Kwenye mapinduzi ya Zanzibar nilikuwa nimezoea zile habari za "Mapinduzi Daima" za kina Sheikh Karume na Kanali Seif Bakari mpaka Komando Salmin Amour Jumaa tulizokuwa tunaziona TVZ, baadaye nikaja kumsoma Harith Ghassany katika "Kwa Heri Ukolini, Kwa Heri Uhuru!" nikaona kuna narrative nyingine kubwa tu na tofauti. Ukweli ni kwamba pande zote zinaongeza chumvi na tunahitaji historia zaidi ziandikwe kupata uhakiki wa kutupa uhalisia zaidi.
'Mapinduzi Daima' hawakuwa na Wasomi wa ku-document. Akina Abdallah Natepe wangetusaidia sana kabla ya kuondoka. A.Babu alikuwa frustrastrated sijui kama aliacha kitu.
Mtu ambaye angetusaidia ni A.H. Mwinyi, hakuwepo kama Mwanamapinduzi lakini elimu yake ingetusaidia kama angeandika.Tatizo ni 'Uchawa' akipewa Benz kwasababu VX ni ndefu kushuka( embezzlement) ya hali ya juu sana.
Mwanae akivizia urais, Mwinyi akaona ' no good to ruffle CCM's Feathers, let the sleeping dog lie'' maktaba imeungua-SSH
Kwenye vita vya Kagera nilikuwa naongea na familia ya Jenerali Muhidini Kimario, Mzee wao alikuwa anaandika kitu, bahati mbaya alifariki kabla ile project haijamalizika sijui aliishia wapi.
Tunahitaji sana ku document haya mambo, kama si kuandika hata kuchukua video tu, hususan mazungumzo na hawa wazee ambao wengi wanatuacha kimoja na wakiondoka kuna mambo mengi hayapo hata kwenye nyaraka.
I wishi tungepata draft tu. Lt Gen Kimario ni mtu muhimu sana.
Tumemjadili sana akiwa na wenzake akina Kitete.
JokaKuu ana inputs nyingi sana za hawa veterans
Kitu ambacho sielewi na hakuna anayekieleza kuhusu Kimario ni kuhusu maisha yake baada ya Jeshi.
Hatukuwahi kumsikia akitajwa kama CoS au kukaribishwa katika shughuli kama tunavyoona wengine.
Msiba wa Kimario haukuadhimishwa kulingana na hadhi yake na mchango wake katika Taifa
Je, Kimario alikuwa disgruntled kwasababu u-CDF ulimpitia pembeni akijua kwamba alikuwa qualified sana?
Je, ni kwasababu alikuwa na influence sana JWTZ
Je, ni kwa kauli yake kuhusu 'vijana wetu kuuawa msumbiji kwa ugomvi wa ndugu'
Kwa mfano, nani kaandika kuhusu urais wa Kikwete na Mkapa extensively? Vipi kuhusu wa Magufuli? Tunatakiwa tuandike mambo mapema wakati kumbukumbu zipo na ushahidi haujaharibika bado.
Hakuna! Si wasomi au '' investigative journalism''