliyeishi miaka zaidi ya mia mbili iliyopita.
Kitambo kidogo, zaidi ya miaka 14 iliyopita, alinitembelea rafiki yangu mmoja hapa kwangu, akaangalia maktaba yangu. Aliifurahia sana. Akakuta upande mmoja una vitabu mamia kwa mamia, angalau vitabu 500 hivi kwa hesabu za haraka. Akaniambia una vitabu vingi sana, nikamwambia hivi hapa vyote ni sehemu maalum ya biographies za marais wa Marekani tu. Akasema wewe kiboko, sasa hawa wote marais wa Marekani tu, marais wa Tanzania vipi?
Nikaona aibu sana, nikamwambia mimi nina makosa kwa sababu sijatafuta sana historia hizo za maisha ya marais wa Tanzania, lakini kuna tatizo kubwa zaidi, historia hizo hazijaandikwa sana. Nimeweza kununua vitabu zaidi ya 500 vya historia za marais wa Marekani kwa sababu vitabu hivyo vipo, sasa hivi, hata nikitaka kutafuta vitabu 500 vingine vya historia za maisha ya marais wa Tanzania siwezi kuvipata, hata nikisema tuondoe 400 kwa sababu hatuna marais wengi, nitafute vitabu 100 tu vya historia za maisha ya marais wa Tanzania, hatuna vitabu hivyo.
Kwa hivyo, nasema haya kukuunga mkono kwamba tunahitaji kuandika zaidi historia zetu. Wewe umeongelea kitabu cha Mwinyi.Nimesoma kitabu cha Mkapa nikaona hayo hayo uliyoyasema, mengi ya muhimu hayajaandikwa.
Ukisoma kitabu cha muandishi kama David McCullough "Truman" akimuelezea rais Harry S. Truman wa Marekani, alivyomchambua mwanzo mwisho, halafu ukasoma kitabu kama cha Mkapa au cha Mwinyi, utagundua kuwa vile si vitabu vya kuelezea maisha yao, zile ni documents tu za kutumika na wachambuzi kuhakiki mambo fulani katika kuandika vitabu comprehensive kuhusu maisha yao, na tunahitaji vitabu vingi kupata picha halisi. Siku hizi kuna biographies mpaka za kisaikolojia. Inawezekana kukahitajika uchunguzi wa changamoto za mtu aliyezaliwa bara, kukulia Zanzibar na kuwa rais wa Zanzibar na Tanzania, katika kuongoza Tanzania. Au kitabu cha kuelezea humility ya Mwinyi faida zake zilikuwa ni zipi, alivyowathamini watendaji wake na kuwaamini, na jinsi gani humility hiyo ilikuwa udhaifu kwa sababu aliwaachia sana wafanye watakavyo. Haya mengi mwenyewe hakuweza kuyaandika au kama aliyaandika aliyaandika kwa juu juu tu.
Unaposema wataalamu watafiti wandike, mmoja wa hao wataalam watafiti ni wewe. Hivyo tukurudishie changamoto. Si lazima iwe kitabu, hata makala ndefu tu inaweza kuwa chanzo kizuri kwa watakaokuja.
Nilikuwa naangalia mtandao wa Twitter (X), kuangalia maneno ya watu kuhusu msiba wa rais Mwinyi. Nikakutana na tweet ya dada mmoja Mtanzania anaitwa Carol Ndosi, anasema anasikitika sana alikuwa anatafuta hotuba za rais Mwinyi mtandaoni, lakini anazoziona ni chache sana.
Inaonekama kunatakiwa juhudi za kuanzisha Ali Hassan Mwinyi digital archive kama alivyoanzishiwa Salim Ahmed Salim ili wachunguzi wapate vyanzo muhimu katika kazi zao.
Hatuna vitabu vya mambo mengi sana kwa kisingizio cha watanzania hawapendi kusoma vitabu, tuhuma ambazo pia nimekuja kugundua sio za kweli.